Maisha magumu sana ila nina imani ipo siku nitafanikiwa

Maisha yanazidi kunichachia kila kukicha, nimetafuta sana kazi bila mafanikio yoyote mpaka ninahisi nimerogwa.

Mtaani thamani yangu imeshuka mno maaana nilipiga hatua kidogo ya kielimu ila nikakosa mtu wa kuniendeleza baada ya kufiwa na mama (baba yupo ila ni baba jina) hivyo nikakata tamaa ya kuandika barua ya ku-postpone maana nilishawahi ku-postpone lakini mambo hayakwenda vizuri hivyo nikaamua kuacha chuo.

Kwa sasa nahitaji angalau kupata kazi niingize japo elfu 7 kwa siku.

Mawazo ya kujiua yananiandama mara kwa mara ila ninapingana nayo kiume. Nina imani ipo siku nitafanikiwa.
Hakuna shida au tatizo lolote jipya duniani nasi tulipita huko miaka 16 iliyopita tukasimama.
Fungia vyeti kabatini,wema aibu pembeni,usipende kukaa ndani utakufa stress toka tembea tembea hata kwa mguu hata Kama huna nauli usikubali kukaa nyumbani,nenda kakae sehemu zenye watu wengi zenye pilikapilika jioni Rudi home hivyo hivyo baada ya wiki utagundua cha kufanya.Uza simu fanya mtaji fungua kijiwe uza chochote upate pa kuanzia.
 
Maisha yanazidi kunichachia kila kukicha, nimetafuta sana kazi bila mafanikio yoyote mpaka ninahisi nimerogwa.

Mtaani thamani yangu imeshuka mno maaana nilipiga hatua kidogo ya kielimu ila nikakosa mtu wa kuniendeleza baada ya kufiwa na mama (baba yupo ila ni baba jina) hivyo nikakata tamaa ya kuandika barua ya ku-postpone maana nilishawahi ku-postpone lakini mambo hayakwenda vizuri hivyo nikaamua kuacha chuo.

Kwa sasa nahitaji angalau kupata kazi niingize japo elfu 7 kwa siku.

Mawazo ya kujiua yananiandama mara kwa mara ila ninapingana nayo kiume. Nina imani ipo siku nitafanikiwa.
Vaa smart ,nenda kwa vinyozi kajifunze hiyo kazi
 
Pana tajiri mmoja Mkubwa sana Nigeria ni motivation pia kuhusu ujasiliamali na mafanikio.Baada ya kumaliza masters ya uchumi UK akarudi nigeria amesaka ajira kwa miaka 10 bila mafanikio na kupelekea kukata tamaa kabisa ikampelekea kwenye ulevi wa pombe chafu akiwa kapoteza kabisa matumaini.Pombe uunganisha urafiki hasa mkikutana vilabuni,akapata rafiki ambae ni mlevi mwenzake wakawa wanaishi wote maana hata uwezo wa kodi hakuwa nao.Yule mlevi aliishi kwa kutegemea kusukuma torori mjini lagosi kubebea watu mizigo uhakika wa kipato utegemea na wingi wa Kazi akipata utumia yote kesho atapata zingine,yule mlevi akawa akimshwishi mchumi waende wakasukume wote mkokotoni kuliko kukaa ndani bila Kazi,kwa shingo upande na hana jinsi mchumi ikabidi aweke masters pembeni akashika torori aibu pembeni asife njaa ajira zimegoma.Wakawa wanaenda wote aibu ikamtoka Kazi ikaingia damuni maana hel ya kula na kulewa sio shida tena uhakika upo, baada ya uzoefu na kuijua Kazi mchumi akaamua kusave akipata utumia robo zingine anasave bank alifanya Kazi ya torori na kusave ndani ya mwaka kwenda kuchungulia akaunti bank hakuamini pesa aliyoikuta ndo akafanya mtaji wa kuanzia kufungua biashara sababu uzoefu wa kuwabebea wafanyabiashara mizigo akafungua duka lake likafanya vizuri plus uchungu na nidhamu ya Kazi na hofu ya kurudi chini kwenye ulevi akafanya vizuri biashara ikakua akafungua maduka mengine na mengine mtaji ukakua akaanza biashara za kuchukua vitu nje ya nchi vinapotoka na kuuza kwenye maduka yake akajenga magodauni ya mizigo akawa ajenti Mkubwa na kuzidi kufungua biashara tele tele zikampa utajiri Mkubwa saana Nigeria.
Funzo hapa tunaona Masters holder amechanganya elimu mbili ya darasani kujua umuhimu wa saving na hofu ya kesho akiwa mgonjwa au mzee je ataendelea kusukuma torori?
Point kubwa hapa ni kwamba wengi waliokwenye hizi shughuli ndogo ndogo hawazioni Kama ni fursa wanazoweza zikuza Ili waje wawe wafanyabiashara wakubwa kupitia savings.
Hizi shughuli zenye kudharauliwa na wengi ukizifanya kwa malengo ni rahisi kufikia malengo yako.
Weka vyeti kabatini fungia aibu nyumbani ingia mtaani fanya chochote kiingizacho zingatia savings upate msingi baada ya mwaka au miaka.
 
