Maisha ya connection yanatutesa vijana.

Maisha ya connection yanatutesa vijana.

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
5,104
Reaction score
14,029
Connection ni conspiracy yenye lengo la kuhakikisha masikini anabaki masikini na tajiri azidi kupeta. Kwa kifupi huu ni mpango wa kishetani ambao inabidi upigwe vita kwa nguvu zote. Madhara yake ni.
1. Elimu kuchukuliwa poa.
2. Kutengeneza matabaka masikini na tajiri(class)
3. Undugulazition makazini.
4. Kutokuwa na ubunifu makazini sababu kigezo cha kuajiriwa kinakuwa ni undugu
5. Na madhara makubwa kabisa ni VITA za wenyewe kwa wenyewe.

Kiukweli vijana tuliokosa connection tunaumia sana kwa yanayoendelea kwenye ajira na sio kwamba hatuna uwezo hapana Bali uwezo tunao kuanzia darasani(vyeti) mpaka uwezo binafsi ila connection tu ndo inatufanya tuonekane hamnazo.

Tanzania ni yetu sote kama jamii tupinge ubaguzi unaofanyika kwenye ajira.
 
Duuh
500_F_232674998_hwr987y4WSqcdch9KjOxR0bgD6gUbBw9.jpeg
 
Connection ni conspiracy yenye lengo la kuhakikisha masikini anabaki masikini na tajiri azidi kupeta. Kwa kifupi huu ni mpango wa kishetani ambao inabidi upigwe vita kwa nguvu zote. Madhara yake ni.
1. Elimu kuchukuliwa poa.
2. Kutengeneza matabaka masikini na tajiri(Racist)
3. Undugulazition makazini.
4. Kutokuwa na ubunifu makazini sababu kigezo cha kuajiriwa kinakuwa ni undugu
5. Na madhara makubwa kabisa ni VITA za wenyewe kwa wenyewe.

Kiukweli vijana tuliokosa connection tunaumia sana kwa yanayoendelea kwenye ajira na sio kwamba hatuna uwezo hapana Bali uwezo tunao kuanzia darasani(vyeti) mpaka uwezo binafsi ila connection tu ndo inatufanya tuonekane hamnazo.

Tanzania ni yetu sote kama jamii tupinge ubaguzi unaofanyika kwenye ajira.
Acha mambo ya kulia lia. Hakuna cha connection. Serikali inatangaza ajila na watanzania wote wanaomba na mchujo, interview na selection zinafanyika kulingana criteria na vigezo. Wee kalia kuti na mkeka wa bibi na kulalamika eti kuna upendeleo. Mengine masikini wamefungwa na ujinga wa kutojiamini, kukosa hata 1000 ya kuingia internet na kufanya application au kutype na postal charges za barua, kuzungukwa na masikini wanakujaza ujinga wa kimasikini, kulogana, n.k. pambana struggle for existence and survival for fittest!
 
Kujiajiri akuhitaji connection ni kitambulisho tu cha machinga pale kwa mkuu wa wilaya.
 
Nakubaliana na wewe. Kiufupi inabidi tubadilike sio tu kuangalia viongozi/serikali. Kuna masuala yanaanzia kwenye jamii zetu yaani ngazi ya familia
 
Connection ni conspiracy yenye lengo la kuhakikisha masikini anabaki masikini na tajiri azidi kupeta. Kwa kifupi huu ni mpango wa kishetani ambao inabidi upigwe vita kwa nguvu zote. Madhara yake ni.
1. Elimu kuchukuliwa poa.
2. Kutengeneza matabaka masikini na tajiri(Racist)
3. Undugulazition makazini.
4. Kutokuwa na ubunifu makazini sababu kigezo cha kuajiriwa kinakuwa ni undugu
5. Na madhara makubwa kabisa ni VITA za wenyewe kwa wenyewe.

Kiukweli vijana tuliokosa connection tunaumia sana kwa yanayoendelea kwenye ajira na sio kwamba hatuna uwezo hapana Bali uwezo tunao kuanzia darasani(vyeti) mpaka uwezo binafsi ila connection tu ndo inatufanya tuonekane hamnazo.

