Maisha Ndani Ya Umasikini Ni Darasa Tosha

Maisha Ndani Ya Umasikini Ni Darasa Tosha

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
274
Reaction score
486
MAISHA NDANI YA UMASIKINI NI DARASA TOSHA.

Kuna msemo unasema, "Umasikini ni mbaya tena unatia haya." Nami nakubali kwamba umasikini ni mbaya sana, tena siupendi.

Kwa wale waliopitia maisha ya umasikini au wale wanaopitia sasa maisha ya umasikini wanaweza kunielewa vizuri bila shaka.

Lakini licha ya ukweli huu kuwa umasikini ni mbaya lakini tunaweza kuwa na mtazamo chanya juu ya umasikini katika jamii zetu.

Umasikini sio tu ukosefu wa pesa, bali tunaweza kuutazama kama ni shule ngumu inayofundisha mambo mengi sana.

Maisha ndani ya umasikini ni darasa linalotoa elimu ambayo hata shule ya msingi, sekondari au Chuo Kikuu haiwezi kukufundishwa.

Hata vitabu vinavyoelezea kuhusu maisha ya umasikini havijaeleza kwa undani na huwezi kupata darasa halisi sawa na yule aliyekulia au anayeishi maisha ya umasikini.

Maisha ndani ya umasikini ni elimu iliyoambatana na mteso makali. Huku hakuna viboko lakini maisha yenyewe ni kiboko tosha, tena kina makali zaidi ya kile kiboko cha mkoloni.

Ukiyatazama maisha katika mtazamo chanya kuna funzo kubwa utalipata katika maisha ndani ya umasikini. Mfano: unaweza kujifunza mambo kama haya yafuatayo;

1. Ustahimilivu na subira. - Umasikini unakufunza kuwa mvumilivu na mwenye subira ukiamini kesho mambo yatakuwa mazuri.
=Hapa utajua thamani ya kila senti au chakula kidogo unachopata.

2. Ubunifu na akili ya kuishi. - Maisha yanakufanya ubuni mbinu za kukupa chakula, mavazi na namna gani kesho utainua maisha yako.
=Hapa unajifunza jinsi ya kuishi kwa kipato kidogo, kutafuta suluhu za haraka, na kuishi bila misaada ya watu wengine.

3. Kutambua thamani ya vitu vidogo. - Maisha yanafanya ujue kufurahia vitu vidogo unavyopata vilivyo ndani ya uwezo wako kuliko vikubwa ambavyo bado huna uwezo navyo.
=Hapa hata ukipewa kidogo unashukuru sana kwani unajua kuwa hakipatikani kirahisi.

4. Kujitambua na kujiamini. - unapojua unaweza kuishi bila anasa nyingi, unapata nguvu ya ndani ambayo haitaweza kuondolewa kwa urahisi hata ukipata pesa baadaye.
=Hapa wengi waliopata pesa kwa kupambana kwa juhudi zao hawawi limbukeni wa pesa.

5. Kujifunza kutokana na makosa. - Mara nyingi umasikini unafanya uone makosa yako wazi, na hivyo kujirekebisha haraka.
=Hii ni kwa wenye kupata muda wa kujitafakari juu ya nini sababu umasikini wao na nini wafanye kujinasua hapo walipo.

NB: wengi waliopanda juu kutoka chini kabisa wanasema maisha ndani ya umasikini na kujitafuta ni shule iliyowapa misingi imara ya maisha yao hadi kujipata kwenye mafanikio.
=Maisha hayo yamewapa hekima ya kutumia vizuri kila senti wanayoipata.

UMASIKINI sio hatima bali ni darasa tu watu tunapitia.
Baada ya kufundishwa, ni wakati wa kutumia elimu hiyo kuondoka hapo, kuishi maisha ya utoshelevu na maendeleo ya kimaisha.


Je, umewahi kuuchukulia umasikini kama darasa?

Je, una mtazamo tofauti na mtazamo huu? Tuandikie hapa kwenye comments.

#No_learnig_No_earning
So We Have To Learn.

Content By George Francis

#mrgeorgefrancis #highlight #motivation #viral
 
Umaskini ni shule tena unatoa cheti na moyo na ubongo hupokea chet icho,umaskini ni fulsa asa apa afrika wanasia wengi hutumia umaskini wa wananchi kama fulsa,
 
Back
Top Bottom