Mahusiano ya ndoa na mikopo

Mahusiano ya ndoa na mikopo

Nimejaribu tu kupiga hesabu ya marejesho, nikaona sio rafiki; wengi nyumba zao zimeuzwa kwa sababu ya mikopo, na hatimaye familia ikawa kwenye matatizo.
Yah nakubaliana na wew kwa asilimia 100 tatz ni suala la kukosekana na maamuzi sahihi na ushauri wa WATAALAMU Kama sisi wakati wa ukopaji na kiwango Cha mkopo husika
 
Kuna mwanamke mmoja kakopa shilingi milioni 4 kikoba, na kuweka rehani nyumba yake ya vyumba viwili, kwa marejesho ya muda wa miezi 5.

Kabla ya kupewa fedha hizo, mkopaji aliulizwa mara tatu tatu kama yuko siriazi na anachotaka kufanya; mbaya zaidi mkopaji ni mama wa nyumbani, na mumewe ni dereva wa kampuni moja ya wahindi huko mkoani.

Alipopata fedha hizo, alimtumia zote mumewe huyo aliyeko mkoani, ili kutimiza yale waliyokubaliana.

Mjadala: Je ataweza kurejesha zaidi ya laki 8 kila mwezi ili kunusuru nyumba yake isiuzwe?
Consent ya mume ipo kuruhusu mke kukopa kwa kuweka nyumba ya familia rehani?

Kama wamefunga ndoa na hilo hapo juu haikufanyika.
Huo Sio mkopo mliompatia Bali mlimpa sadaka na sadaka hairudishwi au grant,mungu awabariki.
 
Consent ya mume ipo kuhusu mke kukopa kwa kuweka nyumba ya familia rehani?

Kama wamefunga ndoa na hilo hapo juu haikufanyika.
Huo Sio mkopo mliompatia ni Bali mlimpa sadaka mungu awabariki.
Ni mtihani mkuu, tunatakiwa tuweze kuzuia tamaa zetu ili zisije kuathiri maisha ya familia.
 
Dah laki 8 ni nyingi sana, tusichukue mikopo hovyo hovyo, lazima kuwe na mkakati jinsi ya kuzitumia/ kuzizalisha
 
Back
Top Bottom