Mahojiano ya Rais mstaafu Ally H. Mwinyi na BBC: Akumbuka kundi la Wabunge wakaidi G.55

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,471
Habari JF siasa.

Niende kwenye mada hapo juu.
Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi amefanyiwa mahojiano na BBC radio Leo asubuhi. Ktk mahojiano hayo anakumbuka kundi la wabunge waliodai serikali tatu la G 55. Wabunge hao walidai serikali ya Zanzibar, Tanganyika na ya Muungano. Alimshukuru Mwl Nyerere kwa kulimaliza sakata hilo la wabunge hawa.

Pia anakumbuka alivyofungua milango kwa kuruhusu bidhaa mbalimbali kuingia nchini na kumaliza uhaba wa bidhaa muhimu. Hii ilijulikana kama Sera za Ruksa.


Anadai hadi Leo akikatiza mitaa ya Tandika, vijana humshangilia na kumwambia Mzee Ruksa chukua Fomu ugombee tena sisi tutakuchangia.

Mola ampe Maisha marefu Mzee Ruksa.
 
Huyu atachangulika pamoja na umri wake sio huyu mwingine akitoka
 
Back
Top Bottom