Mahakama yafuta hati ya kumkamata Chenge

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Kinondoni imefuta hati yake ya kuruhusu kukamatwa kwa mwanasheria mkuu wa zamani, Andrew Chenge iliyotolewa juzi kutokana na mshtakiwa huyo kushindwa kutokea mahakamani.

Hakimu Sundi Fimbo alitoa hati hiyo juzi wakati Chenge, ambaye anatetea kiti chake cha ubunge wa Jimbo la Bariadi Mashariki akiwa kwenye mkutano wa kampeni ambako alipigiwa debe na mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete ambaye kwa sasa yuko mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Lakini mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, David Mwafwimbo aliiambia Mwananchi jana kuwa mdhamini wa Chenge aliibuka juzi akiwa amechelewa na akamuomba hakimu afute hati hiyo na ombi lake likakubaliwa.

"Mdhamini wake anayeitwa Masanja alimrudisha Hakimu Fimbo mahakamani ili kuomba kufutwa kwa kibali cha kumkamata mshtakiwa... ingawa mdhamini huyo alifika mahakamani hapo akiwa amechelewa, alienda kumuomba hakimu afute hati hiyo na akakubaliwa" alisema Mwafwimbo.

Mwafwimbo alisema baada ya mdhamini huyo kufika, hakimu aliitisha tena jalada hilo na kuifuta amri hiyo ya kukamatwa kwa mshtakiwa huyo.

Chenge alitakiwa kuanza kujitetea jana katika kesi inayomkabili ya kuendesha gari kizembe na kufanya makosa mawili ya kusababisha vifo vya watu wawili na jingine la kuendesha gari bila bima halali.

Chenge anadaiwa kugonga pikipiki ya maguruduma matatu, maarufu kama Bajaj iliyowabeba wasichana wawili na kusababisha vifo vyao ambavyo kisheria huchukuliwa kama makosa mawili tofauti.

Kutokuwepo kwake kulimfanya Hakimu Fimbo kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 5.

Lakini Zulfa Mfinanga na Herman Meza wanaripoti kutoka Shinyanga kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo lilikuwa halijapokea hati ya kumkamata.

Afisa upelelezi mkoani humo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi((SSP), Adam Nyakipande alikiri kusikia habari hiyo, lakini akasema walishindwa kuitekeleza kwa kuwa hawakupata kibali cha mahakama hiyo.

"Ninachoweza kusema ni kwamba sisi tunasubiri hati ya kumtia nguvuni... kwa ufupi bado hatujapewa kibali cha kumkamata lakini tukipata tutalifanyia kazi," alisema.

Chanzo: Mwananchi.
 
Wizi mtupu, hivi mpaka vyombo vyote vya habari vinakwenda hewani kweli hakuna hata kimoja kilichopewa hiyo habari mpya ya kufuta hati ya kukamatwa mpaka siku ya pili????? Serikali corrupt, system corrupt!!!!!! Ndio maana Polisi wanauwa raia wema halafu wanaendelea kula kuku mtaani.
 
I don't know what the key to success is, but the key to failure is trying to please everyone
 
Sishangai na nilitegemea muujiza kujitokeza katika kumuepusha Chenge au mzee wa Vijisenti na aibu ya kushikwa na polisi. Wanasheria naomba mtusaidie, hivi kesi ikashahairishwa na hakimu kuamka kitini, inawezekana akarudi tena mahakamani tena kwa kuombwa na MSHITAKIWA...???

Je, hakimu akishatoa amri, huwa inageuzwa baada ya kesi iliyoamua kuahirishwa au inageuzwa baada ya siku iliyopangwa kesi kusikilizwa tena..?? Je hakimu akiamua mtu ashikwe, je, kuacha vigezo vya dhamana alivyotoa, kuna sheria inayomruhusu hakimu kugeuza maamuzi kabla ya siku iliyopangwa kesi kusikilizwa tena...??

Naomba maoni...!!! Wanasheria plzzzzzzzzzzzzz....!!! Nchi imeoza kiasi kwamba unaweza tukana kabla ya kuomba ushauri. Naomba ushauri ili nitoe duku duku langu vizuri...!!!!
 
Kishazi kwa Tanzania hii yote yawezekana mradi tu uwe mwenzao
 
Kama alichelewa kufika mahakamani aliwezaje kumuona Jaji? Au walikutana C*h*o*o*n*i? Je, siku ya tatu leo kwa nini Chenge hakukamatwa huko aliko? JK hii ni mizoga yako .... ...... ......
 
May be ule usemi wa kwamba "...Hakuna aliye juu ya sheria....." ni feki, (a.k.a wakichina). Ninaomba ufutwe mara moja
 
Hizo hasira zetu tuzioneshe kwenye sanduku la kura hapo oktoba wakuu wangu.
Kuna vibudu wamekaa mahala ambapo sio pao
 
Back
Top Bottom