MAHAKIMU wagonga mwamba

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,105
17,104
Harakati za Mahakimu wa Mahakama mbalimbali Tanzania kuapishwa kuwa Mawakili zimegonga mwamba. Taarifa toka Mahakama ya Rufani Tanzania zinasema kuwa Jaji Mkuu Othman Chande amewakatalia mahakimu wote kuapishwa kuwa Mawakili hapo tar 7 ya mwezi huu wa Disemba. Mahakimu hao wametakiwa kuacha kazi ili waapishwe. Je,ni halali?
 
ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,130
919
Dhana ya kuwazuia mawakili wa Serikali au Mahakimu kutoapishwa kwa kile kinachodaiwa ni mgongano wa maslahi ni ubinafis na upuuuzi mtupu wa watendaji wetu wakuu (Mwanasheria Mkuu na Jaji Mkuu). Hakuna Sheria yeyote inayowazuia kuapishwa. Wala pia hakuna Sheria au waraka unaozuia Mtu akiwa wakili (aliyeapishwa kuwa wakili wa kujitegemea - Advocate) kutoomba kazi za uwakili wa Serikali au Uhakimu. Mbona Majaji wengi walioteuliwa kwenye Bench wanatokana na Mawakili binfasi na mgongano wa maslahi hautajwi??. Sasa imekuwa vutugu tupu kwani wapo vijana kibao wanaomaliza shule ya Sheria (LAW SCHOOL ) wanaapishwa kuwa mawakili na baadae kuajiriwa kama Mawakili (STATE ATTORNEYS) au Mahakimu (MAGISTRATES) . Hawa vijana waliobahatika kupitia LAW SCHOOL wanawapiku kaka na dada zao waliowatangulia ambao waliamua kufanya kazi ya Uwakili wa Serikali au Uhakimu na kujikuta wakizuiwa kuapishwa kwa hila tu za mtu binafsi.

Sasa huyo Jaji Mkuu haoni kama hawatendei haki baadhi ya Mahakimu walioanza pasipo kuapishwa?? au aoni kuwa anatengeneza matabaka miongoni mwa mahakimu (wale ambao tayari ni Mawakili na wale ambao sio Mawakili)??...Kwa nini majaji watokane na mawakili kama dhana ni kuwa ukiwa wakili basi hupaswi kuwa Hakimu??. Nimeambiwa kule kwa Mwanasheria Mkuu, Mawakili wa Serikali wameruhusiwa kuapishwa lakini hawapewi vyeti (practising certificates ) Hii itasaidia kuwatambua kwa maana ya Seneority kwenye Uwakili.

Wakati wenzetu wa Kenya na Waganda wanapigania kuaongeza idadi ya Mawakili, sisi tunatengeneza sera mbovu za kuwazuia wasiongezeke.
 
Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,442
2,467
dhana ya CJ ni kuacha kazi kwanza kwa hakimu ndio aweze kuapishwa
huwezi kuapishwa kuwa private advocate wakati wewe ni hakimu
CJ yuko sawa.
suala la kimgongano wa maslahi litakuwepo
imagine hakimu kapewa kesi ambayo firm yake ndio inasimamia lazima atoe upendeleo ili mteja wao ashinde
Magistrate Act na Advocate Ordinance nadhani ziko clear kuhusu hili
who may serve as advocate of the High court save for primary courts.
haiwezi kutokea hakimu awe wakili akiwa kazini
au jaji akubaliwe kuwa wakili wa kujitegemea akiwa kazini.
 
mhondo

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
968
332
dhana ya CJ ni kuacha kazi kwanza kwa hakimu ndio aweze kuapishwa
huwezi kuapishwa kuwa private advocate wakati wewe ni hakimu
CJ yuko sawa.
suala la kimgongano wa maslahi litakuwepo
imagine hakimu kapewa kesi ambayo firm yake ndio inasimamia lazima atoe upendeleo ili mteja wao ashinde
Mgaistrate Act na Advocate Ordinance nadhani ziko clear kuhusu hili
who may serve as advocate of the High court save for primary courts.

Wawe wanaomba kujitoa kwenye kesi zenye maslahi nazo na kama hawafanyi hivyo na ikabainika wawe wanapewa adhabu kali.
 
Kijana, kwani akina Jaji Zainabu Muruke, Twaib, Mujulizi, Masati, Jundu, Nyangarika, Sheikh et al sio Mawakili wa Kujitegemea?? Hawa ameteuliwa wakiwa mawakili wa kujitegemea toka Private Law firms na hawakuambiwa wajivue uwakili kwanza ila kwa sasa hawapewi tu vyeti.

Suala la Mgongano wa maslahi haliepukiki. Ni maadili ya mtu tu
 
Mwanasazi

JF-Expert Member
Aug 5, 2012
237
54

Hapo issue ni ku practice sio kusajiliwa uwakili, ndio maana unaona certificate of practice inatolewa kila mwaka kwa iyo unaweza kuwa wakili lakini hauruhusiwi kupractise, kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo hiyo kuteuliwa kuwa judge, wakili wa serikali, hakimu, unethical issue, kutolipia ada.
Kwa iyo all in all CJ yuko sawa, na hata hao majaji hawawezi ku practice.
 
Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,975
8,274
Tulio wakulima wa nyanya huku Itabagumba tunasoma comment za watu alafu tunachanganya na zetu ila kama CJ yupo sahihi vile kwa michango niliyoona japo CJ kwa kirefu zijui maana kithungu nacho kwa sie wakulima ni issue nzito
 
Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,518
1,336
Kuonesha ukomavu wao wa kisheria ni kheri wamfungulie kesi ya kikatiba jaji mkuu, wasiogope, it's an open and close case, watashinda tu.

MisIngi ya kesi:
Haki ya kufanya kazi
Haki ya kusikilizwa
Maamuzi ya kibaguzi
 
Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,442
2,467
toafutisha kati ya wakili wa kujitegemea kuwa jaji
na hakimu kuwa wakili wa kujitegemea akiwa kazini
akishakuwa jaji haruhusiwi kuendesha kesi zitokazo kwenye firm yake na haruhusiwi kupractice kama wakili,
haijawahi na haitokaa itokee hakimu awe wakili bila kuacha kazi
au jaji akubaliwe kuwa wakili wa kujitegemea akiwa kazini
Kijana, kwani akina Jaji Zainabu Muruke, Twaib, Mujulizi, Masati, Jundu, Nyangarika, Sheikh et al sio Mawakili wa Kujitegemea?? Hawa ameteuliwa wakiwa mawakili wa kujitegemea toka Private Law firms na hawakuambiwa wajivue uwakili kwanza ila kwa sasa hawapewi tu vyeti.

Suala la Mgongano wa maslahi haliepukiki. Ni maadili ya mtu tu
 
assuredly4

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
1,216
217
Dhana ya kuwazuia mawakili wa Serikali au Mahakimu kutoapishwa kwa kile kinachodaiwa ni mgongano wa maslahi ni ubinafis na upuuuzi mtupu wa watendaji wetu wakuu (Mwanasheria Mkuu na Jaji Mkuu). Hakuna Sheria yeyote inayowazuia kuapishwa. Wala pia hakuna Sheria au waraka unaozuia Mtu akiwa wakili (aliyeapishwa kuwa wakili wa kujitegemea - Advocate) kutoomba kazi za uwakili wa Serikali au Uhakimu. Mbona Majaji wengi walioteuliwa kwenye Bench wanatokana na Mawakili binfasi na mgongano wa maslahi hautajwi??. Sasa imekuwa vutugu tupu kwani wapo vijana kibao wanaomaliza shule ya Sheria (LAW SCHOOL ) wanaapishwa kuwa mawakili na baadae kuajiriwa kama Mawakili (STATE ATTORNEYS) au Mahakimu (MAGISTRATES) . Hawa vijana waliobahatika kupitia LAW SCHOOL wanawapiku kaka na dada zao waliowatangulia ambao waliamua kufanya kazi ya Uwakili wa Serikali au Uhakimu na kujikuta wakizuiwa kuapishwa kwa hila tu za mtu binafsi.

