Mahitaji ya mwanamke na mwanaume katika mapenzi

Mahitaji ya mwanamke na mwanaume katika mapenzi

mpalu

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2010
Posts
2,521
Reaction score
876
MAHITAJI YA MWANAMKE: JITAHIDI KUMFANYA MPENZI WAKO AFURAHI

1.
Ulinzi (security) – mwanamke anapenda kuhakikishiwa ulinzi na usalama wake kiafya, kihisia, na kiuchumi. Sio yeye tu bali na familia yake yote.

2.Mazungumzo (conversation) – mwanamke huumizwa sana na vipindi virefu vya ukimya, sio tu kwamba wanataka mazungumzo bali mazungumzo yenye hamasa na mvuto

3.Kumwamini (trust) – mwanamke anakiu ya kuaminiwa, anataka mtu aliye muwazi, asiye ficha kitu chochote, anatamani umwamini na sio kuhofia kila anachokifanya au kumhofu kila aliyeko naye

4.
Mvuto na ukaribu (affection) – maneno na matendo yachochee mvuto na ukaribu, Kwamfano. Kukubali alivyopendeza, kumsifia nk

5.Ushirikishwaji ktk mambo ya familia (participation) – Sio kila kitu kinafanyika yeye hajuo, anaona tu vitu vinaenda kama vile yeye sio mmoja wa wanafamilia na mzazi. Mfano, anagundua unasomesha ndugu yako pasipo hata yeye kujua. Mwanamke anatamani kuona anashirikishwa katika yote yahusuyo nyumbani kwake maana kwake nyumbani ndiyo kitovu cha maisha yake zaidi ya kazi yake na marafiki zake

MAHITAJI YA MWANAUME:KILA SIKU HAKIKISHA ANAFURAHI

1.Kutoshelezwa ktk tendo la ndoa – kuambiwa umependeza, nakupenda kunaweza kumtosheleza mwanamke lakini sio mwanaume, yeye anahitaji kushiba tendo la ndo

2.Heshima – Mwanaume huyatafsiri matendo yote yanayoonyesha heshima kama upendo au penzi kwake, heshima hapa haijalishi umemzidi mume wako kiwango cha elimu, uwezo wa fedha, fursa au hata kujulikana. Wakati mwanaume anajukumu la kuonyesha penzi kwa mke wake, mwanamke hana budi kuonyesha heshima kwa mumewe.

3.Mwanamke anayevutia – jiweke safi, jitunze na uvutie ili kumfanya mume wako akutoshek

4.Kiu ya kuwa na nyumbani kusafi – pamoja na kwamba anaweza asiwe msafi kama wewe lakini ana kiu ya kuona kwake ni kusafi. Anatamani marafiki zake wavutiwe na kwake

5.Kiu ya kukubaliwa (admiration)
– pamoja na madhaifu yake bado anakiu ya wewe kutambua mchango wake na kukubali yote yahusuyo taaluma yake, uwezo wake na mafanikio yake. Heshimu na kubali mchango wake ktk familia

Dk. Chris Mauki

Hapo kwenye TRUST upande wa mwanamke baadhi yetu wanaume panakuwaga pagumu.Ila ili nimuamini kweli mwanamke inambidi ajiweke ktk namna,,hali na mazingira ya mimi kumwamini pasipo na chembe ya shaka.
 
Hapo kwenye TRUST upande wa mwanamke baadhi yetu wanaume panakuwaga pagumu.Ila ili nimuamini kweli mwanamke inambidi ajiweke ktk namna,,hali na mazingira ya mimi kumwamini pasipo na chembe ya shaka.

Asante sana mkuu umenikosha na maneno yako mi kila siku nagombana na shemeji yako kuhusu suala hilo hataki kujiweka kwenye mazingira ya mm kumuamini kabisa japokuwa ni faithfull
 
Loh!!! kumbe unastress za kujeruhiwa na watu wakasonga mbele na maisha ndio maana majuzi ulikuwa unajazba sana na mimi kwenye ile thread. bila shaka unahitaji ushauri nasaha.
alafu wewe mkorofi wewe, alafu unaroho ngumu kweli, sinilikwambia ukafie mbele alafu bado mzima na unaishi... lol..!!
hamna iyo ndo hali halisi buana, nyie kama nyoka hamchelewi kugeuka mbele mkapafanya nyuma na nyuma mbele, kuwaamini tabu sana.
 
Hahahahaha!!! sasa ningefia mbele hayo uyasemayo ungemwambia nani saa hizi?????

Acha usiwe na mtazamo hasi juu ya wanawake bhana, hakuna bin adamu mkamilifu.
 
money for a woman

ha ha..kama kawaida yako ...pesa kwanza....
Lakini pesa inaingia kwenye namba nne.....Ulinzi (security) – mwanamke anapenda kuhakikishiwa ulinzi na usalama wake kiafya, kihisia, na kiuchumi. Sio yeye tu bali na familia yake yote......

Aisee niaje lkn....ndugu yako atoto mzima?
 
Last edited by a moderator:
Asante sana mkuu umenikosha na maneno yako mi kila siku nagombana na shemeji yako kuhusu suala hilo hataki kujiweka kwenye mazingira ya mm kumuamini kabisa japokuwa ni faithfull

vitu gani vinaashiria kwamba hataki kuweka mazingira ya wewe kumuaamini?
 
Lingine ambalo limekuwa shida ama hitaji kubwa sana kwa dada zetu ni kuridhishwa katika tendo la ndoa... Na ili limepelekea wanaume wengi sana kufia Guest..
 
Back
Top Bottom