Ni kweli De Novo wote tuko katika risk but tukisema mtu akiamua kuwa makini na maisha yake kwa hali halisi mtu single anaweza akasimama na kujilinda tofauti na married kwani inatengemea na partner wako!! Sasa mfano hao waume ambao wanachukua mashoga wakati wake zao wako masomoni au safarini au wake wanaotoka na watu wengine aka ving'asti, mabuzi (sijui kama bado hili jina latumika) wote hao partners zao wanajiamini kuwa wako salama.
SingeLE:
- - hao walio single watakuwa single mpaka lini?? Siku akisema anataka kuoa au kuolewa ndio siku ambayo "singleness" yake inaisha. Maamuzi ya kuingia kwenye tendo la zinaa au ndoa ndio "risks" ambayo inazungumziwa katika vita dhidi ya UKIMWI.
- - Mwenyewe unaweza kujikinga, lakini huwezi kujua nafsi ya mwenzio ipoje, na moyo wa binadamu siku zote umebeba siri kubwa.
- - Ukisema unampenda sanaaaa, huwezi pia kumwohofia na wengi huwa anaishia kuamini kwa kauli, kama ukitongozwa unakubali pengine hata kwa kusema "nakuonea huruma" iweje pale mtu anapokuambia "hunianmini" wakati mshakuwa pamoja kwa zaidi ya miaka miwili na haujawahi kumwona akiugua hata malaria au kikohozi?? (pagumu!!).
- Ukishaanza kujiingiza kwenye mambo ya "kudonoana", hatari ya kuambukizwa au kuambukiza ni kubwa zaidi kwani pengine hata mazingira ya kufanya hilo tendo yanachochea kwa sana kutotumia kinga kwa mfano mkiwa mmelewa, ukiwa mbali na eneo ambalo kinga zinapatikana na tayari hamu ya kuingiliana kimwili ipo juu, au hata kama huna fedha za kupata hiyo kinga na bado unasema mwenzio unampenda na unahitaji kumtimizia haja yake ambayo pia itauridhisha mtima wako!!.
- Pengine hata ukimtaka mwenzio kupima, na mkawa wote salama kwa muda, haimaanishi kuwa mtaendelea kuwa hivyo na kulindana, kwani kichoche kikubwa katika kutekeleza agano hilo la "kulindana" ni mapenzi ya dhati..wapo watu ambao katika kipindi cha mapenzi wakikwazana inachukua mwezi na zaidi kurejeana na hapo ndipo wakati hatari...
- Kuna hatari pia kwa wale ambao wapo "single" ambao hawajajitambua, wanapenda starehe na mambo makuu ambayo kwa uwezo wa hali na akili zao wanaweza kujikuta wameingia katika mahusiano na watu ambao hawawezi hata kuwaelezeza "tukapime" (kwa mfano hali ya sasa ambapo mijimama inataka vijana wadogo wenye miaka chini ya 18 (Serengeti Boyz) au Mibaba inataka "vikuku"(mabinti wadogo).Sidhani kama hawa vijana wetu wanaweza kuwa na kauli kwa wale wanaowahadaa kimapenzi katika mazingira haya.
- Wapo wale "single" kule vijijini ambapo maisha tunayoyaona na kuyasimulia mijini kwao ni kama ndoto ya kufika mbinguni, na kule ndo hizo "kondomu" au "kupima" sijui kama vipo kwenye misamiati yao..wengi wanakufa kwa kuhadaika na wale wanaotoka mjini pengine kwa kutaka kuolewa wakaishi mjini nk.
Wanandoa
- Wanandoa nao ni yale yale, kama huwezi kuiamini nafsi yako, je ya mwenzako utaiamini? na ukiamini hutachukua tahadhari..
Kwenye ndoa yeyote hakuna suala la kutoaminiana , na ukisikia wanandoa hawaaminiani ujue kuwa hiyo ndoa imefika mwisho. Kwenye hakuna "kondomu" au "Kinga dhidi ya maradhi" labda kama ni ya kuzuia "mimba tu".
Dini ya kweli hairuhusu mwanandoa kutoka nje ya ndoa yake, na kwa zile dini zinazoruhusu kwa mwanaume kuoa zaidi ya mke mmoja, ni sawa na kumwambia asiwe mwaminifu kwa mkewe katika muda fulani wa kumpata mke mpya.
Tabaka jingine:
Ukiacha matabaka hayo mawili: Pia wapo wale ambao wanapata kutkana na dhambi ya wengine (watoto, wauguzi, wale wanaohudumia waathirika hasa kule vijijini ambapo hali za maisha inakuwa ngumu kuzingatia kanuni za afya). Wapo pia wale wanaomabukizwa kutokana na matukio kama ajali na uokoaji, kubakwa nk.
Changamoto:
Kwa matedo ya zinaa, kama ambavyo sheria za dini zisivyoruhusu matumizi ya kondomu kwa maanda ya kuchochea zinaa na kupingana na amri ya 6 ya Mungu, ni vyema tukazidi kuomba Mungu ili tamaa zetu za mwili zinazotupa raha ya muda mfupi zisije kutuangusha katika mateso na majuto makuu katika maisha na kuwasababishia na wengine wasiohusika shida na maumivu hapa duniani.