Kwanza nampa POLE. Ila pia kwa yule ambaye alikuw na uwezo wa kununua loti, basi alikuwa ameshajipanga kimaisha kwa yanayofuata.
So, anasikitika kupoteza lori, japo naamini alikuwa amelikatia BIMA, so kapata maumivu, japo yatapunguzwa kidogo na bima aliyokata.
Ugumu wa maisha, muwazie mama ambaye anapanga nyanya, na vitunguu barabarani na bado anasomesha, hata uwezo wa bodaboda hana. Muwazie mzee anayepita njiani nauza manati (wapo, binafsi nakutana nao), huwa nabaki kuwaza HIVI KWA WIKI ANAWEZA AKAUZA MANATI NGAPI..??
So, mwenye uwezo wa kununua lori, HUYO TAYARI AMESHAJIPANGA KIMAISHA. Narudia tena NAMPA POLE, ila nyuma yake wapo wengi sana wenye shida nyingi sana kuliko yeye. Ambao kwao wanatamani wawe na genge la kupanga bidhaa zao hata mtaani kwa sababu USHURU WA SOKONI, hawawezi kulipa...!!!