Maharusi wapanda na kuendesha Tingatinga /Katapila

Maharusi wapanda na kuendesha Tingatinga /Katapila

Bedui la bongo

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2018
Posts
297
Reaction score
307
Mrembo Lilian Peter Ndagiwe mkazi wa Shinyanga Mjini amezua gumzo wakati akifunga ndoa na Ottoh Yanga baada ya kupanda na kuendesha Tinga Tinga /Katapila ambalo hulitumia katika kazi zake katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga.

Wanandoa hao wamepanda kwenye tingatinga hilo muda mfupi leo Disemba 28,2018 walipomaliza kufunga ndoa katika Kanisa la Katoliki Parokia ya Buhangija mjini Shinyanga.

Kama ilivyozoeleka kuwa wanandoa hupanda kwenye magari, lakini kwa wanandoa hawa hali imekuwa tofauti kabisa kwani wao wameamua kupanda kwenye tinga tinga la kutengenezea barabara na kupita nalo mtaani.

Imeelezwa kuwa bibi harusi Lilian Peter ni mtaalamu wa kuendesha tingatinga, kutokana na mahaba aliyonayo kwenye kazi yake ,ili kukamilisha furaha yake ya ndoa basi kaamua kuendesha Tinga Tinga na hakuona haja ya kupanda kwenye gari na mmewe.

IMG_20181228_233352_487.JPG
Screenshot_2018-12-28-23-32-44.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom