Mahari ya Single Mom

Watu kama nyinyi mara nyingi mnaingia kichwa kichwa kwa wanawake ambao wakati mnaanza uhusiano wanakudanganyeni ya kuwa hawana Mtoto, kumbe Mtoto yuko kwa Bibi yake kitambo.

Tena shukuru wanawake wengine Mapenzi yakishakolea ndio wanakuambia, na wewe sababu umeshaingia kichwa kichwa/umependa inabidi utunze siri kwa kuogopa aibu.
Na kuna wanawake wengine hawakuambii mpaka siku unaliona kaburi.

Bado hujawajua vizuri wanawake
 

Pamoja na kuwa na point kuhusu mahusiano ila suala la kusema mahari ya binti wa miaka 18-22 asiye na mtoto uyafananishe na wa 30 mwenye mtoto!. Hapana.
 
Tatizo hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unalaana sio bure
Mimi siwezi kuwa na laana nimezaliwa na mama aliyejitunza hadi kwenye ndoa na wala siyo single father laana unayo wewe single mama uliyezaa hovyo kisha akitokea domo zege wa kukuonea huruma mnajikusanya familia nzima mna-discuss mahari apigwe bei gani as if anaowa bikra,tena kama mimi mkisema hata 80,000/= tu naondoka sitakuwa na muda wa kupatana.

Hapo juu kwenye namba nimemaanisha elfu themanini usije ukapasoma kama laki nane.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Si unaona nilisema unalaana yani unarusha giwe gizan mzee mm bdo mchini hata kutotoa sijaanza ss ww jiropokeshe

Elfu80 kubwa ww hata wa 2k hautampata
 
Mkuu punguza kidogo ukali wa maneno Daah, si vyema sana kuwa na maneno makali hivyo
.........................Tunaokoa kizazi kaka hili jambo siku hizi mabinti wanalichukulia kiwepesi sana kumbuka na sisi tunazaa nachotaka wale waliopo humu na hawajafikia stage inayozungumzwa hapa waogope na wajiepushe na ujinga huu so called “singo mama”.

Hutajisikia vibaya mama yake umuowe akiwa na heshima yake kwa mahari 1.2mill kisha siku ile Mungu amekupa mtoto wa kike anakuja mtoto wa mwenzio unamtajia 1.5mill wakati ndani kuna mjukuu wako aliyetokana na huyu binti,Mimi kwa aibu nitatamka mchukueni tu bure na asante nyingi juu.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Si unaona nilisema unalaana yani unarusha giwe gizan mzee mm bdo mchini hata kutotoa sijaanza ss ww jiropokeshe

Elfu80 kubwa ww hata wa 2k hautampata
Hii ID nakumbuka kubishana nayo somewhere kuhusu mambo haya haya ila wakati huo ilikuwa kuhusu “BIKRA” wewe na mwenzako wakujiita somebody @tufitufi povu liliwatoka kweli kweli na nakumbuka mmoja wenu akakiri post ya #3 baada ya main post kwamba alitolewa bikra akiwa aged 16 sasa sikumbuki kama ni wewe au yule mwenzio.

Nimekufahamu baada ya kuona maandishi yako uliyoandika ukiwa panicked kama wakati ule,anyway siwezi bishana na gume gume ndo kwanza kumekucha nilichoandika hapo juu nimemaanisha kama wewe singo mama ambia ndugu zako akitokea mtu wamwambie asante akuokote mkasaidiane maisha.

Am out!!!

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Bora kaka useme wewe, dah wanaume wengine wana dhihaka sana tasema hawakuzaliwa na wanawake jamani.,,ukimfatili utakuta kenyewe mama ake aliolewa akiwa nako
, alafu dada zake wote wamezalishwa wako nyumbani binamu zake usiseme, ila wakijua humu wanajimwambafaii weeeee as if wanaishi Mars na si huku kwenye jamii zilizojaa ma single mom

Tuwapende na kuwaheshimu, kumbukeni nyie ndo mnaowapa hizo mimba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata milion 5 unatoa kutokana na ulivyompenda.
Mi kuna single mom, alinipenda katika uhai wangu hakuna aliyenipenda sana Kama yeye japo wapo waliokuja badala yake.
Na imani nikifa , tutaonana Tena.
Rest in peace mainah😥😥😥.
😭😭😭😭 mkuu hii comment imenitoa chozi langu imeniumiza sana.
 
Unajua venye naelewaga comments zako my brother from another mama
 
Comments za watoto wadogo na primitives zinajidhihirisha wazi. Hayo mambo ya single mother visababishi ni sisi sisi wanaume. Acheni kuropoka upumbavu nyinyi washenzi.
Unajikutaga diiiingi kuliko sisi kumbe upuuzi tu.

Kuna koo kama yangu ni fedheha kubwa kwa mtoto wa kiume kuoa janamke liliozalishwa kwingine unatengwa na kwenye matambiko huendi na ndugu hawaji tena kwako.

Can you please pretend to be equal with everyone in this platform?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…