Mahojiano Mbatia ITV jana yamenigusa

Mahojiano Mbatia ITV jana yamenigusa

kichema

Senior Member
Joined
Mar 31, 2015
Posts
137
Reaction score
39
Ndugu wana JF, jana Mh. Mbatia amekuwa na mahojiano na ITV kwa takribani dakika 45 akiwa na Ndg. Buohera. Amezungumuza mengi sana lakini kibwa alichoongea na kikanigusa ni SERA MPYA YA ELIMU. Alitamka mwenyewe kabisa kuwa hii kitu ya elimu haina mshiko kabisa na ajamuelewa nani alimdanganya Rais Kikwete na kumfanya azindue mkenge huo.

Kimsingi alinigusa pale aliposema Tunahitaji elimu ya Kujitambua. Hii ndo itatusogeza mbele pale tunapotaka kuwa 2025.

Nimefurahishwa na alivyojenga hoja na jinsi alivyoweza kuilinda na kupambana na maswali ya Buohera. Nimefurahishwa na jinsi alivyoweza kutambua jinsi gani Profesa wa sasa walivyo choka kuanzia vaa yao na fikira. Jinsi gani graduate wetu wa sasa walivyo Bora iende.

Ndugu wana JF mjadala huo ulikuwa moto sana na kama tunaweza kuudadadua unaweza kutuletea mshiko kwenye elimu yetu hapa Bongo ambayo imekuwa Bora Iende.

===============Penye nia, Pana Njia=================
 
Hivi vyama vya siasa vya upinzani ifike mahali viwe vinafanya mambo kwa matendo walau hata kwa uchache tu...

Kila siku kuiponda serikali kwa maneno haina msaada na wala haitoi fundisho kwa wapiga kura...
Serikali haikubali kuwapa nafasi ya kuonyesha matendo yao. Labda rais ajaye ajaribu ili tuone makali yao.
Lakini Dr. Slaa amefanya kwa matendo kule kwao kwa upande wa uduma za kijamii.
 
Nwenye macho haambiwi tazama mpaka ss tumefaulu kuleta BRN Ya kuongeza madaraja ya ufaulu huku kwetu kuna DIVISION FIVE na wengine wanafaulu mtihani wa Drs vii hawajui kusoma na kuandika
 
Hivi vyama vya siasa vya upinzani ifike mahali viwe vinafanya mambo kwa matendo walau hata kwa uchache tu...

Kila siku kuiponda serikali kwa maneno haina msaada na wala haitoi fundisho kwa wapiga kura...

Mkuu sana Watu8, mfano katika swala hili la Elimu unadhania hawa wapinzani wafanye nini "kwa matendo", na kupitia jukwaa gani?

Maana wao ni wapiga miluzi tu wa kuwaambia watawala hili si bora tunadhani mwapaswa kufanya hivi.

Mfano wakati wa kampeni 2010 CHADEMA Walipiga " kelele" hizi hizi kuwa wakipewa dola elimu itakuwa bure, tukawachamba kuwa ooo kazi zao kuongea tu hawafanyi matendo!

Leo miaka mitano sasa hao hao walikuwa wanadai wapinzanini ni wapiga kelele na hawafanyi "matendo" ndio wanaimplement sera zao!
 
Last edited by a moderator:
Hivi vyama vya siasa vya upinzani ifike mahali viwe vinafanya mambo kwa matendo walau hata kwa uchache tu...

Kila siku kuiponda serikali kwa maneno haina msaada na wala haitoi fundisho kwa wapiga kura...

Mkuu Watu8, wapinzani hawana serikali...wataonyeshea wapi matendo yao...!!?

Tafakari...
 
Serikali haikubali kuwapa nafasi ya kuonyesha matendo yao. Labda rais ajaye ajaribu ili tuone makali yao.
Lakini Dr. Slaa amefanya kwa matendo kule kwao kwa upande wa uduma za kijamii.

Mkuu vyama walau viwe hata na zahanati kama sio mahospitali nk

Vijenge mfumo wa vitendo wa kuaminiwa zaidi na wapiga kura...

Kukosoa kuwe kwa matendo zaidi...
 
Tenga muda wako isome hiyo sera vizuri alafu urudi hapa with concrete arguments. Hii tabia ya kusubiri kusikia toka kwa mtu ni hatari kwa ustawi wa taifa letu
 
Mkuu mathalani katika sekta ya elimu, hapa ndipo ambapo kuna fursa ya wazi kabisa...

Wapinzani wangeweza japo kujenga shule walau katika kila jimbo wanaloshikilia...

Halafu sasa ile sera yao ya elimu bora, elimu bure wangeifanya kwa vitendo...

Kuweza kupata kura za Watanzania inakupasa kwanza uthubutu kujenga kuaminika...

