Maharage Chande, MD mpya TANESCO ni nani?

Maharage Chande, MD mpya TANESCO ni nani?

Maharage chande hana nasaba zozote na kina chande wanaotajwa wa awamu ya nne na ya tano. Binafsi namfahamu ni mtu yuko very objective, modern and result oriented. Ukiwa mvivu huwezi kufanya kazi chini ya maharage naunga mkono uteuzi wake sababu najua akienda na spirit aliyonayo mwenyewe ya ku achieve beyond targets itasaidia kuondoa utendaji wa mazoea wa Tanesco.

Alijaribu mzee Idrisa Rashid kuitrasnform tanesco lakini alikwama kutokana na wazee aliowakuta Tanesco yaani hata vijana tanesco wanautendaji kama wa wazee very slow, hawatendi mpaka wapate kitu kidogo.

Nadhani ana direct connection na mambo ya IT yaliyofanyika 2015 kwenye uchaguzi chini ya uratibu wa Januzaj. Kwa wengine wasio na macho watu wengine wanachaguliwa ili kuweka logistics sawa uchaguzi ujao 2025.
Result oriented wa huu mgawo unaoendelea?
 
Mimi mama namuunga mkono 100% kuifumua tanesco , wateuliwa wa jpm walikuwa nakiburi mno , kazi ilikuwa nikumsifia rais na kusema uongo. Eti kuunganishiwa umeme 27000/= 🤣🤣 tena huyo karemanii alichereweshwa.
Sawa mgawo usikuwa na kikomo, kwaiyo Chande ni mtu sahihi kuliko Karemanii😂
 
Inaonekana jamaa ana kitu kizuri, tumpe muda ...
Je hadi sasa hiko kitu kizuri cha maharage ya chande umeshakipata kutoka kwa huyu aliyekuwa MD wa DSTv Tanzania? Graduate wa Master of Buisiness Administration from the University of South Africa ambaye hana utalaam wo wote wa umeme lakini sisi tukaona ndiye mtu sahihi kuwa mkuu wa electrical engineers wetu huko tanesco? Yaani ni kama pale Jakaya Kikwete Heart Institute tupeleke mtu wa MBA akasimamie upasuaji wa mioyo ya watu halafu utegemee watapona!
 
Je hadi sasa hiko kitu kizuri cha maharage ya chande umeshakipata kutoka kwa huyu aliyekuwa MD wa DSTv Tanzania? Graduate wa Master of Buisiness Administration from the University of South Africa ambaye hana utalaam wo wote wa umeme lakini sisi tukaona ndiye mtu sahihi kuwa mkuu wa electrical engineers wetu huko tanesco? Yaani ni kama pale Jakaya Kikwete Heart Institute tupeleke mtu wa MBA akasimamie upasuaji wa mioyo ya watu halafu utegemee watapona!
Nimeanza kumtilia shaka, huenda kuna malengo mengine
 
Nimeanza kumtilia shaka, huenda kuna malengo mengine
Hafai kabisa huko tanesco. Huko siyo fani yake. Arudi huko DSTV au Vodacom au kule NBC inayomilikiwa na kampuni ya Afrika kusini. Mkurugenzi Mkuu wa tanesco anapaswa kuwa ni mhandisi mbobevu kwenye masuala ya umeme.
 
Mkurugenzi Mkuu wa tanesco anapaswa kuwa ni mhandisi mbobevu kwenye masuala ya umeme.
Uhandisi umeme na kuwa manager havina uhusiano. Dr Idris Rashid alikuwa meneja wa benki na alipopewa tanesco aliendesha shirika kwa mafanikio makubwa.

Hao wahandisi wabobevu wanatakiwa kuwa wakurugenzi wa vitengo ili ujuzi wao uweze kutumika ipasavyo. Umeneja lazima awe amesomea
 
Uhandisi umeme na kuwa manager havina uhusiano. Dr Idris Rashid alikuwa meneja wa benki na alipopewa tanesco aliendesha shirika kwa mafanikio makubwa.

