Poleni kwa ujenzi wa viwanda ndugu zangu..
Kuna ndugu yangu yupo kwenye ndoa miaka nane ila kwa sasa maisha wanayoishi ni ya ajabu sana,
Washagawana vyumba mwaka wa pili sasa,jamaa hata arudi saa nne usiku lazima awaamshe watoto ale nao pamoja hata kama wameshiba ni wazi anahofia kulishwa sumu na mkewe.
Ni familia bora sana kiuchumi mwanamke ana pesa mwanaume ana pesa lakini wamechagua kuishi kwa kuviziana, Kwao ni jambo la kawaida mtu kutoka saa nne usiku kurudi asubuhi
Vipi wakuu kuna uwezekano wowote wakuinusuru ndoa hii???