Kupiga kelele za kuikosoa serikali pekee haitoshi maana hata sisi tusio wanasiasa tunaona udhaifu uliopo lakini hatuoni mwenye kuonesha mfano na kuongoza njia Watanzania watayoifuata...

Mkuu sana Watu8, mfano katika swala hili la Elimu unadhania hawa wapinzani wafanye nini "kwa matendo", na kupitia jukwaa gani?

Mfano wakati wa kampeni 2010 CHADEMA Walipiga " kelele" hizi hizi kuwa wakipewa dola elimu itakuwa bure, tukawachamba kuwa ooo kazi zao kuongea tu hawafanyi matendo!

Leo miaka mitano sasa hao hao walikuwa wanadai wapinzanini ni wapiga kelele na hawafanyi "matendo" ndio wanaimplement sera zao!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu huitaji serikali kuonesha sera na ilani kwa vitendo...

Mathalani kama chama cha siasa cha upinzani, huitaji kuwa na serikali kuanzisha mashamba ya kilimo cha kisasa ambapo wananchi wataalikwa kujifunza huko...

Kama chama cha siasa huitaji kuwa na serikali kuweka na kusambaza mfumo mzuri wa kutupa takataka mijini badala ya watu kutupa tu hivyo takataka...

Yapo mambo mengi mkuu ni suala la kuamua tu no vipi unawaonesha Watanzania kuwa mnaweza kuwaongoza na hata wakiwapa dhamana mtawafikisha wapi...

Mkuu Watu8, wapinzani hawana serikali...wataonyeshea wapi matendo yao...!!?

Tafakari...
 
Malalika;

Je umesoma bajeti kivuli ya Elimu? Hilo suala la bure sijaliona. Sorry
 
Last edited by a moderator:
Mkuu vyama walau viwe hata na zahanati kama sio mahospitali nk

Vijenge mfumo wa vitendo wa kuaminiwa zaidi na wapiga kura...

Kukosoa kuwe kwa matendo zaidi...

Hii inaweza kuwa innovation kwenye siasa lakini utekelezaji wake sio rahisi hivyo. Mfano Chadema au CUF wakiwa na hospitali yao mkoa fulani, kwa vyanzo vyao vya fedha ni ngumu kumudu operesheni cost sustainably. Viti vya ubunge vikipungua na ruzuku inapungua. Kulipa madaktari na wauguzi kila mwezi na kumudu gharama nyingine sio suala dogo. Njia pekee ni collaboration na serikali,mathalani wasaidie kulipa mishahara ya watendaji. Swali ni: je serikali unadhani inaweza kufanya kitu kama hicho? Wakati majimbo tu ya upinzani wanayabana kwenye bajeti ili wabunge wake waonekana mizigo.
 
Watu8;

Mkuu hivi upo ndani ya Tanzania hii kweli ..!?
Jaribu siku Moja kwenda kufatilia tenda yoyote ile utapata majibu ya uwazayo. Najua bado unamapenzi moto moto na wananchi wa nchii hii ila tatizo ni kujua kama na wao bado wanajipenda ndio swali gumu pia.
 
Last edited by a moderator:
Hivi vyama vya siasa vya upinzani ifike mahali viwe vinafanya mambo kwa matendo walau hata kwa uchache tu...

Kila siku kuiponda serikali kwa maneno haina msaada na wala haitoi fundisho kwa wapiga kura...

watafanyia wapi wakati hwawsikilizwi
 
Hivi vyama vya siasa vya upinzani ifike mahali viwe vinafanya mambo kwa matendo walau hata kwa uchache tu...

Kila siku kuiponda serikali kwa maneno haina msaada na wala haitoi fundisho kwa wapiga kura...

Wakiwezeshwa wanaweza, mwenye kuwezesha ni wewe. Piga kura ya ndiyo kwa mtu mwenye weledi siyo chama chenye weledi.
 
Hivi vyama vya siasa vya upinzani ifike mahali viwe vinafanya mambo kwa matendo walau hata kwa uchache tu...

Kila siku kuiponda serikali kwa maneno haina msaada na wala haitoi fundisho kwa wapiga kura...

Wananyimwa nafasi kama unafiri niungo wapewe uone
 
Sidhani kama hili linaweza kutokea...

Basi hata majengo ya ofisi zao yangeshaamriwa kubomolewa na serikali...

Jenga uone kama kesho hujaambiwa "bomoa hapa ni eneo la wazi"
 
Fursa huwa haisubiriwi hadi upewe bali unaitafuta ilipo na kuinyakua...

Wananchi sisi tutawapaje hawa wanaotegemea sauti zao pekee, wanapaswa kuwa wanaharakati wakati huo huo wanasiasa...

Wanapaswa kuamsha hamasa ya maendeleo kwa wananchi si hadi wapewe nchi...

Wananyimwa nafasi kama unafiri niungo wapewe uone
 
Back
Top Bottom