Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
Image captionMahujaji
Saudia inatarajiwa kuwapatia bangili za kielektroniki mahujaji wanaoelekea Mecca kwa Hajj ya mwaka huu ambalo ni kongomano kubwa la Waislamu kutoka kote duniani.
Hatua hiyo inafuatia mkanyagano uliotokea mwaka uliopita ambapo zaidi ya mahujaji 750 wanaaminikia kuuawa huku wengine 900 wakijeruhiwa.
Image captionMahujaji
Bangili hizo zitakuwa na habari za kibinafsi za kila hujaji pamoja na zile za matibabu kusaidia mamlaka ya Saudia kuwatambua na kuwalinda mahujaji hao.
Takriban kamera 1000 pia zimewekwa.
Image captionMahujaji
Bangili hiyo ya utambulisho itukuwa na habari muhimu kama vile pasipoti na anwani lakini pia zitatoa habari kwa mahujaji kama vile mda wa ibada pamoja na lugha tofauti kuwasaidia wale wasiozungumza lugha ya Kiarabu wakati huo.
Bangili hizo zitakuwa haziingii maji na zitaunganishwa na programu ya ramani