Ava Sancez
Member
- Jan 27, 2017
- 33
- 50
Taarifa kutoka Somalia zinasema maharamia wa Kisomali wameiteka meli ya mizigo ya India.
Kumezuka utata kuhusu eneo halisi ambako meli hiyo ya kutoka India ilikotekwa.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini vinaarifu kuwa tukio hilo linaarifiwa kutokea Somalia ya kati, eneo la Elhur kiasi ya kilomita 50 kusini mwa Hobyo, eneo ambalo miaka michache iliyopita lilikuwa ndio kitovu cha maharamia wa Kisomali.
Kaimu rais wa eneo la Galmud, Somalia ya kati ameithibitishia BBC kwamba meli ya mizigo imetekwa siku ya Jumamosi karibu na eneo la Haradhere.
Ameeleza kuwa meli hiyo ilikuwa inaelekea Kismayo.
Wakati huo huo maafisa huko Puntland wanasema utekaji huo umefanyika katika eneo lao.
Inaarifiwa kuwa meli hiyo ilikuwa inaelekea Yemen kutoka India wakati ilipotekwa na ina mabaharia 11 ndani.
Mapema mwezi uliopta maharamia katika eneo la Puntland waliiteka meli ya mafuta ambayo baadaye waliachia huru.
Kilikuwa ni kisa cha kwanza cha uharamia kushuhudiwa tangu 2012.
Chanzo: BBC/Swahili