Uzoefu wangu nilipiga Kazi za ulinzi usiku nikaongea na mpanga malindo nikapangwa night shift mchana napiga umachinga kwa mwaka mzima Hadi nilipokuja kutoboa.Usisubirie embe chini liive lifate juu
 
Maisha yanazidi kunichachia kila kukicha, nimetafuta sana kazi bila mafanikio yoyote mpaka ninahisi nimerogwa.

Mtaani thamani yangu imeshuka mno maaana nilipiga hatua kidogo ya kielimu ila nikakosa mtu wa kuniendeleza baada ya kufiwa na mama (baba yupo ila ni baba jina) hivyo nikakata tamaa ya kuandika barua ya ku-postpone maana nilishawahi ku-postpone lakini mambo hayakwenda vizuri hivyo nikaamua kuacha chuo.

Kwa sasa nahitaji angalau kupata kazi niingize japo elfu 7 kwa siku.

Mawazo ya kujiua yananiandama mara kwa mara ila ninapingana nayo kiume. Nina imani ipo siku nitafanikiwa.
Mkuu nilikuwa na shughuli yangu nilikuwa naifanya, nilikuwa natumia nguvu na akili mingi sana, mambo yakaingiliana nikapata kesi ambayo sijui mbele wala nyuma. Yaani jambo limefanywa na mtu mwingine ila mawasiliano yangu kukutwa kwenye simu ya mhusika nikadakwa na Mimi.

Nimekaa mahabusu siku 11 , usiku na mchana nipo polisi, dhamana hakuna aliyetegemea kama ningepata, kesi ni ya jamhuri ndiyo inayonishtaki.

Vifaa vyangu vyote vya kazi vipo polisi. Nina mtoto mmoja na mke, balance yangu iliyokuwepo nilikuwa pesa ya kulipa kodi tu maana nilitegemea kadiri ambavyo ningeendelea na kazi yangu pesa za kutumia zingeendelea kupatikana.

Sina balance yoyote, kodi mwisho ilikuwa December 2020, inatakiwa familia iudumiwe, nitafute pesa ya kodi maana imeisha iliyokuwepo mzee wangu mwenye nyumba hodi na vikao haviishi, mpaka sina kazi yoyote, sijui hatima ya kesi maana naambiwa upelelezi bado unaendelea na kila siku inatakiwa nitoe nauli kwenda kuripoti.

Kuna mengi sana ambayo yanaendelea kwasasa katika maisha ILA mpak sasa mkuu sijakata tamaa bado na nina hustle kutafuta kazi yoyote ili kujikwamua.

December na hii January imekuwa nyakati ngumu sana kwangu.

Ila bado sijakata tamaa.

Mkuu nikuweke wazi tu, wewe huna MATATIZO ila una CHANGAMOTO.

Changamoto zipo kukujenga

Changamoto zipo kukufundisha.

Changamoto zipo kukuonyesha watu wako.

Changamoto zipo kukufunulia yale yaliyojificha.

Changamoto zipo kukuandaa kwaajili ya fursa kubwa zaidi.

Changamoto zipo kukufungua kichwa.

Nyakati ngumu zisikufanye ukate tamaa na kuona ndiyo mwisho wa maisha, hapana. Nyakati ngumu zinakuja pale ambapo unahitajika kuingia hatua nyingine katika maisha hivyo lazima uandaliwe mkuu.

Huu ni wakati wa maandalizi. We ni mwanaume, kaa, tafakari, tafuta njia za kutatua na pia fanya juu chini kutekeleza njia hizo ili kufikia lengo.

Huna matatizo mkuu, kuna watu humu wana shida kiasi kwamba wakiona unapata mawazo ya kujikatisha uhai kisa hayo, watakushangaa sana.

Simama mkuu, nyakati ngumu hazidumu milele.
 
Mimi nina NDOTO ya kua Bilionea kama Babu yangu,

Nae alikufa na NDOTO hii hii..
 
Hapo kwenye baba jina umeharibu humu kuna watu wanajiheshim kwakauli hii unaweza kuwakatisha tamaa .futa au toa ufafanuzi kwann baba jina
 
Back
Top Bottom