Mahanga: Fukuzeni Waitara Ukonga

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Ilala, Dk Makongoro Mahanga amewataka wananchi wa jimbo la Ukonga kumfukuza mgombea wa CCM, Mwita Waitara.

Amesema Waitara anapaswa kutimuliwa na wananchi hao kila watakapomuona kwa kuwa walimchagua katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kabla ya kumalizia kipindi chake cha ubunge cha miaka mitano, amewakimbia.

Waitara alikuwa mbunge wa Chadema katika jimbo hilo tangu 2015 lakini Julai 28, 2018 alijiuzulu na kujiunga na CCM ambako amepitishwa kuwania tena ubunge.

Mahanga ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 30, 2018 katika mkutano wa kampeni wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Gulu Salala Gongo la Mboto.

Dk Mahanga ambaye alikuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne, amesema makosa yamefanywa na Waitara lakini wanaotukanwa ni wananchi waliompiga kura.

“Mnaonekana mandondocha na yeye anawafanya mandondocha kwa kumpigia kura. Msikubari cheo hicho nyinyi mna akili timamu fanyeni maamuzi kwenye sanduku la kura,” amesema.

Mahanga amesema kinachofanyika sasa na CCM ni kukusanya shahada za kura kwa wananchi kwa kutumia mabalozi.

"Juzi nililisema wakati nikiwa CCM tulikuwa tunatumia mabalozi kuiba kura na kununua shahada kwa wananchi, wamekasirika wanatamani kupasuka,” amesema.

"Nasisitiza huo ndio ukweli, wakija majumbani mwenu wafukuzeni na kingine cha kuwafanya mnakijua.”

Amedai kuwa kwa sasa CCM ni kama imekufa kwa maelezo kuwa inategemea zaidi Jeshi la Polisi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), vinginevyo hawawezi kufanya lolote.

Diwani Kata ya Kipawa, Kenedy Simon amesema, “ndugu yetu Waitara aliyeondoka ana shida. Amekosa fikra yakinifu kwa sababu hata nyumba anayoishi imejengwa na Chadema.”

Amebainisha kuwa Waitara alinunuliwa hadi pikipiki lakini ameona hayo yote ni bure na kuamua kutimkia CCM kwa kuwasaliti wapigakura.

"Achaneni na Waitara kwa sababu anawafanya mtaji wananchi wa Ukonga. Alipokuwa Chadema mmempa Ubunge anahamia CCM anataka mumpe tena,” amesema Saimon.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahahah Makongoro anatukumbusha jinsi alivyoiba boksi la kura na kukamatwa nazo kule buguruni..mwizi mkubwa yule..
 
Eti Waitara alinunuliwa pikipiki hana shukurani.jamani Waitara sio saizi ya pikipiki wewe diwani Tunga Uongo mwingine ni sawa Na kusema alinunuliwa baiskeli hana shukurani!!!!!!
Hujaona la nyumba umeliona la pikipiki tu?
 
Ubunge sio uwakilishi tena ni kama Government instrumental! Wananchi wamedharaulika mno japo ni haki mbunge kuhama chama,ila kuhama na bado anakuja kuomba nafasi Ile ille!.inasikitisha sana ndani ya five years! Kura haina thamani.
 
Mahanga pamoja na wewe uliyekubali kuiba enzi hizo kwa manufaa yako na hao unaowasema inafaa ufukuzwe kabisa wewe muanzilishi hapo ukonga wa dhuluma za wananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
safi sana !

Anachoongea Makongoro Mahanga ni ukweli mtupu.
Waitara hatakiwi kurudi Bungeni tena kwa kura za watu walewale waliompigia kura 2015 na leo amewasaliti.......kitendo cha kumrudisha Bungeni hakika ni undondocha wa kiwango cha lami...!!
NO VOTE FOR MRISYA WAITARA.....mwambieni arudi kijijini akare kichuri....nyambaf>
 
Sikumbuki kama kauli hii aliitoa kwa wananchi wa Singida Kaskazini baada ya aliyekuwa mbunge wao Nyarandu kuhama CCM!
Hayo utajua wewe , kwani Mh Nyalandu alipoondoka ccm uliona tena akipeleka pua kuomba ubunge ?
 
Back
Top Bottom