Maisha jamani!

Raymanu KE

JF-Expert Member
Jan 20, 2022
6,843
12,612
Mama mjane aliyeachiwa wanawe wakiwa wadogo amepambana Sana katika kuwalea.Hana shughuli inayomuingizia kipato Cha kueleweka anaishi kwa kuunga unga ilmradi maisha yasonge.

Amekuwa akifanya vibarua mbali mbali Kwenye mashamba ya watu ili aweze kukidhi mahitaji ya wanawe ikiwemo chakula,mavazi na Karo ya shule.Hana ndugu wa kumsaidia Wala msamaria mwema Bali amekuwa akimtegemea Mungu kwa kila Jambo afanyalo.

Amejichanga changa mpaka watoto wamehitimu shule ya msingi wameingia shule ya upili.
Kula yao imekuwa Ni chai ya rangi bila vitafunwa,mchana mihogo mikavu wanashusha kwa maji na jioni ugali kwa mlenda.Hii Ndio imekuwa menyu yao siku nenda siku Rudi.

Kwa jasho na bidii za mama yao hatimaye watoto wamehitimu elimu ya chuo na Mungu amewaneesha wamepata kazi nzuri.Sasa watoto wapo Kwenye nafasi ya kubadilishana mfumo was maisha ya nyumbani kwao kuanzi chakula, mavazi na makazi.Yaani umaskini Ndio Basi Tena.
Kwa hiyo Sasa Ni muda muafaka kwa mama kupokea chochote kutoka kwa wanawe aliowapambania mpaka wakafanikiwa.

Mama naye umri umemtupa amechoka Sana yupo Kwenye 85+ na anatembea kwa mkongojo.She has now become vulnerable and prone to diseases.Amekuwa Ni mtu was kuumwa umwa kila Mara na kuwahishwa hospitilini kutibiwa magonjwa mbali mbali Kama pressure, kisukari, kiharusi na mengineyo.

Madaktari wamempa tahadhari juu ya vyakula mbali mbali ambavyo Ni hatari kwa afya Yake.
Wamemuonya dhidi ya matumizi ya sukari,chumvi,mafuta na vyakula vingine ambavyo vinaweza kuwa na athari Kwenye afya Yake.

Imagine watoto Ndio wamefika Kwenye nafasi nzuri ya kumpa mama yao chochote ambacho alikuwa hawezi kukimudu kipindi anawalea wanawe kutokana na Hali mbaya ya kiuchumi.

Watoto wapo Kwenye nafasi ya kumnunulia sukari ili naye anywe chai nzuri tofauti na awali ambapo walikuwa wanakunywa chai ya rangi isiyo na sukari, Leo hii madaktari wamemuonya dhidi ya matumizi ya sukari.

Wanawe wapo katika nafasi nzuri ya kumnunulia mafuta ya kupikia ili na yeye aweze kula chakula kitamu kilichopikwa kwa mafuta tofauti na siku za awali ila Ndio hivyo Tena madaktari wamemuonya dhidi ya matumizi ya mafuta.

Watoto wapo Kwenye nafasi nzuri ya kumnunulia gari ili naye awe anasafiri akiwa amekaa ila ndo ivo Tena umri umeshamtupa macho hayaoni vizuri kwa hiyo hawezi kuendesha gari.

Kwa hiyo Ina maana mama ataendelea kuyaishi maisha Yake ya awali ya kunywa chai isiyo na sukari, kula vyakula visivyo na mafuta na mengineyo licha ya wanawe kuwa katika nafasi nzuri ya kumpa chochote kwa wakati wowote.Inasikitisha Sana kwa kweli.

This life no balance.
 
Mama ana watoto wa ngapi kwanza? Tuanzie hapo.
 
Mama atakua na furaha tu coz ametimiza majukumu yake na kuona wanae sasa wamekua na wanaishi maisha yao kwa kujitegemea wao,hilo ni jambo kubwa sana kwa huyo Mama,

Kama ulivyosema alikua akimtegemea Mungu kwa kila afanyalo,basi bila shaka bado ana imani kwa Mungu kua maradhi aliyonayo ni mipango ya Mungu na kila jambo huja kwa sababu maalum japo kuna mengine sisi kama Binadamu hua tunashindwa kuyaona au kuyatafsiri,

Huyo Mama ataishi vizuri tu coz mzigo aliokua nao wa kuhangaika na watoto wake, sasa ameutua,

Hao watoto nawashauri wawe na moyo wakusaidia watu wenye shida,hiyo ni zawadi tosha kabisa kwa Mungu na waendelee kumlea Mama yao kwani huo ni mtihani kwao toka kwa muumba.
 
Umenena point nzuri Sana mkuu hongera
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom