Maisha ni fumbo lichoshalo akili

Maisha ni fumbo lichoshalo akili

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,980
Reaction score
831,550
Wenye Chakula hawana appetite (hamu ya kula) na wenye appetite hawana chakula. Wenye majumba ya kifahari wanakosa usingizi, na wenye usingizi wa kutosha hawana hata pakulala. Wagonjwa mahututi wanaomba uzima, wazima wa afya wanajiua.

Wagumba wanalilia watoto, wasio wagumba wanatoa mimba na kutupa watoto chooni. Wenye mialiko mingi hawana nafasi ya kwenda na wenye nafasi hawana mialiko.

Wasio na kope wamejikubali kama walivyo, wenye kope wanavaa za bandia. Anayepewa upendo hauthamini asiyependwa analilia upendo.

Wenye amani wanaomba vita na kutishia machafuko, wenye vita wanalilia amani.

Mwenye nafasi ya kusoma na ada analipiwa hataki shule wala haitilii maanani, mwenye kiu ya kusoma hana ada.

Ni kama binadamu hajui anachokitaka hivyo hata akipata alichodhani anataka bado haridhiki kwani sicho hicho anachotafuta.

CHA KUSHANGAZA

1. Hicho unachokidharau Leo ndicho kilikuwa kinakuliza jana na kukunyima usingizi.

2. Hayo unayotafuta Leo pia kesho hayatakuwa na mashiko kwako.

MAISHA NI FUMBO LILILOSHEHENI VIFUMBO* KAMA MFALME SULEIMAN ALIVYOSEMA " *TUNAFUKUZA UPEPO"* ambao hatutakaa tuukamate!!

SHUKURU KWA UHAI. VINGINE VYOTE VINATHAMANI USIPOKUWA NAVYO, UKIVIPATA THAMANI YAKE INAISHIA HAPO. HIVYO USIRUHUSU VIKAKUTAWALA

Niwatakieni maisha mema

NA MUWE NA WEEKEND NONO HUKU MKILITAFAKARI FUMBO HILO
 
Brother mshana umemaliza kila kitu! Nilichojifunza ni kuthamini ulichonacho lakini pia ukikosa chochote kilicho nje ya uwezo wako usifadhaike moyo maisha ni haya haya tunayoyaishi leo. Asante sana
 
Brother mshana umemaliza kila kitu! Nilichojifunza ni kuthamini ulichonacho lakini pia ukikosa chochote kilicho nje ya uwezo wako usifadhaike moyo maisha ni haya haya tunayoyaishi leo. Asante sana
Sahihi kabisa
 
Wanatamani cdm ishike dola,kesho watatamani tlp nayo ishike dola..kesho kutwa cuf nayo ishike dola...ndo binadamu tulivyo.
 
*Ni kama binadamu hajui anachokitaka hivyo hata akipata alichodhani anataka bado haridhiki kwani sicho hicho anachotafuta.*
Kuna swali tulishaulizwa na lecturer wa philosophy and social ethics kwamba
Is human ultimate happiness is attainable?
Dah ...yaani mwanadamu ni complicated Sana
 
Back
Top Bottom