Tanzania ni yetu sote kama jamii tupinge ubaguzi unaofanyika kwenye ajira.
Racist kama ulivyoitaja kumaanisha Racism wala si mfumo wa kimatabaka kwa misingi ya kipato, huo ni mfumo wa ubaguzi kwa misingi ya rangi au asili ya mtu anapotokea....
 
Acha mambo ya kulia lia. Hakuna cha connection. Serikali inatangaza ajila na watanzania wote wanaomba na mchujo, interview na selection zinafanyika kulingana criteria na vigezo. Wee kalia kuti na mkeka wa bibi na kulalamika eti kuna upendeleo. Mengine masikini wamefungwa na ujinga wa kutojiamini, kukosa hata 1000 ya kuingia internet na kufanya application au kutype na postal charges za barua, kuzungukwa na masikini wanakujaza ujinga wa kimasikini, kulogana, n.k. pambana struggle for existence and survival for fittest!

We jamaa itakuwa huishi bongo au ni miongoni mwa watu waliokonektiwa kwenye baadhi ya vitengo nyeti nchini
 
Connection ni conspiracy yenye lengo la kuhakikisha masikini anabaki masikini na tajiri azidi kupeta. Kwa kifupi huu ni mpango wa kishetani ambao inabidi upigwe vita kwa nguvu zote. Madhara yake ni.
1. Elimu kuchukuliwa poa.
2. Kutengeneza matabaka masikini na tajiri(Racist)
3. Undugulazition makazini.
4. Kutokuwa na ubunifu makazini sababu kigezo cha kuajiriwa kinakuwa ni undugu
5. Na madhara makubwa kabisa ni VITA za wenyewe kwa wenyewe.

Kiukweli vijana tuliokosa connection tunaumia sana kwa yanayoendelea kwenye ajira na sio kwamba hatuna uwezo hapana Bali uwezo tunao kuanzia darasani(vyeti) mpaka uwezo binafsi ila connection tu ndo inatufanya tuonekane hamnazo.

Tanzania ni yetu sote kama jamii tupinge ubaguzi unaofanyika kwenye ajira.

Habari ya kupata kitu kwa connection inaweza kuwa nzuri au mbaya. Kwenye kazi tunaaswa kutengeneza "professional network", kujuana na watu tutakaoweza kusaidiana nao kitaaluma, kibiashara na kadhalika.

Jambo hili likifanywa kwa nia na njia nzuri, si jambo baya. Maisha hayawezi kuepuka kabisa connection.Kuna watu uliosoma nao, ulioishi nao, uliokua nao, unawajua vizuri.Ukiwa na nafasi ya kufanya kitu unaweza kuwafikiria zaidi kuliko watu ambao huwajui.Hususan nakusudia kuzungumzia watu wenye sifa.

Tatizo linakuja pale connection ndiyo inayokuwa sifa kubwa inayoangaliwa, hata mtu hana sifa anapewa pande kwa sababu ana connection tu.

Hapo tunaharibu kazi.

Katika kitabu chao wasomi wa uchumi Daron Acemoglu (MIT) na James A Robinson (Chicago) "Why Nations Fail: The Origins of Power, Prosperity and Poverty" wamechambua sana sababu nyingi zinazofanya nchi nyingine ziwe masikini na nyingine ziwe tajiri.

Sababu walizozitaja ni nyingi, na chambuzi zao ni ndefu na za kisomi sana kwa mimi kuzifupisha hapa, hivyo kufaidika kabisa kama hujasoma kitabu, kitafute. Ila kitu kimoja kikubwa kabisa walichoandika ni kwamba, nchi zinazokuwa masikini mara nyingi zinakuwa hivyo kwa kuwa na mfumo wa watu kupata fursa kwa connections.

Mfumo huu una tabia hizi.

