Mahakama yaamuru Mbowe akamatwe mara moja

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Makahama mjini Arusha imetoa arrest warrant ili Mh. Freeman Mbowe akamatwe. Mbowe hakuwepo mahakamani na wala mdhamini wake hakuwepo. Ndesamburo kaponea chupuchupu kutokana na mdhamini wake kuwasili mahakamani.

Dr. Slaa alikuwepo mwenyewe na Lema alikuwepo mwenyewe pia.

===========
UPDATES:

From AFP:

Tanzania judge urges arrest of opposition leader

A Tanzanian judge on Thursday urged police to execute an arrest warrant issued last week against the country's opposition leader in parliament, lawmaker Freeman Mbowe.

Mbowe, who is president of the main opposition Chadema party, and 18 others are being prosecuted in an Arusha court for conspiracy to commit an offence, unlawful assembly and rioting.

Judge Charles Magesa issued arrest warrants for Mbowe and six others on May 27 when they failed to appear in court for a hearing on their case, which has been repeatedly delayed.

Magesa withdrew the warrants for everyone but Mbowe after the others appeared in person or sent representatives to explain their failure to show up for the previous hearing.

"The arrest warrant has not been executed and (Mbowe) did not come to explain why he was absent," Magesa said at an open hearing on the case.

He then instructed "the police to ensure that he be arrested."

The charges stem from a January 5 opposition rally in Arusha that was dispursed violently by police where three people were killed by gunfire.

Chadema Secretary General Wilbrod Slaa, a loser in the country's October presidential election and a Chadema lawmaker face additional charges for demanding that President Jakaya Kikwete resign
 
Makahama mjini Arusha imetoa arrest warrant ili Mh. Freeman Mbowe akamatwe. Mbowe hakuwepo mahakamani na wala mdhamini wake hakuwepo. Ndesamburo kaponea chupuchupu kutokana na mdhamini wake kuwasili mahakamani.

Dr. Slaa alikuwepo mwenyewe na Lema alikuwepo mwenyewe pia.

Source Mkuu?
 
Walio karibu na Mhe. Mbowe watueleze kwanini yeye na mdhamini wake hawakufika Mahakamani leo? Hawakuwa na taarifa ya kesi kuwepo au nini basi?
 
mi sioni mantiki ya kukiuka amri halali ya mahakama ya kuitwa mahakamani, nadhan anatuambia na sisi wananchi wengine tufate nyayo zake
 
Sasa waliokuwepo wamesomewa mashitaka? Au ndo umeendelea uleule utaratibu wa kuahirisha kesi. Na kama hawajasomewa mashitaka, kulikuwa na umhimu gani Mbowe kuwepo? Raha ya mahakama ni kuona tu watuhumiwa wamefika kwenye kesi kila siku, kupoteza masaa kadhaa halafu kuambiwa kesi imeahirishwa?

Hizi sifa hizi za mahakama za Tanzania zina mwisho mbaya hizi. Kila siku ukienda mahakamani unatajiwa tarehe, kesi haisomwi, cha ajabu siku ukishinda ndo wanatoa warrant ya kukamatwa hata kama kesi hawajaisoma.

Aibu kwa mahakama zetu za bongo na jaji mkuu wake.
 
Huyu ndio kiongozi Mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni, halafu ndio Mwenyekiti wa Chadema Taifa, anakuwa muhuni hivi je raia wa kawaida watakuje? Mbowe ebu heshimu sheria ya nchi, mambo yako ya kihuni peleka huko Bilicanas
 
kesi yenyewe haina kichwa wala miguu, hongera Mbowe kutokuhuduria, Endelea na majukum yako makubwa tuliokupatia
pia nimefurahishwa na bajeti ya kampi ya upinzani... jiandae na bunge bana

hakimu mwenyewe na hao waendesha mashitaka sina imani nao
 
mi sioni mantiki ya kukiuka amri halali ya mahakama ya kuitwa mahakamani, nadhan anatuambia na sisi wananchi wengine tufate nyayo zake
Mdhamini wake alipopigiwa simu alisema ameshikwa na tumbo la kuharisha....na ndiyo aliekuwa anatakiwa kumwakilisha na kwa bahati mbaya tarehe 27.5 siku ambayo alitakiwa pia nae alikuwa na kesi sehemu nyingine inayo inahusiana na issue ya uchaguzi, hivyo alichelewa kufika mahakamani na kukuta hati ya kukamatwa Mh Mbowe imeshatolewa, na siku ya leo ndiyo hivyo tena anaumwa....

Ngoja tusubiri kumuona kamanda wa anga akiwa amevishwa pingu....
 
Mimi hapa sijaelewa kitu, yaani Mbowe aache kazi za manufaa kwa ili aende kusikiliza hakimu anavyohairisha kesi mpaka tarehe nyingine? hawa wapumbavu hawajui kwamba bunge linataka kuanza! kwani wakili si alikuwapo mahakamani?
 
Huyu ndio kiongozi Mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni, halafu ndio Mwenyekiti wa Chadema Taifa, anakuwa muhuni hivi je raia wa kawaida watakuje? Mbowe ebu heshimu sheria ya nchi, mambo yako ya kihuni peleka huko Bilicanas
Mhuni atakuwa JK anayeshindwa kuwa kamata mafisadi wa ukweli anaanza porojo tyu ooh siwajui Richmond ohh hawani hii taji....matokeo yake ana anamfunga alieiba bil 1.8, huku alie iba bilion 40 anadunda mitaani...
 
Mimi hapa sijaelewa kitu, yaani Mbowe aache kazi za manufaa kwa ili aende kusikiliza hakimu anavyohairisha kesi mpaka tarehe nyingine? hawa wapumbavu hawajui kwamba bunge linataka kuanza! kwani wakili si alikuwapo mahakamani? nyoko zao.
Mkuu, Mbowe siyo lazima afika afike ila kilicho takiwa ni mdhamini wake afike badala yake nakuieleza mahakama kilicho mfanya asifike kama taratibu zinavyotaka.....
 
Mie nilidhani hizi hati za kukamatwa zinafanya kazi nchi nzima? maana Mbowe yuko Dar na anaendelea na majukumu yake au mpaka akifika Arusha ndio anakamatwa. Juzi tuliona Polisi wakimfata Slaa Mahakamani na eti kumwambia "mzee hebu inuka utufuate Polisi" Dr akawashtukia na kugoma.
 
Back
Top Bottom