Kama kuna sehemu imeathiriwa kwa kiwango cha kutisha na ushirikina basi ni mahakama zetu, kumefukiwa madude kule si mchezo
Vifo vingi vya mahakimu wazee wa baraza na watumishi wa mahakama vingi vimejaa utata na vina mahusiano ya moja kwa moja na eneo lao la kazi na kesi wanazozisimamia
Pamoja na watu kufanya makosa mbali mbali kwenye jamii lakini hawako tayari kuukubali mkono wa sheria pale inapotokea wakakamatwa na ndio matatizo huanzia hapo
Watu wanabeba madubwana yao na kwenda kuyafukia pale wengine wanabeba na kuingia nayo kwenye vyumba vya mahakama na kwenda kuwadhuru wasiohusika
Ingekuwa serikali yetu inatambua uwepo wa uchawi ingeweka sheria ya kukagua watu kabla session za mahakama hazijaanza na kwenye vyumba vya mahakama kwakuwa wanaumizwa hata wasiohusika
Mi ni miongoni mwa wenye imani haba ya uchawi. Sina uhakika na utafiti wako wa uchawi mahakamani. Vifo ni kawaida. Tufikirie mazingira ya watumishi wa mahakama zetu. Uadirifu ni mdogo hivo wana ishi kwa hofu. Wanapata ziada hivo kula haina shida. Nenda migahawa eneo la mahakama kajionee. Mwisho hawana mazoezi licha ya kazi zao muda mwingi wamekaa, na ulaji wao na unywaji usio na mgogoro. Hata hivo haya ni maoni binafsi.
Sema wewe unaamini uchawi na sio kila mtu.Ogopa sana mtu anaekwambia haamini katika uchawi. wengi ni wanga waliokubuhu
ogopa sana anaejifanya mwema sana na mtakatifu
vijana nao siku izi tumekuwa wanga hatari. kama imani yako ya kuunga unga lazima uisome namba .
Mdau...!!!
Sema wewe unaamini uchawi na sio kila mtu.
Mimi siamini uchawi wala shetani wala mungu, hivyo vitu havipo.
Sema wewe unaamini uchawi na sio kila mtu.
Mimi siamini uchawi wala shetani wala mungu, hivyo vitu havipo.