MAHUSIANO: kazi Kweli kweli......!!

Mi pia nina mshkaji mtoto wa mamkubwa hatoki. Alikuja akasema anakaa wiki sasa ana miezi mi 2. Sijaoa na wala sina mke na yy hana shughuli. Hasomi alf hata kazi hatafuti. Tena kwa mizinga huyo. Cjui mwisho wake itakuwaje.

Mlie Tyming!
 
watu wa musoma ndo zao,yaani nina dingi mdogo mke wake ni wa huko musoma..ukienda kwake ni full wageni wa upande wa mkewe,..mpe pole huyo mdada

duh!Inatisha Aisee!
 
Khaaaaaaaaaaaaa.....

Mumeo ndo pekee mwenye uwezo wa kuokoa ndoa yako.....

Akisimama kama mwanaume, hata mngekua mnaishi na kijiji hapo kwako wote wangefuata sheria zenu........ Lakini ukiwa na mume dhaifu matokeo yake ndo hayo.....

Bibie vumilia tu......
Hapo unatakiwa ujali mumeo na wanao tu...uweke hg specific kwa wanao na boss ni wewe tu sio mama mkwe...

Kuhusu maji mbonma simple?? Hakikisha una maji ya kukutosha wewe na mumeo,na wanao....

Formula ni asiyefanya kazi na asile...

Vitu vyako valuables vifungie au mpelekee mama yako avihifadhi....

Kama ulikuwa unachangia matumizi ya nyumba acha, hela yako dunduliza nunua kiwanja......

Kisha sali sana mumeo asifumbe macho, akivuta tu umeumia....
 
hlo Neno Zito Sana Bila Shaka Alifanyie Kazi!
 
Hapo pagumu mama
Hivi watu wengine huwa wanashindwaje kukaa kwao jamani?
napenda wageni ila hii too much
..Hivi kama mie nina kwetu kwanini nikajaze mzigo kwa watu ..
 
Boga?!Mh yani nilivyokasirika we dada una moyo sana me nikisema nachagua kabila watu ooh mambo ya kizamani .kuna makabila yanajulikana kabisa kurundikana kwa ndungu ni tabia zao nasema ukweli hasa hao uliowataja japo sijui we mwenzangu umetoka wapi.Asilimia kubwa ya makabila toka kanda ya ziwa iyo ni kawaida na ukikutana na yule asiye mnafiki atakueleza ukweli.Halafu na si tunapenda ndoa mno ulipoona watu wooote hao si ungeweka msimamo kabla ya kuolewa. ona sasa watoto wako wataishia kuharibika .haya me sina hata cha kukushauri nakusikitikia tu ila ingekuwa mimi wewe ningehakikisha namshawishi mume tumehamia kwingine tena nyumba ningetafuta mimi hao tuwaache hapo manake kwa ulvyoeleza kuwaondoa hatakwa winchi ni ngumu

mweee.....nimeudhika sana kwa kweli.....raha ya mume mkae ndani mwenu muanzishe familia yenu......ndugu wakija leo kesho waondoke......mama mkwe kuja kukaa kwangu hilo ni kosa la jinai.....coz hata mama yangu hawezi kukubali kukaa kwangu......
 
hata hao wakigoma kuna shemeji yangu kaacha nyumba kahama na mkewe kwenda kusoma nje na nyumba akapangisha maana alikuwa wageni wanafika mpaka 20 du sasa wakati wanawaambia kuwa wameamua kuhamia nje mmja wao analalamika oh nilijua maish ayangu yataishia njiani alikuw anakula na kulala anaambiwa apelekwe shule hataki du,yaani maisha hayo nimabaya sana ukichinja hata kakuku huwezi kafaidi ,kha inabodi kuwasaidia mimi binafsi ni mhanga wa hili jambo ila ikifika pomonni nawafukuza au naweka mkakati kuwa hapa ni kulala tu kula utajua mwenyewe!
 