Hao wahandisi wabobevu wanatakiwa kuwa wakurugenzi wa vitengo ili ujuzi wao uweze kutumika ipasavyo. Umeneja lazima awe amesomea
Haya jaribu kupeleka meneja wa benki au wa Vodacom kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili National Hospital halafu uje utusimulie muziki wake tutakaoupata. Au mtu wa aina hiyo mpeleke akawe kiongozi mkuu wa mahakama zetu. Taasisi za kitaaluma huongozwa na wenye taaluma husika. Hao wenye MBA au Public Administration ndiyo wanapaswa kuwa wakurugenzi wa vitengo kwenye hizo professional institutions. Na unapaswa kujua kuwa hao professionals pia hufundishwa management na wengine wana post graduate degrees or diplomas za MBA, MPH, Law etc. Hiyo ndiyo maana ya profession.

Huyo Dr Idris Rashid, meneja wa benki alipopelekwa tanesco alienda kuiuza tanesco kwa kampuni ya Afrika kusini. Hawa watu are just business oriented. Tanesco si taasisi ya kibiashara bali ni taasisi ya huduma kwa wananchi kama ilivyo taasisi za afya, maji, barabara, reli na mahakama. Umeme ni huduma nyeti kwa usalaama wa nchi. Tunashuhudia Urusi inavyoisambaratisha Ukraine kwa kuvunja vunja miundo mbinu yake ya umeme, maji na madaraja ya barabara. Maharage Chande naye yuko kwenye harakati ya kubinafisha baadhi ya maeneo ya tanesco. Tumeshuhudia jinsi ambavyo hatuna control ya bei ya gesi yetu kwa sababu yakuimilikisha kwa wawekezaji wa nje kupitia mikataba kama hii anayoongelea Maharage Chande.
 
Huyo Dr Idris Rashid, meneja wa benki alipopelekwa tanesco alienda kuiuza tanesco kwa kampuni ya Afrika kusini. H
Una uhakika na unayoyasema? Kuuzwa kwa tanesco kwa Afrika Kusini ilikuwa enzi ya Mkapa.
 
Una uhakika na unayoyasema? Kuuzwa kwa tanesco kwa Afrika Kusini ilikuwa enzi ya Mkapa.
Nadhani uko sahihi. Baada ya serikali kuitimua hiyo kampuni ya NET group solutions ya Afrika kusini ndipo Dr Idris Rashid aliteuliwa kuwa kiongozi (MD) wa tanesco kutoka kuwa gavana wa benki kuu, kipindi cha awamu ya nne ya Kikwete.

Huyu Dr Idris Rashid ndiye aliyetafuta makampuni ya kigeni kuleta mitambo yake ya kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta kwa gharama ya kufilisi nchi. Ndiye mwanzilishi (founder) wa mitambo ya umeme wa mabeberu pale Ubungo maziwa na mitambo ya Dowans na IPTL. Ndiye ambaye katika kipindi chake walikuwa wanafungulia maji ya bwawa la Kidatu na Mtera ili nchi inunue umeme wa mafuta wa mabeberu hawa. Ndiye mwanzilishi wa capacity charges za makampuni haya. Hata kama hayazalishi umeme tulilazimika kuyalipa mabilioni ya pesa kila siku. Tukitaka yazalishe umeme tulipaswa kuyawekea mafuta kwa gharama zetu etc. Yaani ilikuwa ufisadi wa hali ambayo haijawahi kutokea hapa duniani.

Huyu ndiye aliyeleta sakata la Richmond lilomung'oa Waziri mkuu (Lowasa) na waziri wake wa nishati (Dr Msabaha). August 2009, mbunge Richard Ndasa alilalamika bungeni jinsi mkurugenzi huyu alivyojiuzia nyumba ya serikali Namba 13 iliyoko Osterbay kwa shillingi million 60 baada ya tanesco kuikarabati kwa shilingi million 600.

 
Huyu hapa:

MAHARAGE CHANDE ni nani:
Akiwa katika nafasi ya kuaminiwa ya kiuongozi ,ni mbobezi katika kuleta mabadiliko chanya na kuleta mguso anapojiunga na kampuni yoyote.