Sasa huyo Jaji Mkuu haoni kama hawatendei haki baadhi ya Mahakimu walioanza pasipo kuapishwa?? au aoni kuwa anatengeneza matabaka miongoni mwa mahakimu (wale ambao tayari ni Mawakili na wale ambao sio Mawakili)??...Kwa nini majaji watokane na mawakili kama dhana ni kuwa ukiwa wakili basi hupaswi kuwa Hakimu??. Nimeambiwa kule kwa Mwanasheria Mkuu, Mawakili wa Serikali wameruhusiwa kuapishwa lakini hawapewi vyeti (practising certificates ) Hii itasaidia kuwatambua kwa maana ya Seneority kwenye Uwakili.

Wakati wenzetu wa Kenya na Waganda wanapigania kuaongeza idadi ya Mawakili, sisi tunatengeneza sera mbovu za kuwazuia wasiongezeke.

nina shaka wewe unafanya kazi kwa mwanasheria mkuu wa serikali, kama ndivyo dhambi mliyoiasisi ya kutowatambua wanasheria wengine walioko nje ya ajira ya AG na kutowahesabu mawakili na ksiha mkaenda mbali na kujilipa mishahra kwa scale yenu ndiyo inayowatafuna. mbona hampiganii wanasheria wote muwe na mishahara sawa na wote muwe na power of litigation. hii ndiyo wenzenu waliyotumia kuwapiga bao na lkusajiliwa kama mawakili.

usipige kelele kubali matokeo ya dhambi ya ofisi yako mliyoipigia makofi na kuikumbatia
 
Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,645
4,482
Wawe wanaomba kujitoa kwenye kesi zenye maslahi nazo na kama hawafanyi hivyo na ikabainika wawe wanapewa adhabu kali.

kwa nini mtake kuvaa kofia mbili kwa wakati mmoja? Lengo ni nini? Hizo adhabu kali tz haiwezekani! Mtakuwa mnavujisha siri nyingi kwa maslahi yenu ya chini kwa chini. Jamani kumbukeni hizi ni kazi mbili zenye mgongano wa maslahi. Acheni kazi moja basi.
 
Jajani

Senior Member
Oct 13, 2012
137
16
Tulio wakulima wa nyanya huku Itabagumba tunasoma comment za watu alafu tunachanganya na zetu ila kama CJ yupo sahihi vile kwa michango niliyoona japo CJ kwa kirefu zijui maana kithungu nacho kwa sie wakulima ni issue nzito

CJ yupo sahihi tatizo ni la mazoea tu.
Watanzania wengi ni waroho, wanapenda wafanye kazi nyingi na hata ikiwezeka apewe zote mtu mmoja.
Eg utasikia ni mjumbe wa bodi ya wakurugenz, meneja, mkurugenzi, advoketi, mwenyekiti nk. Na kote huko hupata mipesa na kuzuia wengine wasipate.
Uroho na ubinafsi tu.
 
Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,975
8,274
toafutisha kati ya wakili wa kujitegemea kuwa jaji
na hakimu kuwa wakili wa kujitegemea akiwa kazini
akishakuwa jaji haruhusiwi kuendesha kesi zitokazo kwenye firm yake na haruhusiwi kupractice kama wakili,
haijawahi na haitokaa itokee hakimu awe wakili bila kuacha kazi
au jaji akubaliwe kuwa wakili wa kujitegemea akiwa kazini[/QUOTE]

Kuna logic hapa kiaina kwa sie maamuma wa sheria
 
nlambaa

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
361
55
kwa upande wangu naona watumishi wa serikali kama mahakimu na mawakili wa serikali wanaweza kuapishwa ila wasipewe practising certificate, kwa kuapishwa atalinda seniority yake kwani inatia uchungu kwa mfano mtu aliyemaliza 1990, na kufanya mtihani na kupasi mwaka 1993 anakuwa junior kwa mtu aliye maliza mwaka 2012 eti tu kwa sababu hajaapishwa kama wakili wa kujitegemea kutokana na majukumu yake ya uwakili wa serikali au uhakimu
 
Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,442
2,467
mkuu Jadoki, CJ ni Chief Justice ndio jaji mkuu wetu.
Nlambaa kuapishwa halafu usipractice haina maana kisheria
kuapishwa manake ni kuapa kufanya kazi uliopewa.
sasa mahakimu wataapaje kisha wapewe certificate ya kuwa private advocate afu asifanye kazi husika?
msimamo ya CJ ni wa kisheria,
kama wamechoka na maslahi madogo ya judiciary, na kama wanaona hawawezi waache kazi wataapishwa
 
mpalu

JF-Expert Member
Sep 15, 2010
2,520
868
Harakati za Mahakimu wa Mahakama mbalimbali Tanzania kuapishwa kuwa Mawakili zimegonga mwamba. Taarifa toka Mahakama ya Rufani Tanzania zinasema kuwa Jaji Mkuu Othman Chande amewakatalia mahakimu wote kuapishwa kuwa Mawakili hapo tar 7 ya mwezi huu wa Disemba. Mahakimu hao wametakiwa kuacha kazi ili waapishwe. Je,ni halali?
ni halali
 
WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,459
943
Harakati za Mahakimu wa Mahakama mbalimbali Tanzania kuapishwa kuwa Mawakili zimegonga mwamba. Taarifa toka Mahakama ya Rufani Tanzania zinasema kuwa Jaji Mkuu Othman Chande amewakatalia mahakimu wote kuapishwa kuwa Mawakili hapo tar 7 ya mwezi huu wa Disemba. Mahakimu hao wametakiwa kuacha kazi ili waapishwe. Je,ni halali?
Ni halali kabisa.
Utaratibu ndio huo - Ikiwa umeajiriwa Jaji Mkuu anaweza kukuapisha tu ikiwa utapata barua ya kukuombea kwake kutoka kwa mwajiri wako.
Mahakimu watapewa barua na mwajiri yupi ikiwa wao wako Judiciary?
Hilo linawakumba wengi walio kwenye ajira na siyo wao tu.
Wakiona wanautaka sana uwakili waache kazi.Vinginevyo tunarudi kule kuleee-- wanakuwa silent partners kwenye chambers kisha wanahukumu na kujipendelea kwenye kesi zilizoshikiliwa na partners wao.
 
KIBE

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
943
184
dhana ya cj ni kuacha kazi kwanza kwa hakimu ndio aweze kuapishwa
huwezi kuapishwa kuwa private advocate wakati wewe ni hakimu
cj yuko sawa.
Suala la kimgongano wa maslahi litakuwepo
imagine hakimu kapewa kesi ambayo firm yake ndio inasimamia lazima atoe upendeleo ili mteja wao ashinde
magistrate act na advocate ordinance nadhani ziko clear kuhusu hili
who may serve as advocate of the high court save for primary courts.
Haiwezi kutokea hakimu awe jaji akiwa kazini
au jaji akubaliwe kuwa wakili wa kujitegemea akiwa kazini.

bora uwaambie labda wataelewa mana tumekuwa sasa na taifa hasa vijana wenye mtazamo wa kulalamika kulamamika wakati ukweli uko wazi ...kwani si umeambiwa kama unataka uache kazi kwani tatizo lako wapi????? Acha nenda kawe wakili wa kijitegemea.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom