Usher-smith MD
JF-Expert Member
- Jul 7, 2015
- 9,509
- 12,191
Ni kijana mwenzangu sekta ya afya, mwaka huu mwanzoni aliamua kwenda kutoa posa kwa binti ambaye alipanga aanzishe naye familia.
Binti mwajiriwa wa serikali na asili yao ni kanda ya ziwa ila wanaishi na familia katika moja mikoa wa Pwani.
Mshenga alitumwa pamoja na baadhi ya wanafamilia wa kijana.
Kijana aliaandaa milioni 2 mfukoni siku hiyo ambayo alishika mjomba wake .
Kusikilizwa laki 2 , kishika uchumba laki 3 , wakatoa cash.
Mahari ikatajwa ng'ombe 10 @400,000/- jumla mil 4 na vitu vingine milioni 1, jumla ya mahari milioni 5 itolewe yote kwa pamoja bila kuacha deni.
Mshenga akabembeleza pale ila wapi. Wakajibiwa kwa mila za kwao kupunguza mahari ni dharau , hilo Jambo haliwezekani.
Basi ule msafara wake ukarudi bila muafaka.
Kabla ya hapo Kijana alipanga na mchumba wake kuwa mahari itakuwa milioni 2.5 so yeye alijua akitoa milioni 2 akibakisha deni la laki 5, kama tunavyooambiana mtaani mahari haimaliziwi.
Kijana akamtafuta yule binti akamuuliza vp mbona mambo yameenda ndivyo sivyo, alipanga 2.5 wametajiwa 5.
Binti akamjibu kuwa yeye yupo na ndugu zake lazima mila ifuatwe.
Kijana akasema sawa ngoja nikajipange tena nitarudi nikikamilisha.
Ila septemba hii jamaa ananimbia anafikiria kughairi lile swala lake.
Mimi nikamwambia hakikisha ili lak 5 yako unarudishiwa .