Kiongozi yoyote anapojiunga katika kampuni mpya kazi yake kubwa ni kubadilisha muelekeo wa taasisi au kampuni kufanya vizuri zaidi na kuingiza tamaduni mpya wa jinsi ya utendaji kazi kwa wafanyakazi waliopo na pia wateja wao kunufaika na ujio wa uongozi Mpya kwa kupokea huduma bora, ya bei nafuu pia waliowekeza hisa kuona ktk kampuni kuona hisa zao zikiongezeka thamani na mwisho wa mwaka wa pesa kupata gawio jingi zaidi ya miaka iliyopita.


Maharage Chande – Regional Director for East Africa/ Regional Director for West Africa

Career path since 2010:
Maharage Chande, is MultiChoice Regional Director for East and in an acting capacity for West Region. At the same time, Maharage will continue to look after Tanzania.
According to de Villiers: “Maharage joined MultiChoice Tanzania in June 2016 as MD and has been hugely successful in driving the massive growth that business has experienced”. On his side, Maharage said he has received the appointment wholeheartedly and that without doubt it is the results of a people-focused leadership and meticulous execution of set strategic initiatives by all MultiChoice Tanzania staff members. “I believe that I can use the Tanzanian success story to further enhance our business growth in the regions,” he added.
Before joining MultiChoice Tanzania in 2016, Maharage who has extensively worked in Banking and Telecoms industries, worked at Vodacom Tanzania as Managing Executive of IT and Data from 2004 to 2010, National Bank of Commerce (NBC) as Chief Operating Officer from 2010 to 2014 then moved to the President’s Office as the Director of Corporate Services in the President’s Delivery Bureau from 2014 to 2016.
“We are excited to welcome the senior executives on board. It is our hope that their wealth of experience will complement MultiChoice Africa’s current focus on customer satisfaction and market growth,” concludes de Villiers. Source : Maharage Chande to head Multichoice in East, West Africa as Stephen Isaboke takes up new role | aptantech

Toka maktaba 2017

Maharage Chande aonesha mbinu za kibiashara ndani ya changamoto nyingi. Changamoto ni fursa!


Tutegemee "vifurishi rafiki vya umeme na vyuma kuachia" kama ilivyokuwa Multi Choice DStv





Toka maktaba 2017

Mbinu Mpya ya Kuwa Na Wateja Marafiki-Endelevu ya DStv Multi Choice

‘Vyuma vimeachia’. alieleza Maharage Chande.

Maharage Chande amesisitiza kuwa Multichoice itaendelea kuwasikiliza wateja wake na kuhakikisha kuwa inatekeleza kile wanachohitaji wateja wake pale inapowezekana. “Wateja wetu walituomba tuongeze maudhui ya kitanzania kwenye king’amuzi chetu, tukawasikia, tukaweka chanel maalum kabisa ya Maisha Magic Bongo ambayo ina asilimia 100 ya maudhui ya Kitanzania; wakatuomba tupunguze bei ya vifurushi, tukafanya hivyo mwishoni mwa mwaka jana, na leo tena kwa mara ya pili tumepunguza bei, wakatuomba tuongeze chanel kwenye vifurushi vya bei ndogo, tukafanya hivyo, tukaleta Laliga na Ligi kuu ya uingereza hadi kwenye kifurushi cha chini kabisa cha Bomba”. “Kipekee kabisa Wananchi kupitia serikali wakatuomba tuongeze nguvu kwenye kuinua vipaji vya vijana wetu wa kitanzania, tukasikia, tukaitikia, tukaanza katika riadha ambapo tumemdhamini mwanariadha wetu Alphonce Simbu. Sote tunajua matokeo yake, sasa Tanzania inahofiwa kwenye ulingo wa riadha kimataifa! Haya yote tumefanya kwa sababu tunawasikiliza wateja wetu, tunawasikiliza wadau wetu, tunawasikiliza Watanzania” alisema Maharage.

Kiko wapi!!!? Je umeme ulikuwa vipi?
 
Back
Top Bottom