Vitalis Msungwite
JF-Expert Member
- May 11, 2014
- 3,269
- 7,771
Binafsi, ni mtumiaji mzuri sana wa mitandao ya kijamii. Kwa muda mrefu toka 2012 nilipoanza kutumia sim zenye uwezo wa internet hata ya 2G tu, nimejikuta kwenye ulevi mkubwa.
Hayapiti masaa kadhaa bila kuchungulia chungulia ili kujua Dunia inaendaje. Lakini, kuna kipindi nilitingwa na shughuli fulani na ilinilazimu kutumia sim ndogo kwa muda wa wiki moja.
Ndani ya hiyo wiki, nilihisi kukosa mengi yanayoendelea Nchini na Duniani kwa ujumla. Nje ya hilo niliishi maisha ya raha mustarehe, huku kichwa kikiwa huru kabisa.
Unajua ukiwa offline, unapata wasaa wa kuwa na marafiki na mnapiga stori zinaeleweka. Vile vile unashiriki kwenye makundi katika michezo mbali mbli, Mimi ni draft tu. Wananchi wanapiga kazi kama kawaida tu na life linasonga.
Sasa ukiwasha data sasa!!, unaweza kuhisi tofauti. Huyu, "uchumi unaporomoka kwa kasi ya kimbunga Kenneth", mwingine anajibu "uchumi unapanda kwa kasi ya Catrina". Mara Manji aliuawa, wapinzani wamekamatwa, gwajima hivi, Wasiojulikana wajulikana, magufuli aongezwe muda wa kuongoza, korosho zimehujumiwa, CAG na spika wanamgogoro, Masele kaitwa kule, waziri ajivue, Biashara zimekufa, Biashara zimeimarika, Mabeberu yamesanda kwa Anko, kuna mkuu katenguliwa uteuzi n.k.
Hata Mange na wafuasi wake walipowasha data waliona maandamano yanatekelezeka, lakini walipozima data na kuingia mtaani walikuta watu wapo na hamsini zao.
Makolokolo kibao unakutana nayo mpaka unahisi tumefika mwisho wa Dunia. Lakini hakuna kipindi kizuri kama ukizima data, trust me utaona maisha yalivyo ya raha.