1. Unapendelea watu kwa connection, si kwa uwezo.
2. Kwa sababu ya 1 hapo juu, unanyima watu wenye uwezo fursa
3. Watu wenye uwezo wakinyimwa fursa, na wasio na uwezo wakipewa fursa kwa upendeleo, mfumo mzima wa uchumi unadorora.
4. Kupendelea watu kwa connections tu, bila kuangalia sana uwezo, kunafanya watu wengi waone kuwa na uwezo hakuna maana na hivyo kutokuwa na nia ya kuwa na uwezo zaidi. Kama watu wanapata kazi kwa kujuana, na wewe hata usome mpaka Ph.D utaachwa tu, watu wengi ambao hawana connection wataona hakuna haja ya kuongeza uwezo.
5. Kupendelea watu kwa connection bila kuangalia uwezo kunaleta matabaka ya walio ndani ya mfumo na walio nje, walio nje wakijiona wametengwa sana, watauhujumu mfumo uanguke ili "malaika waishi kama mashetani..."
6. Mfumo huu unawanyima hata watu ambao wana connections fursa za kujiendeleza zaidi, kwa kuwa wengi wanabweteka kwa kuona hakuna haja ya kujiendeleza kama wanachohitaji ni connections tu. Hata ambao wangeweza kuwa na uwezo zaidi wanabweteka.
7. Mfumo huu unatengeneza matajiri wachache wenye hela nyingi na masikini wengi wanaopigania "hela ya kula". Kiuchumi hii ni hali mbaya, kwa sababu uchumi unategemea sana mzunguko wa fedha unaofanywa na watu wengi. Kama fedha zimefungiwa kwa watu wachache, hazizunguki, uchumi wa nchi utadorora.
8.Mfumo huu ukiendelea sana, under ceteris paribus, unakuja kuzaa maisha mafupi, magonjwa, umasikini, vifungo vya jela zaidi, kukosa elimu, matatizo ya afya ya akili, mimba za utotoni na mapinduzi ya nguvu ya kijamii.
9. Mfumo huu husababisha kutowiana kimilinganyo kwa kiuchumi miongoni mwa jamii (social and economic inequality)
10. Hatima ya mfumo huu ni kwamba hauna manufaa hata kwa wale ambao mwanzoni huwa wananufaika nao. Ndiyo maana matajiri wakubwa wenye akili kina Bill Gates na Warren Buffet wanafanya juhudi za kupunguza inequality.

Binafsi nilikuwa napiga vita sana mfumo huu, ambao nilivyoanza kazi Tanzania ulikuwa umeshika moto.

Kiasi kwamba, nilivyopata kazi yangu ya kwanza, watu wote walianza kuniambia "Mzee (baba yangu) kakuunganishia eeh". Wakati yeye alikuja kuambiwa baada ya mimi kupata kazi.

Nikaona isiwe tabu.

Nikajikata Marekani ambako hanijui mtu na kazi nitakayofanya itatokana na mimi kusimama mwenyewe, wala hakuna mtu wa kuniambia "Mzee kakuunganishia eeh"
 
Kujiajiri akuhitaji connection ni kitambulisho tu cha machinga pale kwa mkuu wa wilaya.
Hivi una habari wewe na mwenzako wote mnaweza kujiajiri lakini kama mwenzako ana connection huko kwenye taasisi za umma na wewe ukawa hauna yeye akafanikiwa mapema kuliko wewe?
 
Acha mambo ya kulia lia. Hakuna cha connection. Serikali inatangaza ajila na watanzania wote wanaomba na mchujo, interview na selection zinafanyika kulingana criteria na vigezo. Wee kalia kuti na mkeka wa bibi na kulalamika eti kuna upendeleo. Mengine masikini wamefungwa na ujinga wa kutojiamini, kukosa hata 1000 ya kuingia internet na kufanya application au kutype na postal charges za barua, kuzungukwa na masikini wanakujaza ujinga wa kimasikini, kulogana, n.k. pambana struggle for existence and survival for fittest!
Hapo kwenye ajila unamaanisha ajira?
 
Connection ni conspiracy yenye lengo la kuhakikisha masikini anabaki masikini na tajiri azidi kupeta. Kwa kifupi huu ni mpango wa kishetani ambao inabidi upigwe vita kwa nguvu zote. Madhara yake ni.
1. Elimu kuchukuliwa poa.
2. Kutengeneza matabaka masikini na tajiri(class)
3. Undugulazition makazini.
4. Kutokuwa na ubunifu makazini sababu kigezo cha kuajiriwa kinakuwa ni undugu
5. Na madhara makubwa kabisa ni VITA za wenyewe kwa wenyewe.

