Feedback
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 7,988
- 4,507
Asante Kiungani nafikiri kama Mtazamaji hataelewa maana ya kuwa organised hasa kwenye mambo ya siasa basi kuna tatizo, kwenye siasa kuwa organised ni pamoja na kutokubaliana na sheria zilizopo huwezi kila siku kwenda mahakamani kusikiliza kuahirisha kesi kama hawana ushahidi kesi ifutwe kama wana ushahidi kesi ianze kusikilizwa, Hongera Mbowe kwa kitendo hiki.Kwenda au kutokwenda mahakamani, siyo alama ya mtu kuwa organised au dis-organised.
Bila kujua any more facts beyond speculation za hapa JF, hivi hatuwezi kufikiri kuwa huo unaweza kuwa mpango wa kuliweka hili suala la Arusha kwenye headlines za ki-taifa na ki-mataifa tena?
Jaribu kufikiri, nini kitaleta muamsho mkubwa wa hili suala la Arusha katika kipindi hiki cha kuelekea Bunge la budget?
Jaribu kufikiri msisimko utakaokuwepo wakionyesha magazetini na TV, Mwenyekiti wa Chadema na Mkuu wa Kambi ya Upinzani akiwa kapigwa pingu na kushushwa kwenye karandinga Arusha?
Jaribu kufikiri nini kitakumbushia 'ahadi' za WM Pinda katika kushughulikia suala la Arusha, na kauli za majibu yake kwa Lema, na jitihada za Spika kuzima hoja hizo?
Jaribu kufikiri namna itakavyokoleza uzito wa suala la CCM/Chitanda Arusha, na kuwaamsha 'mbwa' waliolala?
Wakati mwingine katika nchi nyingi zenye sheria za ki-dhalimu (sisemi kuwa Tanzania ni mojawapo, lakini mwingine akisema sitampinga!), mara nyingi msuguano dhidi ya sheria unakuwa na uzito na muono mkubwa kuliko utii wa sheria hizo.
Angalia mifano ya South Africa, Zimbabwe, Malawi, Tunisia, Libya, Misri, Sudan, India (wakati wa Gandhi), USA (wakati wa MLK), Kenya (wakati wa Nyayo), India, Ireland (wakati wa NRA), Burma, Uganda, na kadhalika.