Maisha Bongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha Bongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lily Flower, Mar 15, 2012.

 1. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hivi tunawezaje kuishi kwa matumizi yafuatayo kila mwezi?

  Fikiri matumizi nyumbani: chakula, umeme, gesi, maji, soda/juisi za wageni. Ada za watoto zinazolingana na za chuo kikuu.

  Matibabu hospitalini, pesa ya walinzi kwa mwezi, sherehe za kuaga na kukaribisha mwaka mpya; Zaka ya kanisani na misikitini, Kupanda Mbegu/ Sadaka, Shukurani ya Neno, Tozo za Flying (wazoa taka wa mikokoteni ambao huzit
  upa hapo hapo), Madalali wa nyumba/viwanja, Pango la nyumba, Fremu ya biashara/ofisi, Mazakayo wa mitandao ya simu [airtime vouchers] Mafuta ya gari Walinda/waosha magari (oya sista/blaza, mdogo wako nipo apaaa); Tozo za kuegesha magari, Makato ya Mikopo, Tozo za internet cafe ili uweze ku-surf.

  Rambirambi ya mfiwa mtaani kwetu, Harusi ya ndugu yako wa ukoo na zawadi, Sendoff ya mtoto wa mdogo wake rafiki yako na zawadi, Kumuaga mfanyakazi mwenzetu na zawadi, Michango ya komunio ya 1 & 2 na kipaimara; Michango ya besdei party na zawadi; Ndugu wa kule kijijini, Mshahara wa Hausigeli na hausiboi; Bodaboda, teksi na bajaj; Duka la dawa

  Tuisheni ya mtoto, Kuchangia wahanga wa mabomu na mafuriko. Kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa, Kununua CD/DVD ya Uzinduzi wa Kwaya yetu. Chakula cha mbwa, Machango wa Ujenzi wa Kupanua Kanisa, Kuchangia Uinjilisti Masasi, outing ya kitimoto, Ujenzi wa Nyumba Mabwepande, Kuendeleza shamba mkuranga (linalotaka kutaifishwa kwa kutoendelezwa).

  Na kwa wale wenzetu wanaokwenda umbali wa Viti Virefu, moja moto moja baridi. Maji ya Traffik, Chai ya Nesi na Daktari, Kahawa ya Hakimu, Karani na PP.

  Vishoka waunganisha maji na umeme; Kidogodogo cha mjumbe na mtendaji wa mtaa. Hivi hali inakuwaje? Mia mbili ya watoto wa mtaani/ombaomba, kitu kidogo cha wale wanaolazimisha kuosha kioo cha gari kwenye foleni.

  Umeme uliopanda bei, gesi iliyopanda bei, maji yaliyoadimika, bado contingency mana huu usafiri unaotembelea ball joint, bush, feni belt havijafa - hapo bado service. Bado msosi wa mchana kazini esp kama maofisi yetu mama ntilie wanakaribiana bei za restaurants, bado mchango wa kitchen pati na sare, baby shower. Na hapo bado hujatoa watoto outing jumapili n.k


  Hapo mwajiri amekuongezea mshahara kwa 7% tu wakati inflation ni above 19%. Ndipo unapoimba "Mwokozi nitoe roho niepuke na hili balaaa"

  Ukifikiria kwa makini unajiuliza watanzania wana-survive vipi kwa style hii???

   
 2. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Maisha bongo msoto kila siku, hawataki kucheza kiwasense wanapenda Ndomolo. Darisalama jua nachoma kama pasi.Nataka kwenda Zanziba lakini nogopa ngari ya kwenye maji. Kama ngari napinduka samaki takula mimi. Nahii ni aibu kwa morani, madumoki.
   
 3. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu, lakini tunayaweza vipi maisha ya kila siku spending without proper income?

   
 4. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,171
  Likes Received: 8,194
  Trophy Points: 280
  ndio mana huwa spendi kupoteza wakati kufanya ka-calculations.najua nitaumiza kichwa bure na bado hesabu haitatimia.naacha mambo yaende kama vile yatakavyo kuwa.hii ndio bongo-daslama
   
 5. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii ni hatari unaweza ukajiweka kwenye mstari wa stress, pressure nk.

   
 6. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa namna hiyo tunaishi kwa kubahatisha,ndugu yangu!
   
 7. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ukipiga mahesabu hapo unaweza ukaconclude unaishi kifisadi.

   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,177
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Lily Flower kwa halisi wabgongo wanaisghi kwa kubangaiza
  Kwa hali halisi mishahara yao haiendani na real life wanayoishi
  Nishahara ni midogo sana ila jwa mtu ana amatumizi ambayo hata ukiuliza huwezi amini na unakuta mpaka watoto wake wako shule za maana ila mishahara hiyo sasa ni balaa
  Kwa hali halisi ya ulichoeleza tunaishi kimjini mjini kabbisa na wala sio siri hatuendani na uhalisia
  Hata ukijiuliza haka kamshahara ya laki tatu ila mtoto wake anasoma shule ya bei mbaya huyo mtu anajenga, anapatikana kwenye viti virefu, anatibiwa private hospital, ana usafiri na huo usafiri haujulikani aliupataje
  Yaani full mauza uza
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Mbona ''raundi'' hukuitaja? ...... mwanaume mzani bana....unahitaji kama 200,000 kwa wiki
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,151
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Acha tu mkuu,bora nirudi zangu kijijini nikaendelee kuuza mkaa!!
   
 11. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Hapa ndio mara unajikuta umejikita kwenye uganga wa kienyeji ili kuongeza kipato.
   
 12. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,850
  Likes Received: 23,464
  Trophy Points: 280
  Kifupi ni kuwa sisi wote ni mijizi tu.....

  Wanaotuzidi kwenye kukwiba ndio tunawaita mafisadi.

  Mapadre wezi, wachungaji majizi, mashehe majizi, maaskofu wezi, masista majizi.......... Yaani wizi mtupu!

  Kitu pekee ambacho hakiibi ni BIA.....!
   
 13. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mwana FA aliimba USIJE MJINI; ndo hiyo sasa
   
 14. D

  DURACEF JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 244
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  gudaftrenoon umetisha.
   
 15. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  In green: I will do that, no matter what. So I just balance quality vs quantity na napambana nayo hivo hivo
  In orange: It is important but not crucial, I will spend on those only if I am through spending on the greens
  In red: I don't need it. I just don't! I will use this money to add on my savings and move forward. Labda niwe na account inayo leta interests nzuri, then I will buy that on those interests.
   
 16. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Me like this post!
  Chama cha wanywa beer Tanzania kinawaalika wanywaji wote wa beer kuja kupima afya zao!

  Ukipima presure unapt bia moja, ukipima ngoma unapata bia tatu!!

  Karibuni Sana weekend hii pale mnazi mmoja
   
 17. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Hii nayo ni nyongeza mkuu dah! ni kizungu zungu.
   
 18. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu haya ndio maisha ya kila siku ya mbongo.

  Habari yako binafsi bana

   
 19. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sasa Mkuu huko kijijini kunakalika? inabidi uvae bomu tu.

   
 20. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ya kweli mkuu mwisho wa mwaka mahesabu yanakuwa overspent lakini unaona sawa tu, kimjini mjini.

   
Loading...