Maharusi wapigwa marufuku kupaka 'Shedo'

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
LIPS.jpg

Gazeti la Mtanzania jana limeripoti kuwa waumini wanawake wanaokwenda kufunga ndoa katika kanisa Katoliki Parokia ya Hananasif Kinondoni, jijini Dar es salaam wamepigwa marufuku kupaka rangi ya mdomo “lipstick” wakati wa ibada ya misa takatifu ya ndoa.

Gazeti hilo limeongeza kuwa uamuzi huo ulitangazwa juzi jioni na Paroko wa Parokia ya Hananasif Kinondoni jijini Dar es salaam Padri Gasper Mtengeti, wakati wa ibada ya misa ya kumwombea marehemu Rose Michael iliyofanyika kanisani hapo.

Aidha gazeti hilo limeongeza kuwa kutokana na hali hiyo Padri Mtengeti aliwataka wanawake waache kupaka rangi wakati wa misa takatifu ambapo alitoa sababu tatu zinazotokana na Liturujia ya Ekaristi Takatifu (utaratibu wa uendeshaji wa ibada) chini ya kanisa Katoliki.

Padri Mtengeti alieleza sababu hizo kuwakataza maharusi wa kike kujipaka rangi ya mdomo kuwa rangi hiyo inayopakwa huwa inasalia katika chombo kinachobeba divai ambayo kiimani kwa dhehebu hilo ni damu ya Yesu Kristu.

Sababu nyingine iliyoelezwa kupitia gazeti hilo ni pamoja na kuwa rangi ya mdomo huwa inachanganyika na damu ya Yesu wakati wanapokunywa kitendo ambacho si chema mbele za Mungu, sababu nyingine ni kuwa rangi hizo hubaki kwenye kitambaa cheupe kinachotumika kufuta kikombe cha Hostia baada ya kuguswa na midomo.
 
..."sababu nyingine ni kuwa rangi hizo hubaki kwenye kitambaa cheupe kinachotumika kufuta kikombe cha Hostia baada ya kuguswa na midomo"

Hapa ndo huwa nachoka kabsa, kikombe kimoja kutumika na kila mtu, halafu kinafutwa tu kila baada ya mtumiaji.
 
Back
Top Bottom