Mahakama ya wananchi

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,313
12,613
Hakuna ubishi kuwa wanasheria wanatafuta ukweli kuhusu mambo yaliyofanywa na kufanyiwa wateja wao ambao sisi wananchi wa kawaida tunaufahamu. Tunaufahamu ukweli wote kwakuwa wahalifu na waliofanyiwa uhalifu ni miongoni mwa sisi wananchi ambao tunaishi, kucheza, kusoma, kula, fanyakazi, ama kulala nao huku mitaani, vyumbani, maofisini au mashuleni.

Ingawa hatuna elimu ya sheria, lakini miongoni mwetu tunaufahamu ukweli wa kila tukio linalotokea sehemu zetu tunamoishi na kufanya kazi. Ni bahati mbaya tu kwamba pamoja na kuufahamu ukweli wa kila jambo na kila tukio lakini wengi wetu hatupendi kushiriki katika kuwapa wanasheria na vyombo rasmi ukweli huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo zile za:
1. Jamaa atapata matatizo ukweli ukifahamika
2. Faida gani nipatapa kwa kuutoa ukweli kuhusu ukweli unaotafutwa na wanasheria/serikali
3. Nikifahamika nimeutoa ukweli nitakuwa hatarini
4. Usumbufu wa kwenda kuutoa ukweli
5. Garama za kwenda kutoa ukweli
6. Mila na desturi zetu zinatutaka zinakataza

Wananchi wenzangu tusiokuwa na taaluma ya sheria, polisi wala vyeo kwenye serikali tunaweza kuunda mahakama yetu hapa jf ya kuwahukumu na kuwatetea watu wote wanaotuhumiwa kufanya makosa mabalimbali kwakuwa miongoni mwetu tunafahamu kila mtu na kila tukio linalotoa na linavyotokea na wahusika wa tukio.

Leo kwenye mahakama hii ya wananchi wa kawaida kabisa hebu tumhukumu Mh. Freeman Aikael Mbowe kwa uwazi kabisa kwakuwa miongoni mwetu tunamfahamu zaidi kuliko wanasheria na serikali wanavyomfamu kwakuwa sisi tunaishi, tunakula, tunalala, tunakunywa na kufanyakazi nae 24/7.

NI kweli Freem Mbowe ni gaidi? na kwanini sio gaidi?
 
Back
Top Bottom