Maharage Chande: Tuache kupeana maneno tamutamu; bei ya Tsh 27,000/= haitoshi kuunganisha umeme

Mkuu Mundaliku uko poa kabisa, mbaya na kichekesho ni kwamba unalipia nguzo 2 na unawalipa ths. 600, 000/- na zaidi alafu (then) nguzo hizo wanakuambia sio zako bali ni za TANESCO na wanaanza kuzitumia kwa kuwaunganishia wengine wakati nguzo hizo nimenunua mimi, sasa hapo nani anaibiwa au ANADHURUMIWA?
Tena wanaunganishwa bila kulipia nguzo ili mradi wako jirani na nguzo ulizolipia.
 
Naomba majibu haya :-

Nguzo ni mali ya nani?
Luku / Mita ni mali ya nani?
Tanesco ni Profit au Business oriented?

Je hawajui kwamba pesa watakusanya zaidi wakiwa na wateja wengi zaidi ?. Umeme sio kama mchele unachota kadri unavyotaka ukiwa na megawatts za kutosha (unazalisha inabidi zitumike) unless otherwise hakuna sababu ya kuongeza ma-Megawatt ya kutosha iwapo mahitaji sio makubwa hivyo.

Tukimaliza Bwawa la Nyerere (if ever....) hizo Megawatt tutazitumia wapi?
Faida kubwa ya Tanesco inatakiwa iwe Wakati wa kuuza umeme kwa mteja. Kuweka Bei kubwa ya kuvuta umeme, ni kulimit idadi ya wateja hence Mapato yanayotokana na kuuza umeme.
 
Kwahiyo wewe usiye maharage unaamini kuna umeme wa 27,000/=!

Tupe mchanganuo wa huo umeme kuanzia generation mpaka distribution ili tuone.
tofauti ya kufunga umeme kijijini na mjini ni ipi??? kwanini kijijini iwe 27,000/= alafu mjini wagome???
 
Sijui kwa nini Watanzania mnaelezwa ila hamuelewi. Kuweka umeme nyumbani kwa mtu/mtumiaji ni uwekezaji wa TANESCO. Ni kuisaidia Tanesco kuwekeza kwenye biashara yake ya kuuza umeme; ili mtumiaji aweze kununua nishati na kuiingizia TANESCO mapato. Sasa hoja ya kusema tzs elfu 27 inatoka wapi wakati Tanesco inasaidiwa kuwekeza? Hizo elfu 27 ni mchango wa mwananchi/mtumiaji anayeweka umeme wa Tanesco nyumbani kwake. Kwa nini Tanesco ione mchngo hautoshi wakati ni uwekezaji wake (Tanesco)? Kwa nini Tanesco isiende kwenye soko la mitaji (DSE) kupata mtaji wa kutosha kusambaza (kuwekeza) umeme nchi nzima? Hoja ya Maharage imekaa kimaharage kweli. Ni mipasho tu. Sijui mzaramo huyu ndugu?!
Umeandika vizuri.

Ni kweli kabisa Tanesco wanawekeza ili wafanye biashara yao. Kuweka nguzo ni uwekezaji wenyewe sawa na zile Power line zinazosafirisha umeme toka Kidatu. Hatujawahi kusikia wakisema tulipie yale manguzo ya power line kwa vile ni sehemu ya uwekezaji wao. Hizo ni long term investiment zao .... na wateja tunalipia gharama za umeme kucover all those costs. Ni Tanzania tu ndiyo unakuta this issue become a National issue mpaka inapangiwa bei na serikali. Hiis Tanesco ambayo kila kitu inafanyiwa na serikali kuanzia mitambo mpaka infrastructure za usafirishaji bado inataka kuwakamua wananchi maskini.

Hatujawahi kusikia mashirika ya simu yakiwacharge wateja wao gharama za kujenga minara yao. Nafikiri hii kitu inafanyika Tanzania peke yake!!
 
Tena wanaunganishwa bila kulipia nguzo ili mradi wako jirani na nguzo ulizolipia.
Mkuu nawe umelibaini hilo? Ndio maana tunamashaka
na wachumi wa Project zao. Nguzo moja analipia mtu mmoja kwa bei ya > sh. 300, 000/- inatumika kwa wateja zaidi ya 4, sasa hawa wanalipia tena hiyo nguzo au RUSHWA inachukua nafasi yake?
 
