Maisha ya mwanafunzi

Nov 2, 2020
68
90
Kipindi cha kuwa mwanafunzi,Ni kipindi muhimu sana unachoweza pitia katika ngazi tofauti za Kitaaluma.

Wakati mwingine kwa mwanafunzi huwa na shauku ya kutaka kuhitimu ili tu ayafikie malengo yake,Ikiwemo kuingiza kipato au hata kuisadia familia juu ya mambo kadha yanayoisumbua.

Kuwa na haraka juu ya kutoa msaada si tatizo, ila shida ni pale mtu unapolazimisha hali iwe ndivyo sivyo.

Usipokuwa na tafsiri halisi inayokueleza wewe ni nani na umetoka wapi, pasi na shaka unaweza jikuta unaangukia kufuata mkumbo wa maisha yasiyo ya kwako.

Baadhi ya wanafunzi leo wanatamani kujitoa katika maisha ya maigizo ya mavazi, chakula au hata malazi yasiyoendana na uhalisia wa maisha yao ya kweli, lakini bado hawajapata nini cha kufanya ili kujinasua kwenye mtego huo.

Wengine wamezongwa na wimbi la kujiingiza kwenye mapenzi wasiyo na kifua cha kuyahimiri,Matokeo yake ni kuumizwa na kubaki na majuto,kuacha masomo au hata kuua kwa wale wanaoshindwa dhibiti hasira zao.

Ili kutoingia katika baadhi ya athari tulizozitaja katika maisha yako ya uanafunzi, amua sasa kuwa na tafsiri inayokueleza wewe ni nani,Kiasi hata kama kuna mtu nje anakucheka juu ya kile unachokifanya, utabaki ukimtazama kwa kuwa ni yeye ndie wa kuchekwa kwa kutojua ipi dhamira yako katika maisha.

Kesho yako ni matokeo ya leo, ambayo inatengenezwa na wewe kwa msaada wa Muumba.

Youth Worker

Hardness,Teaches
 
....
9b7d929a33e943ea9b42aa13b3883056.jpg
 
Back
Top Bottom