Maharamia wa Somalia waiteka meli yenye bendera ya Panama

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Haramia

Maharamia wa Somalia wameiteka meli ya yenye bendera ya Panama-iliyokua ikisafiri kutoka Muungano wa Kiarabu ikielekea kwenye bandari mjini Mogadishu.

Meli hiyo ilishambuliwa usiku wakati wahudumu wake walipokua wamelala. Shirika la habari la Anadolu limewanukuu maafisa wa jimbo lililojitenga na Somalia la Puntland.

Maharamia sita walihusika katika shambulio hilo kwa mujibu wa gavana wa eneo la Gardafu katika jimbo la Puntland, Musse Salah, ambaye alinukuliwa na Shirika la habari la Reuters.

Maafisa wa eneo la Bari ambako tukio hilo lilitokea wanasema kuwa meli hiyo ilipatwa na matatizo ya kiufundi.
 
Juzi nilikuwa nimetulia natafakari kuhusu yanayoendelea Msumbiji!!

From nowhere nikajikuta najiuliza hivi wale wateka meli wa Kisomali siku hizi wako wapi!!

Badala ya kutafuta jibu, nikaanza kuwaona akilini wateka meli wa "Kisomali" wakipanga kuhamia Msumbiji!!!
 
Haya mambo hayatokei nchi za ulaya ila kwa weusi tu, sijui wametuona mazuzu 🤣🤣
 
Lazima watakuwa wamesaidiwa na wale maharamia wa kwenye pirates of the Caribbean
 
Hawaja jamaa wanaanzisha buashara mbalimbali duniani kea pesa za kiharamia. Hata huvyo hawakosi kuswali swala tano.
 
Back
Top Bottom