Sungurampole
JF-Expert Member
- Nov 17, 2007
- 984
- 205
Kwa siku za karibuni tumekubaliana katika mengi yanayokwenda vibaya kama nchi. Ambacho hatukubaliani ni njia ipi na mikakati ipi itumike kuyakabili na kuyarekebisha yale tunayofanya vibaya.
Nijikite kwa moja ambalo tunakubaliana Watanzania wa leo hatuna uzalendo.
Makundi yote, watawala, wanasiasa, watawaliwa na hata mafisadi wanakubali hili.
Tukirudi upande wa pili katika nini kifanyike ili kurudisha UZALENDO, hapo tunaanza kuachana. Kila mmoja anakuja na mbinu na mkakati wake. Kwa leo naomba tujikite kuangalia moja ya mikakati unayozungumziwa sana Tutoe mafunzo juu ya uzalendo shuleni kuanzia msingi .ikiwezekana toka chekechea.
Binafsi naamini elimu ni mkakati mzuri katika mambo mengi lakini tunaanza lini na tunaanzaje kufundisha?
Nionavyo mimi tumekwisha anza kufundisha tena kwa bidii kubwa.
Hivi somo la ubaya wa ulevi tukimpa baba afundishe saa 5 usiku akiwa amerudi amependeza na mkononi amebeba kiroba litaelewekaje?
Hapa watoto wale hawatamwelewa na huenda wengine wakaanza kuvizia kiroba kile nao waonje waone anachafurahia baba.
Je, ni mtoto yupi atakubali mahubiri ya uzalendo wakati anafundishwa akiwa amekaa kwenye jiwe darasa la vumbi lisilo na dirisha wala mlango wakati anajua mwenzake wa jirani anasoma ulaya kwa rasilimali zetu?
Naamini tumeanza siku nyingi kuwafundisha watoto wetu somo la uzalendo, ni vile tu tunatumia njia mbaya- tunawapa machungu na kuwajengea vinyongo(wimbo wa mjomba). Mtoto anayekalia jiwe anafundishwa na anajua ubaya wa kuwa mzalendo. Kwa bahati mbaya zaidi awe na baba ambaye amefanya kazi serikalini kwa uaminifu mpaka akastaafu na sasa anaishi Manzese na anategemea pensheni kiduchu, TV ni mpaka wakatizame kwa jirani.
Naomba Great thinkers tutafakari na kujadili hili la kufundisha uzalendo.
:hungry: