Renegade,
Gone are the days when we were shy about HIV/AIDS facts.... sasa hivi ni ulimwengu mwingine wa kujadiLI kwa ukweli NA UWAZI bila unafiki.
Ni UCHAGUZI NA UAMUZI wa mtu binafsi na wala siyo lazima.Fikiria yafuatayo:
1. Maambukizi mengi zaidi au kitakwimu wanandoa ndio wanaoongoza kwa maambukizi ya UKIMWI
2.Wanandoa hawako immune kuambukizwa ati kwa vile wana leseni ya kujamiiana!
3. Wanadoa wako vulnerable to infidelity maana kwa kuoana hawapotezi ubinadamu wao ( udhaifu n.k.)
4. Kama wanandoa hawako waaminifu chances are kosa la mmojawapo ni hatari kwa mwingine aliye innocent.
5. Kwamba wana ndoa wanahitaji kuzaa si hoja ya kuambukizana UKIMWI
6. Kufuatana na sheria ya HAPCAT 2008 ( HIV/AIDS -( Prevention and Control Act) Kumwambukiza mwingine kwa makusudi ni kosa la jinai! Pia sheria hii inatutaka kila mmoja awe responsible kujilinda dhidi ya maambukizi.
7. Kuzaa ni jambo jema.Je wewe mwenye ndoa unapima kabla ya kutafuta mtoto? Kama jibu ni hapana, ukizaa mtoto mwenye maambukizi huoni unamkosea sana huyo mwanao? Kama utazaa na kuhakikisha unafuata PMTCT ( kuzuia maambukizi kutoka mama kwenda kwa mtoto)- je huoni ni busara uendelee kujikinga ili uishi maisha marefu umtunze mwanao? Kumbuka ngono isiyo na kinga baina ya wanandoa pia ni hatari hata kama wote mmeambukizwa tayari!
HIVYO NDUGU ZANGU, BILA KUTAKA YA UNDANI ZAIDI - JIKINGENI!