Mahujaji Waislamu kuvalishwa bangili za kielektroniki

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
160530033109_hajj_640x360_bbc_nocredit.jpg

Saudia inatarajiwa kuwapatia bangili za kielektroniki mahujaji wanaoelekea Mecca kwa Hajj ya mwaka huu ambalo ni kongomano kubwa la Waislamu kutoka kote duniani.

Hatua hiyo inafuatia mkanyagano uliotokea mwaka uliopita ambapo zaidi ya mahujaji 750 wanaaminikia kuuawa huku wengine 900 wakijeruhiwa.

160529154036_hajj_624x351_getty.jpg

Bangili hizo zitakuwa na habari za kibinafsi za kila hujaji pamoja na zile za matibabu kusaidia mamlaka ya Saudia kuwatambua na kuwalinda mahujaji hao.

Takriban kamera 1000 pia zimewekwa.

160529102929_hajj_640x360_ap_nocredit.jpg

Bangili hiyo ya utambulisho itukuwa na habari muhimu kama vile pasipoti na anwani lakini pia zitatoa habari kwa mahujaji kama vile mda wa ibada pamoja na lugha tofauti kuwasaidia wale wasiozungumza lugha ya Kiarabu wakati huo.

Bangili hizo zitakuwa haziingii maji na zitaunganishwa na programu ya ramani.

Chanzo: BBC
 
MI NILIDHANI BANGILI hizo zitazuia watu wasikanyagane au ku zitawaelekeza watu nna nzuri ya kujipanga distance kati ya mtu na mtu kasi gani itumike kutembea(yaani ukizidisha mwendo na kumkaribia mwenzako inakubana kidizain flani au kukupa alarm hivyo unaji panga vyema bila kumuathiri mwenzako)

AU MIMI NDIO SIJAELEWA ZINA UHUSIANO GANI NASWALA ZIMA LA KUKANYAGANA HADI KUPELEKEA UMAUTI KWA BAADHI YA WATU?
Je ni kwa ajili ya matibabu pindi itakapo tokea na kuwa na taarifa binafsi za mtu tu?
 
NILIDHANI BANGILI hizo zitazuia watu wasikanyagane au zitawaelekeza watu namna nzuri ya kujipanga distance kati ya mtu na mtu kasi gani itumike kutembea(yaani ukizidisha mwendo na kumkaribia mwenzako inakubana kidizain flani au kukupa alarm hivyo unaji panga vyema bila kumuathiri mwenzako)

AU MIMI NDIO SIJAELEWA ZINA UHUSIANO GANI NASWALA ZIMA LA KUKANYAGANA HADI KUPELEKEA UMAUTI KWA BAADHI YA WATU?
Je ni kwa ajili ya matibabu pindi itakapo tokea na kuwa na taarifa binafsi za mtu tu?
Kweli kabisa, hata mimi nilikuwa nafikiri wamebuni mbinu ya kupunguza vifo, kumbe wamebuni njia ya kuwatambua watu wakifa!! Nadhani waende mbele zaidi wazuie uwezekano wa kutokea mikanyagano.
 
MI NILIDHANI BANGILI hizo zitazuia watu wasikanyagane au ku zitawaelekeza watu nna nzuri ya kujipanga distance kati ya mtu na mtu kasi gani itumike kutembea(yaani ukizidisha mwendo na kumkaribia mwenzako inakubana kidizain flani au kukupa alarm hivyo unaji panga vyema bila kumuathiri mwenzako)

AU MIMI NDIO SIJAELEWA ZINA UHUSIANO GANI NASWALA ZIMA LA KUKANYAGANA HADI KUPELEKEA UMAUTI KWA BAADHI YA WATU?
Je ni kwa ajili ya matibabu pindi itakapo tokea na kuwa na taarifa binafsi za mtu tu?
Yaani ni kwamba, ukikanyagwa kwa kiwango cha kutotambulika, wanasoma taarifa zako kwenye bangili. Nothing more!
 
Yaani ni kwamba, ukikanyagwa kwa kiwango cha kutotambulika, wanasoma taarifa zako kwenye bangili. Nothing more!
ahaaaa na watu wanashangilia?

yaani hapo ni sawa na kutupa taarifa kuwa vifo huko havitakwepeka kwahiyo ili watoe takwimu sahihi wameamua kuwavalisha bamgili aaahahahhaa mfungo mwema wa Ramadhani shekhe!
 
Hivi haiwezekani wakaanzisha utaratibu mahujaji wasikanyagane? Labda mahujaji wagawanywe katika makundi madogo kupunguza msongamano? Miaka mingi sasa mahujaji wanakanyagana hadi kufariki. Tena si idadi ndogo, mamia anapoteza maisha. Je haiwezekani kuwa na utararibu? Au ni sawa tu mahujaji wadhurike? Nini hasa kinaendelea wakati wa hija? Haya mambo yanashangaza lakini inaonekana kama yemezoeleka.....noma sana.
 
Ha ha ha! Wafia dini utasikia kila mara wakisema kitabu chao kimekamilika kila idara; kwamba hakuna ambacho kitabu kimebakiza kuhusu maisha ya mwanadamu tangu kutungwa mimba hadi mauti yake; eti hata namna ya "kupuu" au kumwingilia mkeo iko well narrated kuanzia muda, mkao, etc.

Sasa naomba waje hapa watueleze ni mstari upi huo unaosema mahujaji watavalishwa bangili za utambulisho kama wanyama! Hii ni dharau ya hali ya juu kabisa.
 
Hivi haiwezekani wakaanzisha utaratibu mahujaji wasikanyagane? Labda mahujaji wagawanywe katika makundi madogo kupunguza msongamano? Miaka mingi sasa mahujaji wanakanyagana hadi kufariki. Tena si idadi ndogo, mamia anapoteza maisha. Je haiwezekani kuwa na utararibu? Au ni sawa tu mahujaji wadhurike? Nini hasa kinaendelea wakati wa hija? Haya mambo yanashangaza lakini inaonekana kama yemezoeleka.....noma sana.
Makafara hayo Mkuu; ni lazima yawepo ili mambo yaende ...
 
Back
Top Bottom