Huwa Nawakumbusha Wadogo Zangu Na Kaka Zangu Kuwa MNAPOTAKA KUOA MSICHAGUE WA UCHANGANYIKENI VILLAGE
Ona Sasa Huyu Nae Kadata Mpaka Kaniomba Ushauri.
Nanunukuu....

Mie nimeolewa nina watoto 2 lkn sina amani na ndoa yangu ndugu wa mwanamme
amenishinda yaani amenikaba koho sina amani sina raha ya ndoa yani npo npo tu yaan hata hamu ya kuchuma tunda na mume wangu haipo tena Mimi ndoa yangu inamiaka 7 na tokea nimeingia kwenye ndoa sikuwahi kuishi mm na mume wangu tu,siku zote nyumba imefulika ndugu wa mume na sio kwamba siwapendi la hasha! mambo wanayonifanyia ndio yanayosabisha nikoseamani na ndoa yangu yaani
vijimanenomaneno vya kila siku visivyokuwa na kichwa wala miguu na ile kukaa na watu kula kulala yaani hawafanyi kazi zozote za nyumbani kwa mfano kuchota maji ni inshu,kufua ni inshu yaani watu wapo nyumbani kutwa lkn mm nitatoka kazini nikirudi kama nguo zangu chafu zpo nyingi inanibidi nifue,kunyoosha yaani hapo nimemtafuta mtu wakuwa anakuja kuninyooshea na namlipa hela na watu wapo hawana kazi yeyote.

Tulianza hivi... Wakati tunaanza urafiki wetu na siku nilipokwenda nyumbani kwa mume wangu kumtembelea nilikuta nyumba inawatu wengi sana na nilimuuliza hv ukija kunioa hawa wote nitaishi nao?yeye alinijibu hao wanapita tu hawatakaa hapa mm nikamwambia sawa lkn siku zilivyokuwa zinazidi kwenda sikuona dalili ya hao watu kuondoka hapo bado hatujafunga ndoa ikabidi nimueleze mama yangu mzazi mama akanieleza mimi niendelee na hayo mahusiano yangu alichosema yy ni kuwa watu wenye familia kubwa huwa wanajitahidi kutafuta sana.
Nikaendelea hvyo hvyo lkn moyoni mwangu sikuwa na furaha
wakati huo ninaishi na wadogo zake 5 wakike 3 na Wakiume 2 na wakati huo walikuwa wakisoma shule ya msingi hadi leo wengine wamemaliza form 6,mwingine alipata ujauzito akiwa likizo ya kumaliza std 7 na kaka yake akakasirika akamtimua nyumbani na kurudi musoma,mwingine ndo yupo form 4 sasahv lkn nae pasua kichwa alipata ujauzito na ndg zake wake wakamtoa ili angalau amalize form 4 mwingine huyu ndio balaa nafikiri kiakili hayupo sawa yupo form 2 sasahv lkn mambo anayoyafanya ni balaa kwanza ni mwizi ndani anaiba hela,chupa za soda
kunakipindi alishauza kreti 2 za soda na bia 1,anavuta bangi anajidunga sindano anabani cd za ngono anakuja nazo nyumbani na anaangalia na still bado ninaishi nae hadi leo hii hv huo ni UVUMILIVU WA AINA GANI NILIONAO?
Mimi ninawatoto wadogo na sijui uwanajifunza nn?

