Pamoja sanaWewe ni mwamba sana Vintage1q. Mungu aendelee kukupigania kaka.
Bila shaka, kuwa huruSamahani vipi nikiamua kuitengenezea movie
Amina!Story inaumiza sana, pole sana mkuu kwa mtiani mzito sana mungu akufanyie wepesi
Ukiwa na huo uthubutu, unaweza kuniambia nikakuongezea mambo mengine mengi ambayo sijaandika hapa kazi yako ikawa nzuri.Samahani vipi nikiamua kuitengenezea movie
Man utakua tajiri na kiongozi mkubwa sana!Sehemu ya saba
Baada ya kunicheka aliniuliza kama ananitumia kwa ile namba. Akatuma elfu 10 na kisha akanitumia ujumbe kwamba yupo na mpenzi wake kwahiyo nisiwe nampigia simu. Nilimshukuru na kumtakia maisha mema. Nilimuomba anisaidie nyaraka zangu za kitaaluma na akanielekeza sehemu ambapo nitazipata.
Nipokea nyaraka zangu. Wakati huu nilikuwa nimechoka. Nilikonda na kuwa mtu wa ajabu kabisa. Kutoka kuvaa suti karibia siku tano za wiki na kufikia kuwa katika mavazi machafu yasiyoelezeka. Nilivaa ndala zilizofungwa na kamba.
Wakati fulani nikiwa katika mawazo mazito, niliamua kutaka kujiua lakini kwanza nikatafuta simu niongee na mtoto wangu niliezaa na Upendo. Mtoto wangu alinisalimia kisha akaniambia kwamba, "Dad, you promised to come back for me. Please remember that I miss you". Nililia sana siku ile na nikaamua kuendelea kupambana.
Nitawataja watu wachache hapa maana najua ni kwa nia njema. Wakati nahangaika, nilitafakari kukutana na kaka yangu mmoja hapa JF. Sikuwahi kuwasiliana nae kabla lakini moyo ulinisukuma kuongea nae. Nilitamani anisaidie viatu ili nipate kwenda kwenye sehemu moja ambayo nilialikwa kwa ajili ya interview. Nilimu-pm akaniomba tuonane kibada. Nilitembea kutoka rangi tatu hadi kibada kwa mguu.
Ilikuwa bahati mbaya maana siku ile hakunipa viatu kama nilivyoomba. Alinitazama kisha akanipa elfu 10. Nilikuwa na njaa sana. Nilikuwa sijapata chakula kwa muda mrefu. Nilitumia ile pesa kiasi kupata chakula pale kibada. Baada ya kuwasiliana tena, aliniomba nifike kibaha. Nilitembea tena kwa mguu hadi kibaha. Nilichoka sana. Alinipa nguo pamoja na viatu. Brother Jr., asante sana na Mungu akubariki.
Nilikuwa na jamaa yangu mwingine yupo humu anaitwa clearmind. Nilisoma nae na alikuwa mtu wangu wa karibu sana. Nakumbuka kipindi anataka kunisaidia aligombana sana mchumba wake na kwa bahati mbaya wakaachana. Niliumia sana nikaogopa kuendelea kumuomba msaada.
Nilipona msongo wa mawazo. Nipo Dar napambana. Sipo kama nilivyokuwa japo hali bado ni ngumu sana. Nina imani nitarejea tena upya. Yaliyotokea yote katika maisha yangu nayaangalia kama changamoto mpya zinazonijenga kuelekea kwenye hatima yangu iliyo njema zaidi. Nimejisikia amani kushea nanyi safari yangu hii ambayo imekuwa na matukio mengi ya kuumiza. Asanteni sana na Mungu awabariki.
Vintage1q.
Enjoy your life to the fullest today because tomorrow's never promised!
Amina mtu wa BabaMan utakua tajiri na kiongozi mkubwa sana!
Hope tutakuja kufanya KAZI office Moja na tutakua team wazalendo!
Nadhani utaniunga mkono kwenye dhamira yangu ya kupunguza mapesa mengi kulipa wanasiasa mishahara na maposho kibao wakati huduma za kijamii zinalega lega!!
Paulo mtume anaandika"najua kushiba na kuona njaa" akielezea Kwa kina mapito yenye maumivu meengi!
Tunapitia nyakati kama hizo maishani ili tukipata tuelewe Hali zote wanazopitia watu wote Ili tuwe msaada!!
See you at the top!! Trust me nitakutafuta ngoja kwanza litimie neno fulani!!
Yasinta aliondoka nayo yoteDah wanawake ni hatari kuliko bomu la nuclear,,,,,
Mkuu kuna kitu sijaelewa vizuri,,,
Kuhusu Pesa uliyoikusanya kwa ajiri ya kuja kujiajiri dar es salaam, umeandika uliiweka kwenye sanduku la chuma, natamani kujua ilikuwa kama kiasi gani? Na Yasinta ndio aliondoka nayo akaemda kwa huyo mpenzi wake???