Mahojiano Maalum: Mhe. Lema na Mhe. Msigwa wakiongelea swala la Mhe. Lissu kwenye kituo cha KTN cha habari nchini Kenya

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,323
24,230
Dakika 56 za Mahojiano maalum ya KTN News Kenya, Godbless Lema na Mchg. Peter Msigwa

Maswali na majibu ya mwendesha kipindi KTN Bw. Paul Nabiswa na pia wananchi kupiga simu kutoka sehemu mbalimbali za Kenya kuwauliza maswali wabunge machachari wa CHADEMA kuhusu siasa za Tanzania.

Hii ni Video ya Mahojiano Kati ya KTN na Mbunge Godbless Lema na Mbunge Peter Msigwa wakizungumzia hasa Swala la Jaribio la Kumuua Mbunge Tundu Lisu kwa Risasi.

Pia demokrasia katika nchi za Afrika pamoja na umuhimu wa uhuru wa mihimili mitatu ya dola yaani Serikali, Mahakama na Bunge. Mahusiano ya demokrasia huru na ukuzi wa kiuchumi. Siasa za ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla .....


Source: KTN Kenya news / Thobias Marandu
 
Lugha ya Malkia imewafanya washindwe kufunguka
Ingekuwa kwa Kiswahili tungemkoma Msigwa

Lema kabaki na Actually actually actually hahahaaa
 
Lugha ya Malkia imewafanya washindwe kufunguka
Ingekuwa kwa Kiswahili tungemkoma Msigwa

Lema kabaki na Actually actually actually hahahaaa

Mkuu
Mahojiano katika kipindi hiki ni exclusively katika lugha ya taifa ya Kiswahili mwanzo-mwisho kinachotumika na wengi na ni tofauti na majadiliado yale ya mwanzo katika lugha ya Kiingereza.
 
Back
Top Bottom