Maisha Tanganyika ni magumu kuliko nchi zote Afrika Mashariki na Kati

tpmazembe

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
2,470
1,225
Kodi wanayotozwa watanganyika ni serikali katili inayojipa jina Tanzania ni kodi kubwa sana, imepelekea kufikia watanganyika hao kwenda nchi nyiingine ya zambia kununua mafuta(fuel) ambayo mepitia bandari ya dar wameweka kodi na bado ni nafuu. Imepelekea watanganyika hao kwenda nchi nyingine kama zanzibar kununua mafriji au magari yaliyotoka nje lakini bei nafuu zaidi ya nusu ya bandari ya dsm.huu ni huzuni mkubwa watu wanachajiwa kodi kubwa. Imepelekea mpaka watu kwenda nchi ya malawi kununua sukari angali tunavyoviwanda vingi na mashamba mengi ya miwa yote hiyo ni kodi kuwa.Imepelekea wafanya biashara kwenda nchi ya uganda kwenda kununua nguo ambazo wao wamenunua ulaya na kupitisha kwenye bandari yetu na kutulipa na kuweka kodi yao lakini bado bei zao ziko chini kuliko za hapa kwetu kisa kubebeshwa zigo la kodi kwa wananchi.Imefikia mahali sasa mpaka watanganyika akina mama kwenda kununua chumvi kenya kama tunavyowaona kule himo wakikimbia kwenye mpaka wa taveta walau kusave vijisent fulani tunavyobebeshwa kwa zigo la kodi wanalotafuna viongozi wa serikali ambao ni ccm.

Hali ni mbaya wananchi wamegeuzwa watumwa ndani ya nchi yao.Je huu ndio uhuru uliopiganiwa na wazee wetu?
 

tpmazembe

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
2,470
1,225
ndio maana afrika wananchi huamua kuingia msitumi kwa sababu ya mambo kama haya. hospital hakuna panadol lakini viongozi waliopewa dhamana wanakwenda kuficha mabilioni uswis wanakuja kuchangisha wananchi vi laki kazaa vya kujenga darasa.huu ni upuuzi wa viongozi kwa africa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom