Mahusiano yako na watu wengine. . . . YANARIDHISHA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahusiano yako na watu wengine. . . . YANARIDHISHA?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Jan 7, 2012.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kuna kipindi nilikua naangalia mdada kamkuta mtu aliyebeba vitu kwa mikono yote miwili anasumbuka kufungua mlango, akafungua alafu akaufunga nyuma yake kana kwamba hakukua na mtu mwingine pale japo alimwona, anapenda kuchungulia chungulia (snooping around) vitu vya watu wengine akijua haonekani. Alipoulizwa ye ni mtu wa aina gani (kabla hajajua alikua anaangaliwa) akajibu mzuri na mstaarabu, baada ya kuonyeshwa video akaishia kulia huku akilalamika kwamba anajijua mwenyewe ni mtu mzuri na blah blah nyingine.

  Wewe kama wewe unajichukualia ni mtu mzuri na mstaarabu kwa ndugu, jamaa,marafiki na hata watu wengine unaokutana nao?Unajitahidi kua mstaarabu hata kidogo au hujali?

  Unadhani hao watu wakiulizwa kuhusu wewe wengi wao watajibu kwamba wewe ni mtu mzuri/mstaarabu au kinyume cha hapo?

  Kama leo hii mtu angekurecord kwa siri wakaonyeshwa watu wasiokufahamu, unadhani wangesema nini kuhusu wewe?

  Binafsi hua najitahidi kwa kiasi changu, hata kumshikia mtu aliyepo nyuma yangu mlango, kumuokotea kitu au kumwambia samahani nikimgonga. Na bahati nzuri na mie hua nafanyiwa, wiki hii tu nimedondosha vitu mara mbili nikaokotewa, kuna siku nilisahau kadi yangu ya benki dukani mtu akanikimbizia. . . vitu kama hivi hua vinanifanya nitabasamu hata kama sikua kwenye mood nzuri. Au rafiki anaekumbuka kukujulia hali siku ya pili baada ya kumwambia unaumwa, mtu anaekumbuka na kukumbusha mambo yako ya maana na vitu kama hivyo. It just makes me happy to know there are really nice, caring and decent people out there. I hope YOU are one of them.

  Week end njema.
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Mi mzuri na mstaarabu sana hadi kuna watu wananiambia wanatamani wangekuwa kama mimi. Lol.
   
 3. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  ..Naamini watu wengi wanaonizunguka wakiulizwa kuhusu mimi watasema ni mstaarabu..kwa mfano,naweza nikagombania basi then napata seat then kituo kinachofuata anapanda mama mjamzito au mama mwenye mtoto chini ya miaka minne,nasimama nakumpisha akae yeye...and her appreciating face makes mi feel good kwakweli...
   
 4. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,282
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Sijali watu wengine wanavyofikiria juu yangu; and I dont know if I am 'really nice, caring and decent'. Najali nawaza na na najitahidi kufanya yale yasiyowakwaza na yanayowasaidia wanapohitaji msaada, watu wote wanaonizunguka na wa mbali ninaoweza kuwafikia.
   
 5. bht

  bht JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  you are who you are what people think of you is non of your business... Au sio FA?
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  yaani mimi ni mkorofi sana, najali mambo yangu tu.
  Lakini nikiishi na watu siku sipo kila mtu ananitafuta, eti njoo bwana tumekumiss.
  Huwa nashangaa sana.
  Kumbe watu bwana wanakukubali kama ulivyo, usijaribu sana kuwa-impress.
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Ni kweli watu wanakupokea kama ulivyo.
  Mie mkorofi mno, siku za mwanzo lazima uje na panado kama tuko sehemu ya kazi moja.

  Lakini, nikiondoka kazini wiki moja siku narudi kama Victoria Bekham, ni mwendo wa kuwasainia auto zao tu.

   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  ila ukitaka kujua mahusiano yako na wengine, pata shida\tatizo
   
 9. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nice thread.

  Mara nyingi sana mimi niko simple, na marafiki zangu wengi wanaipenda tabia yangu...Kuhusu family hao nadhani wananijua vizuri kuliko wengine na mpaa mda huu sijasikia katika family members hawajapendezewa na tabia yangu.

  Upande wa watu kulizwa tabia yangu kama nzuri, na shaka wengi walisha ulizwa na hakuna aliye niponda, zaidi ya Boss wangu mmoja alisema sitoki kwenye face book na forum flani hivi hahaha...Lakini najua lazima kuna wako wako wanaponda tu, unajua binadamu huwezi kuwaradhisha wote...Lakini najitahidi sana kukosa ma-adui hasa siku hizi.

  @Point ya kurecordiwa sidhani kama watakuwa na record kama ya mungu au malaika wa mungu....Yani sidhani kama wataninasa kwa baya, mana mara nyingi sana niko very careful kufanya mabaya...Afu mambo ya kuwa na gf sidhani kama ni baya au uwongo.

  Ikitokea bahati mbaya wakaninasa kwenye video nafanya mabaya, sidhani kama yatakuwa ya aibu sana mana niko na gf wangu:biggrin:
   
 10. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Very tru...Pale ndio kipimo cha socialization ya mtu kinapoonekana..!!! Wale wenye tabia ya kuacha michango kwenye misiba ya wenzao kisha haao wanaishia...wanajuta sana kipindi hiki kikiwafika.
   
 11. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  huwezi jua jamii inayo kuzunguka inakuchukuliaje kama una hela. ukiwa na hela utaona unaishi na watu vizuri na watu wote wanakupenda hata ukipita kwa mbali unasimamishwa ili usalimiwe tu. lakini amini nakuambia hali utaiona ya tofauti pindi utakapo ishiwa hela. binadamu hawatabiliki wala hawafadhiliki. ishi utakavyo na fanya uwezacho. Mia
   
 12. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Namshukuru the way alivyonifanya niwe na kwa malezi ya wazazi wangu niko km nilivyo,
  Kipimo cha kujijua ww ni mtu wa aina gani hasa kwa jamii ni km alivyosema bht hapo juu,
  Ukiwa na shida au tatizo ule muitikio wa jamii au watu wanaokuzunguka utakupa majibu sahihi ya kuwa ww ni mtu wa aina gani,
  Kuna haya mambo mengine yanayotokea kwa watu tusiowajua kumpisha mzee au mama mwenye mtoto au mjamzito akae kwenye daladala ni ya kawaida kufanyiana km binadam,kushukuru,kuomba samahan,kusalimia,kumsaidia mtu km jambo liko ndani ya uwezo wangu na mengine ya kibinadam.
   
 13. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Mi hata sijui wananichukuliaje!!
   
 14. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  sio kweli huwa ninasaidia sana watu walikini siku nina shida nikiingia kwenye pnone book yangu sioni mtu wa kunisaidia. na kuna mama mmoja aliwahi kuniambia kuwa dunia haikulipi kile unachowekeza
   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  afu wewe wanakuogopa sana
  si ni nanii wewe

   
 16. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Wanadata na mimi yooooooooo
   
 17. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  mkuu mimi nakuchukulia poa. vipi, wewe unanchukuliaje? Mia
   
 18. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Siku ukipata shida,ndio utajua wanakuchukuliaje?
  Mzima ww?
   
 19. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #19
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  mi ni nani? Hahahah Kongosho bana, wanaoniogopa ujue walishawahi kunichokoza hao!!
   
 20. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #20
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Kama ndo hivo basi naweza sema wengi wananidharau na kunichukulia kama kituo cha misaada na kutatulia shida zao. Wakiwa na shida esp mkwanja au mahali pa kuishi, nitapokea simu hata za waliokata mawasiliano tangu mwaka 47 ila wanakukumbuka kwa vile wana shida, mambo yakiwanyokea haoo wanapotea!! My dady mwenyewe alikuwa na mahusiano mazuri sana na watu ila alipougua kwani kuna watu walionekana?? My dear, tuseme tu kwamba tujitahidi kuwafanyia mazuri wenzetu, wakituchukulia vema na kuonesha ushirikiano basi itapendeza zaidi!! Btw, mi mzima kabisa, sijui wewe?
   
Loading...