So siku zikaenda na tukaona na siku natoka hnymoon narudi hm nyumba ilikuwa imejaa mama wakwe 4 na hao 5 na ndg wengine na walikaa wengine ndani ya mwezi 1-2 wakwe 3 wakaondoka nikabaki na mama mkwe yaan mama wa mume wangu kwan yy alikuwa ndo ameshafika,sasa huyo mama ni full kualika watu nyumbani waje wamtembelee na wakija atawang'ang'aniza
wabaki yaani hana huruma hata kdg watoto wake wanatunzwa hapo,yy na still anaita ndg wengine niliyavumilia na nikawa naongea na mume wangu
kuhusu alivyoniahidi kuwa wataondoka lkn kwasasa majibu yalikuwa tofauti na yale alinijibu sasa wataenda wapi? wewe vumilia wamalize shule na mwisho wa siku kila mtu atajitegemea

from there furaha ya ndoa ilitoweka nikawa naishi kimazoea nimeshafunga ndoa tayr bac sina jinsi yaani vitu vinanitesa sana
na hadi ndoa yangu imekuwa chungu yaani unajua nime
choka!
Sana nishaurini tafadhali nifanyaje maana nahisi nimefikia mwisho.

¤¤¤-- Mama Wawili--¤¤¤

Pole sana kwa yaliyokukuta! Kuna mtu ninayemfahamu aliwahi kupitia tatizo Kama Lako isipokuwa yeye alikuwa ni mume mtu, mke wake alileta wazazi wake hapo nyumbani na wadogo zake. Isipokuwa hiyo familia ya mke walikuwa wastaarabu na waelewaji. Ila mume alikuwa uncomfortable, so akaamua na mke wake wawaache ndugu wa mke hapo na wao wakaenda kupanga kwingine, na ikumbukwe hata nyumba waliyowaachia ndugu wanalipia rent pia na matumizi wanapeleka. Ila for the sake of children waliamua kufanya hivyo and now they are happy and peaceful. So ukiweza mdada jaribu kufanya hivyo au wazo lingine, punguza hao wadogo kwa kuwapeleka boarding school. Funga na kuomba kwa ajili ya hili Mungu atakuonyesha njia, it is a very challenging situation lakini Ndoa lazima iokolewe, Mungu hapendi Watu waachane! Good luck.
 
Khaaaaaaaaaaaaa.....

Mumeo ndo pekee mwenye uwezo wa kuokoa ndoa yako.....

Akisimama kama mwanaume, hata mngekua mnaishi na kijiji hapo kwako wote wangefuata sheria zenu........ Lakini ukiwa na mume dhaifu matokeo yake ndo hayo.....

Bibie vumilia tu......
Hapo unatakiwa ujali mumeo na wanao tu...uweke hg specific kwa wanao na boss ni wewe tu sio mama mkwe...

Kuhusu maji mbonma simple?? Hakikisha una maji ya kukutosha wewe na mumeo,na wanao....

Formula ni asiyefanya kazi na asile...

Vitu vyako valuables vifungie au mpelekee mama yako avihifadhi....

Kama ulikuwa unachangia matumizi ya nyumba acha, hela yako dunduliza nunua kiwanja......

Kisha sali sana mumeo asifumbe macho, akivuta tu umeumia....

Hii Nayo ukiweza fanya..sometimes inabidi uwe aggressive..wapende yes, ila na wao lazma wawajibike!
 
mweee.....nimeudhika sana kwa kweli.....raha ya mume mkae ndani mwenu muanzishe familia yenu......ndugu wakija leo kesho waondoke......mama mkwe kuja kukaa kwangu hilo ni kosa la jinai.....coz hata mama yangu hawezi kukubali kukaa kwangu......
We hujakasirika kama mimi kha
 
Kuna baadhi ya makabila yanasifika kwa hii tabia, ukiolewa ujue umeolewa na ukoo mzima na ukioa ujue umeoa ukoo mzima, lakini huyo bi dada aliona hali halisi toka mwanzo kwa nini alikubali??
 
kuishi na ndugu lawama katika maisha ya ndoa bora muishi peke yenu ndugu wahudumiwe huko waliko angalau kunakuwa na amani. pili wanaume inabidi tuwe na msimamo hasa tunapoishi na ndugu. mshauri mumeo mhame na watoto mkae mbali kidogo. ila hatma ya amani na furaha ya moyoni mwako iko mikononi mwako ndoa isikuweke kifungoni za JF changanya na zako
 
Back
Top Bottom