Kiukweli vijana tuliokosa connection tunaumia sana kwa yanayoendelea kwenye ajira na sio kwamba hatuna uwezo hapana Bali uwezo tunao kuanzia darasani(vyeti) mpaka uwezo binafsi ila connection tu ndo inatufanya tuonekane hamnazo.

Tanzania ni yetu sote kama jamii tupinge ubaguzi unaofanyika kwenye ajira.
Mimi kinachoniuma zaidi Ni kwamba wengi walioingia kwenye maofisi mbalimbali ni mambulula.
Yaani mtu unakwenda kwenye ofisi kutaka huduma unawauliza maswali jinsi wanavyojibu Kama watoto wa darasa la 5.
Hapo ndio huwa nakasirika Hadi nakuwa mbogo na maswali yangu yanauzi kwa mtu ambaye ni kilaza atajihisi Kama namkejeli kwa ukilaza wake.
 
Mkuu hizo ni dharau za pesa au za kuzaliwa nazo.
 
Racist kama ulivyoitaja kumaanisha Racism wala si mfumo wa kimatabaka kwa misingi ya kipato, huo ni mfumo wa ubaguzi kwa misingi ya rangi au asili ya mtu anapotokea....
Mkuu hizo categories zote za kiubaguzi zipo wala usikatae.
Kwa mfano watoto wanaoishi masaki au mbezi beach automatically anakuwa na connections nyingi ukilinganisha na watoto wa tandika, gongolamboto,tandale hata Kama wote ni wa kabila moja.
 
Mimi kinachoniuma zaidi Ni kwamba wengi walioingia kwenye maofisi mbalimbali ni mambulula.
Yaani mtu unakwenda kwenye ofisi kutaka huduma unawauliza maswali jinsi wanavyojibu Kama watoto wa darasa la 5.
Hapo ndio huwa nakasirika Hadi nakuwa mbogo na maswali yangu yanauzi kwa mtu ambaye ni kilaza atajihisi Kama namkejeli kwa ukilaza wake.
Huduma mbovu na kauli za ajabu kwenye maofisi afu ndo wanaongoza kuharibu goodwill za taasisi nyingi.
 
Connection ni conspiracy yenye lengo la kuhakikisha masikini anabaki masikini na tajiri azidi kupeta. Kwa kifupi huu ni mpango wa kishetani ambao inabidi upigwe vita kwa nguvu zote. Madhara yake ni.
1. Elimu kuchukuliwa poa.
2. Kutengeneza matabaka masikini na tajiri(class)
3. Undugulazition makazini.
4. Kutokuwa na ubunifu makazini sababu kigezo cha kuajiriwa kinakuwa ni undugu
5. Na madhara makubwa kabisa ni VITA za wenyewe kwa wenyewe.

Kiukweli vijana tuliokosa connection tunaumia sana kwa yanayoendelea kwenye ajira na sio kwamba hatuna uwezo hapana Bali uwezo tunao kuanzia darasani(vyeti) mpaka uwezo binafsi ila connection tu ndo inatufanya tuonekane hamnazo.

Tanzania ni yetu sote kama jamii tupinge ubaguzi unaofanyika kwenye ajira.
Miaka kadhaa iliyopita enzi ya utawala Wa JK( awamu ya NNE) nikimshauri kijana wetu baada ya kumaliza degree yake ya BAF, nilimwbia aamdike barua na kuzisamabaza kwenye mabenki, alifanya kama milivyomuagiza, Alifanya na zaidi, aliandika barua za Maombi ya kazi mabenki yote, alimwandikia na mpemzie,
Aliitwa kwenye benki 2, akifanya Interview benki moja akapata kazi, na mwenzie aliitwa benki moja akafanya Interview naye akapata kazi kwenye hiyo Benki. Wakaoana na maisha yakaendelea.
Baadaye akaomba kazi sehemu nyingine akaitwa Interview. Tukakutana kwenye Panel kila mtu kaja kivyake, baadaye akapata hiyo kazi kwa nguvu zake mwenyewe japo nilikuwa kwenye Panel sikufanya chochote.
 
Back
Top Bottom