Mahakama yamsafisha mke wa Chiluba.....................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,574
2,000
Mahakama yamsafisha mke wa Chiluba

Wednesday, 08 December 2010 18:52 newsroom
LUSAKA, Zambia
MAHAKAMA ya Zambia imemsafisha mke wa Rais mstaafu Frederick Chuliba, Regina, dhidi ya tuhuma za rushwa.
Regina aliolewa na Chiluba baada ya kiongozi huyo kuondoka madarakani mwaka 2001. Majaji wa Mahakama Kuu ya Zambia walisema serikali imeshindwa kuthibitisha kuwa Regina alipata fedha za umma kinyemela wakati mumewe akiwa madarakani.

Mwaka jana, Regina alipatikana na hatia ya kupokea pauni za Uingereza 200,000 ikiwa ni vifaa na fedha taslimu na kuhukumiwa na mahakama ya chini kifungo cha miaka mitatu na miezi sita. Mumewe alisema hukumu dhidi ya mkewe ilikuwa sehemu ya ‘kuwindana’ kunakoongozwa na watu wanaompinga. Agosti mwaka huu, Mahakama ya Zambia ilikataa kutekeleza hukumu iliyotolewa na majaji wa Uingereza ambao waliagiza Chiluba arudishe pauni milioni 46 alizotuhumiwa kuzipata akiwa madarakani. Taasisiya kuzuiana na kupambana na rushwa na wadau wengine wamepinga uamuzi huo wa mahakama wa kumfutia adhabu mke huyo wa Chiluba.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom