Muuza simu used
JF-Expert Member
- Aug 23, 2017
- 4,393
- 7,101
Nitazungumzia kidogo kuhusu maisha ya mapenzi pindi mtu unapokuwa Ughaibuni, kwanza kitu cha kwanza unakumbana na upweke wa hali ya juu lakini unaendelea kujifariji kwa kuchati na kidemu fulani ambacho ulikiacha home lakini haya mawasiliano hayataenda umbali mrefu sana.
Sababu ya kwanza utaona huko ulipomwacha anakusaliti tu na yeye pia atahisi hivyo pia kutokana na mawasiliano yakusua sua hii Mara nyingine inatokana na kutofautiana majira sehemu uliyotoka na sehemu uliyopo.
Unaweza ukatuma ujumbe mfupi wakati yeye amelala na wewe pia unaweza kujibu SMS yake na yeye pia tayari akiwa ameshalala kwa hiyo utajikuta tu mapenzi yamefika kikomo, kwahiyo kinachokujia sasa ni kusonga mbele na wewe kutafuta mwanamke mwingine kwa kutumia ile kauli mbiu kuwa "kama unayempenda yupo mbali, mpende aliye karibu yako".
Utajikuta umempenda mwanamke mwingine na kuazisha uhusiano mwingine na uhusiano huo unaweza kuzaa ndoa au watoto pia, sasa kimbembe kinakuja pindi umezaa na mwanamke wa ughaibuni na mkagombana.
Hapo kupata watoto wako ni ngumu kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano zaidi ya hapo utakutana na kitu kinaitwa children saport na ukajikuta kimshahara cha kibarua unachokifanya nusu kinakatwa kwa lazima kinaenda kwa watoto na watoto ambao hauwezi kuwapata! Stress zinakuelemea unakumbuka hata ungeoa home wakati imeshakuwa too late! Yapo mengi kwa Leo naishia hapo