Mkuu tunaye mwongelea alipe 27, 000/- watu wa vijijini. Vitu ulivyo taja pamoja na bei zake wao hawana uwezo huo, sanasana tv inchi 14 ya 50 - 70, 000/- simu ya 10 - 12, 000/- hizo harusi kwa asilimia 90% - 99% ni MKEKA TU.
mkuu vijijini ni 27000
 
Huyu toka wafanye tukio mahali fulani wakishirikiana na msela wake mafuru ndio nikajua kwamba hawa ni wasaliti.
Tanzania inapigwa sana. Poleni wanyonge

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app

Sasa juu ya historia yake mbaya iliyomfanya Jiwe amuondoe hazina , Samia amemrudisha Mafuru Hazina kuwa naibu Katibu Mkuu !! Hivi Samia Kweli alikuwa anaunga mkono juhudi na maamuzi ya Jiwe au alikuwa ndio anasambaza siri za Jiwe kwa KIGOGO?
 
Serikali TANESCO ni wezi tu,mtu unatoa 500k uunganishiwe umeme halafu

Luku wanakwambia ni mali yao,Nguzo mali Yao tena kama ukitaka umeme na Nguzo

Bei inaongezeka zaidi na zaidi kutegemea na uhitaji wa nguzo watakazoweka,Hiyo hela mteja

anayolipa huwa ni ya nini au inaenda wapi? Maana kila kitu pale ni mali ya TANESCO haya mahela wanayoyataka n yanini kama sio wizi wa wazi wazi?

Umeme ulitakiwa ubaki kwenye 27,000 kama kweli kila kitu ni mali ya TANESCO, lakini kurudsha bei ya zamani na wakati vifaa vyote ni mali yao huo ni uwizi.

ifike Mahali watanzania wawe service Free,tujue tu gharama za kupata huduma ila sio kuletewa huduma,Naamini akipatikana RAIS anaejua hesabu vyema vyema Hta ahiyo 27,000 anaweza akaiondoa akasema watu watoe 10,000Tsh,

YES inawezekana,n namna tu ya kupangilia na kujua NAMNA ya kufanya... Tanesco isiwashe gari kwenda kuwekea luku mteja mmoja mmoja,otherwise mteja aamue kulipia gharama extra.

ila waweke tu utaratbu Wateja wakifika 50 ndio gari inawashwa wanaenda fungia watu LUKU,shida ninayoiona hapa ni Hajapatikana mtaalamu wakupga hesabu akaziwasilisha mezani watu wakazielewa.

kinachofanyika sasa hivi ni wizi wa wazi wazi,N sawa na mtu ananunua Gari online analipia kila kitu usajili kila kitu kinasoma jina lake lakini Siku unapewa unaambiwa hili n gari lako ila huruhusiwi kufanya chochote wala kumpa mtu aendeshe, yani masharti kibaoooooo, BASI mngenipa bure hilo gari basi nijue 1 kama yafanyavyo makampuni mengine yanayogawa magari kwa wafanyakazi zao.

kwa hili la tanesco nadhani linadhihirisha UWEZO wa upeo wa RAIS tulie nae FULL STOP.
 
Huku weng ni wawamva ngoma wanavutia kwa upande wao ila kmsingi ndugu alitoa ufafanuzi wa kina na wa kueleweka utafikir kafanya Kazi miaka 20 Tanesco
 
Kiufupi kuunganishiwa umeme ilipaswa kuwa bure!
Mimi nadhani ingechorwa ramani ambapo Tanesco inapitisha nguzo zao kulingana na eneo husika!Walioko nje ya Mpango ndio walipie gharama za kupelekewa mpaka huko!Halafu siku wateja wakiongezeka kwenye mkondo Huo basi mtu aliyelipa Kwa gharama zake awe anarejeshewa fedha aliyotumia kidogo kidogo!
 
Akili za maharage bana...yaani mazoea ni kitu kibaya sana ..yaani unaniuzia vifaa kwa bei ya soko lakini bado unasema ni mali yako...hivi mita , waya, nguzo ni mali ya nani?nikinunua nguzo nitatumia peke yangu?kama Tanesco haina fedha basi itukope itulipe umeme...yaani nikilipia vifaa vya laki 4 wakishaniunganishia waniwekee na umeme wa laki 4 ...Maharage ajue mtumiaji wa umeme ana wajibu wa kulipa matumizi ya umeme tu.
 
Hawa wizara na management nzima wamekalia maneno mengi wakati hatuna tunachokiona zaidi ya nchi kuwa gizani kila kukicha. Watu wanaendesha makampuni bila umeme.. nyumba zinashinda kutwa na kulala bila umeme. Nchi imerudi nyumaaa
 
Tupo tunajipepea kwa makaratasi na magazeti hapa. Jirani zangu wameamua wao kulala nje barazani. Umeme katenj tu hata moja kwa moja. Nyie endeleeni kula nchi bwana Maharage. Ila 2025 si mbali. Hatutaangalia cha mwanamke wala special group yoyote.
 
Back
Top Bottom