Mahrez ni better kuliko Drogba?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,229
116,840
Natamani Leicester wachukue ubingwa
naamini pia mchezaji wao Mahrez amestahili kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka

lakini niliposikia atakuwa 'mwafrika wa kwanza kushinda tuzo hiyo'

nikajikuta najiuliza ina maana Drogba hakuwahi kustahili kushinda?
na wengineo je waafrika?

Nakumbuka Benni Mc Carthy aliwahi shinda kiatu cha silver EPL akiwa mfungaji bora wa pili
lakini sikuwahi kusikia hata kutajwa tu kugombania hiyo tuzo
tena alikuwa akichezea timu sio kubwa na sio kali sana lakini alifunga magoli tele...

na waafrika wengine wengi tu ....

je hawakustahili kushinda tuzo hiyo?
 
mkuu unajaribu kulinganisha mbingu na dunia? au almas na shaba? yaani huyo mahrez umlinganishe na striking machine dogba?
 
Kiwango cha ligi ya EPL kwa sasa kimeshuka,Mahrez angekuwa enzi zile asingeweza kuchukua hiyo tuzo.Drogba amecheza kipindi ambacho Liverpool,Manchester United na Chelsea walichukua UEFA Champions League lakini siku hizi wamekuwa wasindikizaji
 
Sometimes ni masuala ya bahati ya mtu. Drogba ni fundi sana ila wakati wake kulikuwa na mafundi zaidi ndio maana hakuchukua.

Ila kwa sasa Mahrez hana mpinzani serious kwa kuwa wakubwa timu zao zipo hoi hata wachezaji wao ni hoi.

Maana Fabio Cannavaro amebeba Ballon D'or wakati mtu kama Iniesta hajawahi hata kuibeba licha ya ufundi wake wa soka uliotukuka.

Hivyo ni bahati ya mtu katika kile kipindi anachocheza.
 
Drogba habari nyingine wewe ,ingia kwenye yutube uone magori aliyowafunga vinala wa soka kama Bayern,PSG,Real Madrid,Bacelona nk

article-1334782917466-12A8975D000005DC-188746_636x407.jpg
 
Natamani Leicester wachukue ubingwa
naamini pia mchezaji wao Mahrez amestahili kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka

lakini niliposikia atakuwa 'mwafrika wa kwanza kushinda tuzo hiyo'

nikajikuta najiuliza ina maana Drogba hakuwahi kustahili kushinda?
na wengineo je waafrika?

Nakumbuka Benni Mc Carthy aliwahi shinda kiatu cha silver EPL akiwa mfungaji bora wa pili
lakini sikuwahi kusikia hata kutajwa tu kugombania hiyo tuzo
tena alikuwa akichezea timu sio kubwa na sio kali sana lakini alifunga magoli tele...

na waafrika wengine wengi tu ....

je hawakustahili kushinda tuzo hiyo?

Kaka hapa issue ipo kwenye unacheza mpira kipindi gani? Unashindana na nani?, kwa sasa kwenye EPL ukitaja wachezaji watano bora kabisa jina la Mahrez haliwezi kosa, wachezaji kama Hazard, Ozil na wengineo, wameshindwa kwa kiasi fulani kuonyesha viwango vya kuridhisha vya kuweza kunyanyua timu zao.

Hebu angalia uchezaji bora wa Dunia, tunaona ni Messi na Ronaldo tu ndio wanaoshindania hiyo tuzo, na kweli wanaonekana wao tu, lakini kweli Ronaldo angeingia kwenye kitimtimu cha Uchezaji bora wakati wa kina Gaucho, De lima, Zidane, Figo?

Huyo jamaa anastahili kupewa, maana kaonyesha mpira mzuri na kaisaidia sana timu yake japo haina kikosi cha maana
 
Drogba garasa hilo alikua na mpira wa kizamani kulala kwenye migongo ya watu ili afunge halafu kipindi cha Drogba alikuwapo Ronaldo on fire Rooney on fire Torres on fire unategemea nini sasa hapo nakubali mahrez ni fundi kuliko Drogba
 
Mchezaji kucheza vizuri na kuonekana yupo vizuri inategemea majira ya Ligi pamoja na timu ina perform kwa kipindi flani,kama unakumbuka msimu wa mwaka jana namna hazard alivyokuwa vizuri na namna alivyoisaidia timu yake kuchukua vikombe mbalimbali,huu ni msimu tu wa Maherez kufanya vizuri kwa sababu macho yote kwa Lester city kwa sasa Leicester ipo vizuri,Tunachozungumzia hapa sio msimu ,tunazongumzia namna yupo vizuri na ameweza kuisaidia timu yake kufanya vizuri kwa misimu tofauti,Maherez huwezi kuwafananisha na kina Rooney ,Drogba,Van Persia na wengine wengi walioperform vizuri kwa misimu mfurulizo.Nitawapa mfano Mahrez alikuwa Leicester to 2014 ,Leicester city haikufanya vizuri na mpaka hii timu ilikaribia kushuka daraja.Mahrez huwezi kumfananisha na Drogba tuache ushabibiki.
 
Riyad Mahrez: “I’m not better than Yaya Toure or Drogba!”
After winning the best player in the English Premier League‘s trophy, Riyad Mahrez expressed his big happiness to the press. The Algerian player said during an interview after winning this trophy: “I’m really proud for this achievement. I can’t find the words to describe my happiness. One thing is sure, my teammates are the main reason behind this success”.

Riyad Mahrez added: “Being the first African player to win this trophy ? I didn’t know it! Drogba and Yaya Touredidn’t win it ? I’m not better than those two big names for sure!”.

Riyad Mahrez scored 17 goals and made 11 assists this season with Leicester City.

Copyright : Riyad Mahrez: “I’m not better than Yaya Toure or Drogba!” | BONGO YETU
 
ivyo vigezo Okocha hakuwahi kuwa mchezaji bora wa Afrika inataka kusema huyo wa dortmund ni bora kuriko Okocha?
 
Back
Top Bottom