Maimamu watoa neno kwa JPM kuhusu Masheikh wa Uamsho

wilcoxon

JF-Expert Member
Jun 25, 2017
1,094
2,831
Taasisi ya Imamu Bukhari imelalamikia utaratibu uliowekwa na Askari Magereza wa kuwahudumia Masheikh wa uamsho wanaoshikiliwa kwa kosa la kujihusisha na ugaidi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sheikh Khalifa Khamis alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,amesema kuwa utaratibu wa kutoa huduma kwa masheikh hao.

“Tunasikitishwa sana na jinsi watu hawa wanavyotendewa utadhani kama sio Watanzania, sasa tunajua hata rais Dkt. Magufuli hajui kinachoendelea, inasikitisha sana ndio maana tumeamua kuliweka hadharani ili kila mtu aelewe kinachoendelea,”amesema Sheikh Khamis.

Hata hivyo, ametaja orodha ya watuhumiwa wa ugaidi katika mikoa yote hapa nchini na kuiomba Serikali kutolea maamuzi kesi hizo kwani watuhumiwa hao wamekaa kwa muda mrefu Magerezani.

Chanzo: Dar24
 
Kweli waislamu wa awamu ya 5 sio wale wa awamu ya 2 na ya 3.....wamekuwaje?? Wanashinda hata kuwapigia kelele ndugu zao haki itendeke? Kweli?? Wamedanganywa na gorofa la Bakwata la 5bil Toka kwa kafiri Wamekuwa kama wana ganzi??..... wasimame sasa awamu hii sio rafiki kW uislam.....tusimame haki!!
 
Lkn hawa watu walikuwa wakitamba na kumtukana Rais waziwazi na kumtishia waziwazi, walisababisha mauaji na kumwagiwa tindikali watu wasio na hatia mapadri hata watu waliojitolea kuja kusaidia watu wa znz.
Ni uislam gani una sapoti hayo? Nimemsikiliza Shehe ameeleza vizuri tu wewe ndiwe unaleta maelezo tofauti hajasema serikali hii ni adui wa uislam. Ugaidi ni uhaini dhidi ya binadamu afanyaye hivyo ni ajenti wa shetwan na hata apangaye au kusaidia hawastahili kuishi katka jamii ya watu

Sent from my ALE-UL00 using JamiiForums mobile app
 
Kweli waislamu wa awamu ya 5 sio wale wa awamu ya 2 na ya 3.....wamekuwaje?? Wanashinda hata kuwapigia kelele ndugu zao haki itendeke? Kweli?? Wamedanganywa na gorofa la Bakwata la 5bil Toka kwa kafiri Wamekuwa kama wana ganzi??..... wasimame sasa awamu hii sio rafiki kW uislam.....tusimame haki!!
Shehe hajaongea hayo....tusiongeze chumvi.
 
Back
Top Bottom