Mahakama yakana kuandika Barua kuzuia mjadala wa Tegeta Escrow Account bungeni

Wakati Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakichachamaa wakisema hawatakubali Bunge hilo kuingiliwa na mhimili wa Mahakama, Mahakama hiyo imejiweka kando na tuhuma hizo.

Msajili wa Mahakama Kuu, Amir Msumi, alipotakiwa jana na NIPASHE kuthibitisha kama Mahakama imeandika barua hiyo kwenda Ofisi ya Spika wa Bunge kuzuia suala hilo lisijadiliwe kwa kuwa kiko mahakamani, alisema yeye na wasajili wenzake hawana taarifa kuhusu kuandikwa kwa barua hiyo.

Labda unieleze hiyo barua imeandikwa na nani na lini, kama ni Jaji au Msajili nitajie jina lake ili iwe rahisi kufuatilia, lakini hadi sasa nimepekua kwenye kumbukumbu zetu sijaona barua hiyo,” alisema Msumi.

Aliahidi kwamba jana angewasiliana na wenzake wa Mahakma ya Rufani kama kuna barua imeandikwa kutoka mahakama hiyo kwenda bungeni.

Nipashe
 
Nimependa sana upinzani umekuwa pro-acitve na sio reactive. Wanapata taarifa kabla hata lengo halijatekelzwa. safi sana. Wangesubiri barua ikafika ingeweza kuwa ngumu kuzuia. Serikli walijaribu kupima kina cha maji na walipoona ni kirefu wamepotezea.
 
Akina Mbatia walitaka kujichukulia umaarufu kwenye jambo hili. Hongera Mahakama kwa kuweka wazi

We mwanamke huwa unatia kinyaa hata kwenye mambo ya msingi unaongea utumbo........ Jirekebishe ndugu yangu khaaaa
 
tunataka barua hakuna cha kusema kama ipo,wasingeenda kwenye vyombo vya habari kutangaza,tunataka kujua nani muongo,waliosema kuna barua toka mahakamani na wanaokana hamna barua kutoka mahakamani. lisiwe bunge la kisanii. TRURH WILL ALWAYS PREVAIL
“Hakuna huo utaratibu wa
kukufundisha wewe kuongoza Bunge, hivyo kama kuna barua
imetoka mahakamani
kwa jaji fulani naomba iwekwe mezani ili
tumjadili huyo jaji, kama barua hiyo haipo basi tuendelee
na shughuli zetu
,” alisema Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu
wa Kambi ya Upinzani.
 
tunataka barua hakuna cha kusema kama ipo,wasingeenda kwenye vyombo vya habari kutangaza,tunataka kujua nani muongo,waliosema kuna barua toka mahakamani na wanaokana hamna barua kutoka mahakamani. lisiwe bunge la kisanii. TRURH WILL ALWAYS PREVAIL
“Hakuna huo utaratibu wa
kukufundisha wewe kuongoza Bunge, hivyo kama kuna barua
imetoka mahakamani
kwa jaji fulani naomba iwekwe mezani ili
tumjadili huyo jaji, kama barua hiyo haipo basi tuendelee
na shughuli zetu
,” alisema Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu
wa Kambi ya Upinzani.
 
Wabunge wa upinzani walikuwa wazua kuwa kuna barua kutoka mahakamani iliyozuwia mjadala wa Escrow bungeni.

Mwenyekiti wa Bunge Mheshimiwa Azzan Zungu, amethibitisha sasa hivi bungeni kuwa hakuna barua kutoka mahakamani iliyozuwia mjadala huo au mwingine wowote ule bungeni na mjadala utakuwepo kama ilivyopangwa awali.

Hapo sasa!
 
We tulua watamkana mpaka boss wao prof wa kichina
Wamekanusha tena kuwa Shyrose hakupigana kule Kenya, lakini hawakueleza kwanini alilala lumande. Ni mwendo wa kukanusha tu. Bado kidogo watasema kuwa singasinga Harbinder hahusiki IPTL.
 
Real ila kuna kitu hapa kinaleta uwezo mwingine wa kufikiri nimesoma gazeti la majira hebu pitieni wadau
 
WAMESHAONA HAIWEZEKANI IMEBIDI WAKUBALI YAISHE UNADHANI NIKWELI KWAMBA HAUKUKUA NA HIYO BARUA?KAMA ULIMSKILIZA PINDA JANA UTAFAHAMU KUNA MCHEZO ULIKUA UCHEZWE. Mwenye VIDEO YA BUNGE LA JANA AU LINK TAFADHALI JAMANI MUITUPE HIYO LINK KUNA WENGINE TULIKUA MAOFISINI.
 
wabunge wa upinzani wapuuzi wao kazi yao ni kuzusha uongo usiokuwa na maana acheni yapuyange yamezoea kupuyanga kwa uongo.

ivi si ndio hawa walianzisha hili jambo mkawatukana na kidogo mpigane mbona yamekuwa haya tena
 
Back
Top Bottom