Kwa hili tuipongeze serikali kwa juhudi zilizofanyika kuweka shule angalau ya msingi na sekondari kila kata. Na ikiwezekana zijengwe na Veta karibia kila kata.
Kwa hali ya kawaida kuna watu kwa kipato chao tu hawatakiwi kuitwa waajiri ila unakuta ana mtoto wa mtu anamfanyisha kazi anamwita mdada wangu wa kazi, anachomlipa cha maana hamna huu ni utumwa kama aina nyingine za biashara za utumwa zilizokomeshwa.
Na hali hii ya wasichana wa ndani kupotea/ kupatikana kwa shida iendelee na kuzidi, ili hili jina la wadada wandani lifutike kabisa ili kila atakaye zaa mtoto ajue kuna vituo vinaitwa day care kwaajili ya kutunza watoto na ikishindikana aajiriwe mtumishi wa nyumbani ambaye atakuwa na haki zote za kiutumishi.
Utumwa wa kuwatumikisha watoto wa watu waliotoka familia duni ufe.