MAHUSIANO YA NDOA NA UCHUMI - Usije ruhusu mwanamke akutawale kiuchumi labda akushirikishe kiyakinifu

matemabi

Senior Member
May 2, 2017
103
125
Nakumbuka mama alishawahi niambia kwamba nikihitaji heshima ndani ya nyumba ni kuwa bora kiuchumi kumzidi mwanamke wangu.

Lakini mpaka sasa mapambano yanaendelea naona kabisa naelekea kubaya zaidi.

Mke wangu ni mwajiliwa kwenye mashirika makubwa hapa nchini, analipwa pesa ya kawaida lakini posho zinampatia hrla nyingi sana kiasi kwamba anatoa mchango mkubwa sana kwenye swala la ujenzi hapa nyumbani.

Kutokana na hali hii, amekuwa na maamuzi zaidi ya kiuchumi haswa kayika matumizi ya pesa inayopatikana. Ninaweza kusema mawazo yangu kama hayajayaelewa basi yake hatengenezi muda kunishawishi labda naongea point au lah.

Wakati mimi nawaza tuwekeze hata cash point ya MPESA mwenzangu anawaza nyumba tuu. Leo turekebishe hiki kesho hiki, ingawa ananishirikisha ila kiuana ume nahisi ni utumwa sasa.

Hii inanikumbusha ile kauli ya mama kuwa nitafute hela, na ninafikiri kuwa hakuna namna yoyote ile zaidi ya kupambana kivyangu kujua uanaume wangu utajistili kivipi maana sasa nina miaka 30 na mtoto mmoja kesho mtoto akiongezeka na majukumu yakiongezeka hali inaweza kuwa tete zaidi.

Japokuwa naheshimu mawazo ya mwenzangu ila naona ushirikishwaji ama kuaminiana kwenye mashauri bado ni tatizo na suruisho lake ni mimi kuwa na pesa zaidi. Asikudanganye mtu mwanamke atakaye kaa chini kukusikiliza na kuzingatia angalau machache unayo shauri huyo ni bonge la mtu.

Mniombee naenda kutafuta hela, ipo siku nitarudi kuwashuhudia mafanikio.

Sent from my SM-N976N using JamiiForums mobile app
 
Nakumbuka mama alishawahi niambia kwamba nikihitaji heshima ndani ya nyumba ni kuwa bora kiuchumi kumzidi mwanamke wangu.
Sent from my SM-N976N using JamiiForums mobile app
Shida ya kuzaliwa maskini Ndiyo hiyo vi principle vingi vya ajabu ajabu

Waliozaliwa familia zenye uwezo na kuoana wote Wana uwezo huo ujinga haupo .

Oaneni Kwa saizi yenu ndicho alichotakiwa kukuambia kama wewe kidume lofa kaoe lofa mwenzio kijijini huko
 
Hata huyo mama yako usipokuwa na hela atakuona takataka ingawaje atakusitiri na ikizidi atakuchana tu! Itakuwa mkeo?
Sahihi Tena kama akina mama wa kizaramo uvumilivu hawana kabisa anakwambia wazi hicho chumba unacholala mawili ukatafute kwako ukapange mimi nimeshatafuta mpangaji wa kukaa awe ananilipa Kodi nipate Hela ya kuwalisha au wewe upange uwe unanilipa Kodi niwalishe .Ni mawili tu hakuna kukaa Bure Tena humo ndani ni amri sio ombi.Na wako kibao wanalipa Kodi kwenye nyumba za wazazi wao akijisikia kuchoka ruksa kuondoka
 
Back
Top Bottom