GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,645
- 10,867
Huenda hili tatizo halipo kwa ndugu zetu Wazanzibar. Pengine, imani ya kidini inaweza ikawa imewasaidia kuondokana na fikra za kutendeana kwa hila.
Hali si shwari Kwa upande wa Tanganyika. Imefikia hatua watu wengi hawaamini kupata haki zao bila kufanya jambo la ziada, kutoa rushwa.
Kama unataka kumhamisha mtoto kutoka shule moja ya Serikali kwenda shule nyingine ya Serikali, unaweza ukazungukia shule zote Tanzania na bado usifanikiwe. Lakini "ukiongea" vizuri na "mkubwa" wa shule, unaweza ukapata nafasi hata kwenye shule iliyoweka bango "HAKUNA NAFASI"
Kwenye ajira nako kizumkuti. Mtu anaweza akawa na sifa zote lakini asipotanguliza "chochote", anaweza akaishia kuwa msindikizaji wa wanaoajiriwa. Labda kama mfanya maamuzi ya wanaostahili kuajiriwa siyo Mtanganyika, japo si Watanganyika wote pia wana roho mbaya.
Juzi nilikutana na kisanga cha aina yake iliyonipa picha jinsi hali ilivyo mbaya. Nilifuatwa na mtu mmoja aliyetaka nimsaidie kupata kazi mahali fulani.
Aliniambia angenipa kiasi cha fedha nitakachomwambia, au mshahara wa kwanza. Angeniachia vyeti vyake viwe dhamana, nikae navyo mpaka siku atakapoitimiza ahadi yake, kunipa mshahara wake wote wa mwezi mmoja.
Aliponiona nimeshtushwa na alichoniambia, aliamua kunisimulia kilichomsukuma kuchukua huo uamuzi. Alihitimu Chuo mwaka 2015. Lakini wenzake ambao amekuwa akiomba nao kazi, tena wengine wakiwa wamehitimu Chuo baada ya yeye kuhitimu, wamekuwa wakifanikiwa kwa sababu ama wanafahamika na wafanya maamuzi au wanatoa "kitu kidogo". Kwa hiyo naye aliamua kutembea na hiyo mbinu, kununua ajira.
Nilishawahi kuambiwa na mtu mwingine kuwa nikimfanyia mpango wa kupata kazi, angenipa sehemu ya mshahara wake kwa miezi kadhaa.
Hiyo roho mbaya imetoka wapi? Imefikia hatua Watanganyika wanaamini, linapokuja suala la kazi, watatendewa haki tu endapo msimamizi atakuwa Mzungu au Mchina. Tunaipeleka wapi nchi yetu? Tunaridhisha tabia gani kwa vizazi vijavyo?
Kuna makampuni ambayo ili mtu apate kazi ya udereva, anatanguliza kwanza kiasi fulani cha pesa kwa HR.
Mwingine aliitiwa kazi ya "uoperator" kwenye kwenye mgodi wa Wachina. Lakini kwa kuwa Wasimamizi walikuwa Watanganyika wenzake, alipewa sharti la kutoa sh 300,000/= ili apate kazi. Hakuwa tayari kuhonga kwa hiyo naye hakupata kazi kwenye hiyo kampuni.
Kazi imeshakuwa ya kuuzwa?
Hali ni tete! Haipendezi kunyanyasana kiasi hicho. Ni vibaya sana kutumia nafasi yako kuwaumiza wengine. Kuomba rushwa ni kuwaumiza wenzako. Mabadiliko yanahitajika.
Hali iliyopo ilisababishwa. Na mabadiliko nayo hayatajileta yenyewe. Lazima yasababishwe.
Mabadiliko yanawezekana endapo nia itakuwepo.
Swali ni kwamba ni kwa namna gani na lini tutayafikia hayo mabadiliko?