Mahusiano ya ndoa na mikopo

Mahusiano ya ndoa na mikopo

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,612
Reaction score
65,066
Kuna mwanamke mmoja kakopa shilingi milioni 4 kikoba, na kuweka rehani nyumba yake ya vyumba viwili, kwa marejesho ya muda wa miezi 5.

Kabla ya kupewa fedha hizo, mkopaji aliulizwa mara tatu tatu kama yuko siriazi na anachotaka kufanya; mbaya zaidi mkopaji ni mama wa nyumbani, na mumewe ni dereva wa kampuni moja ya wahindi huko mkoani.

Alipopata fedha hizo, alimtumia zote mumewe huyo aliyeko mkoani, ili kutimiza yale waliyokubaliana.

Mjadala: Je ataweza kurejesha zaidi ya laki 8 kila mwezi ili kunusuru nyumba yake isiuzwe?
 
we kwako inaweza kuwa ni kitu kidogo ila wao ndio wanajua ukubwa wa wanachotaka ufanya na matokeo yake.. kuna jamaa mmoja alishawa uza nyumba ili kununua canter ya kubeba mizigo na alikuwa na nyumba moja tu.. na leo ana nyumba tatu .. maisha ni kursk tu rafiki zaidi mkono wa Mngu uwe pamoja na wewe nje ya hapo hakuna mafanikio Nakubaliana na wewe; kwa makato hayo kwa mwezi yanaumiza, na pia ni risk kuweka rehani nyumba kwa kitu kidogo
 
Sio Lazima!
Mfano unataka kuogelea kwenye bwawa na mko watatu; wa kwanza kudumbukia akazama chini hakuonekana, wa pili naye akadumbukia na hakuonekana; je, wewe utaingia kwenye bwawa?
 
Kuna mwanamke mmoja kakopa shilingi milioni 4 kikoba, na kuweka rehani nyumba yake ya vyumba viwili, kwa marejesho ya muda wa miezi 5.

Kabla ya kupewa fedha hizo, mkopaji aliulizwa mara tatu tatu kama yuko siriazi na anachotaka kufanya; mbaya zaidi mkopaji ni mama wa nyumbani, na mumewe ni dereva wa kampuni moja ya wahindi huko mkoani.

Alipopata fedha hizo, alimtumia zote mumewe huyo aliyeko mkoani, ili kutimiza yale waliyokubaliana.

Mjadala: Je ataweza kurejesha zaidi ya laki 8 kila mwezi ili kunusuru nyumba yake isiuzwe?
Naona unataka ashindwe kurejesha utumie advantage hiyo kula kimasihara
 
Naona unataka ashindwe kurejesha utumie advantage hiyo kula kimasihara
Nimejaribu tu kupiga hesabu ya marejesho, nikaona sio rafiki; wengi nyumba zao zimeuzwa kwa sababu ya mikopo, na hatimaye familia ikawa kwenye matatizo.
 
Back
Top Bottom