Mahakama yaamuru mke aachike kisa nyumba haina choo

Mahakama yaamuru mke aachike kisa nyumba haina choo

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,273
Reaction score
25,296

Mahakama kaskazini mwa India, imempa ruhusa mwanamke katika jimbo la Rajasthan ruhusa aachwe na mumewe, kwa sababu nyumba yao haina choo.

Wakili wa mke, alidai kuwa kwa vile mume hakumjengea choo ndani ya nyumba, katika miaka mitano ya ndoa, basi huo ni ukatili.

Jaji alisema kwenda kufanya haja nje ni kitu cha aibu, na ni kumuadhibu mwanamke, kukosa kumuweka mwanamke pahala salama anapokwenda haja.

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa karibu nusu ya watu nchini India, karibu watu milioni 600 hawana choo.

Mwaka uliopita mwanamke alikataa kuolewa na mwanamume mmoja katika jimbo la Uttar Pradesh baada ya mwanamume kukataa kujenga choo.

Chanzo: Muungwana
 
huku sisi tunasema nyumba choo bwana. nyumba ipo jamiiforums choo facebook..kwa wenzetu haipendezi unakatiza na kikopo chako cha maji kila mtu ajua mke wa flani sasa anaenda kunya...ni rahisi kumjadili mtu maana akitoka hiyo harufu anayoacha huko mtu anayefuata inabidi asubir nusu saa pilipili hazijawah kuwaacha hawa jamaa salama.
 
Mahakama haioni ni wajibu wa wote wawili kushirikiana kujenga hicho choo?
 
huku kwetu wahindi ndo maboss wakati kwao maisha ya ajabj
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom