Mahakama ya rufaa yaiamuru TANESCO iwalipe DOWANS

Mahakama ya rufaa yaiamuru TANESCO iwalipe DOWANS

Fikra kama hizi zako ndio zilizosababisha tozo kuongezeka kutoka USD mil 58 mpaka USD mil 122. Mijadala ingefanyika sanely, dowans wangekuwa wameshalipwa na sasa tungebaki tunajadili nani wa kumuadhibu.

Jifunzeni busara inayosema "the fox must be chased away before the chicken is warned not to go into the bush"

Sawa, tujadiri basi nani wakuadhibiwa. Who is dowans by the way?
 
Kwako usd mil 58 zilikuwa kidogo na uliona inafaa serikali yako kupitia tanesco walipe kampuni hewa?

Hapo umeanza kuongea kama uko kweye kikao cha bavicha. Kampuni hewa haiwezi kushinda kesi ICC wala kwenye mahakama ya rufaa ya JMT.
 
Sawa, tujadiri basi nani wakuadhibiwa. Who is dowans by way?

Huwezi kujadili mtu wa kumuadhibu kabla hujatekeleza adhabu. Na hili ndio kosa lililofanyika from the start.

Tulipe deni kwanza. Then tuanza kuprobe wa kumuadhibu.
 
Tuwalipe fasta, tujipange upya. Ni matokeo ya utendaji uliojaa rushwa, so tukubali uchungu huu
 
Umekataa kununua mitambo ukapigwa fine ya mil. 58. Umekataa kulipa kwa sababu za kisiasa sasa hivi imefika mil 122. Bado unaendeleza ubishi.

Sijui unataka Mungu akutumie malaika wa kuiamsha saneness yako ili ujue kuwa kadri unavyozidi kupoliticise swala hili la kisheria ndivyo unavyozidi kuingia gharama zaidi!!!

Aliyekataa nani kama si tricks za magamba kuona ubishi ungewapa faida zaidi? Mangapi wamefanya kwa kurazimisha hata kama hayanafaida kwa wengi ila kwa interest za chama chao? Kilichoshindikana kwa hili nini kama ingekuwa faida kwa wa tanzania. Watwambie dowans ni nani?
 
Hapo umeanza kuongea kama uko kweye kikao cha bavicha. Kampuni hewa haiwezi kushinda kesi ICC wala kwenye mahakama ya rufaa ya JMT.

Ungekuwa ume-refer nini alichosema rais wako akiwa Dodoma in sametime April two years (if not one) ago ningekuona wa maana. Sorry mara zote nimekwepa mijadara yako humu jf na sijui nini kimetokea leo.


Wishing you a good sundy
 
Chanzo cha haya mambo ni UBISHI na tabia ya kupinga kila jambo linalosemwa na watu fulani.USHABIKI umeshamiri kwenye mambo ya kitaalam ya sheria, gharama zake ndio hizi...
Hujajibu swali ni wa chama gani?
 
Ni vigumu kujua. Siku hizi watu wana kadi za vyama mbalimbali. Mtu anaweza kuwa katibu wa chama kimoja lakini vilevile ni mwanachama wa chama kingine.
Mimi nimekuuliza kwenye sakata hili la dowans na richmond ni viongozi wa chama gani wanaohusika na hii kasha usilete majibu ya kitoto.
 
Mimi nimekuuliza kwenye sakata hili la dowans na richmond ni viongozi wa chama gani wanaohusika na hii kasha usilete majibu ya kitoto.

Wewe ndio unauliza kama mtoto.

Jambo limeamuliwa na Bunge halafu unauliza maswala ya chama.

Bunge ni la JMT sio la chama.
 
Tambo za Sitta, Dk. Mwakyembe zashindwa kunusuru TANESCO
• Ushauri wao waineemesha Dowans, yazoa mabilioni mara dufu

na Mwandishi wetu
Tanzania Daima


BAADA ya Kampuni ya Dowans kuibwaga TANESCO na kustahili kulipwa mabilioni ya fedha mara mbili kuliko ilizopaswa kulipwa awali, wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kisheria wamelaumu wanasiasa na wanasheria maarufu waliosababisha hasara hiyo.

Kosa kuu lililosababisha shauri lililozaa hukumu hiyo ni TANESCO kuvunja mkataba kinyume na makubaliano, na kuchelewa kutekeleza uamuzi wa mahakama wa kuilipa Dowans, hatua ambayo imegharimu taifa dola za Kimarekani za ziada milioni 58.

Kama uamuzi wa awali wa mahakama ungezingatiwa, Dowans ilistahili kulipwa dola za Kimarekani bilioni 65. Sasa italipwa dola za Kimarekani bilioni 122.

Miongoni mwa wanaolaumiwa ni mawaziri waandamizi Samuel Sitta na Dk. Harrison Mwakyembe, na Rais Jakaya Kikwete, ambao kwa sababu za kisiasa, hasa vita ya makundi ndani ya CCM, waliigomesha TANESCO kulipa deni hilo wakiogopa kelele za upinzani, na wakiitumia kama kete ya kukomoa washindani wao ndani ya chama.

Wengine wanaolaumiwa ni wanasheria wa serikali walioiingiza TANESCO katika mkataba na Dowans, na kuweka vifungu vya kujifunga iwapo mkataba ungevunjwa.

Baadhi ya wanasiasa na wanasheria hao ndio walioshinikiza mkataba uvunjwe, halafu baadhi yao wakawa watetezi kwenye kesi hiyo na kuzoa mabilioni mengine ya fedha.

Kosa la akina Sitta na Mwakyembe kwa mujibu wa wachambuzi, ni kushinikiza mkataba uvunjwe kinyume na sheria, na kutamba kuwa wangeitetea serikali, halafu wakaitosa.

Baadhi ya wachambuzi wamefika mahali na kusema wanasiasa hao walitumia fursa hiyo kumtisha rais na kumgombanisha na marafiki zake, naye akawazawadia uwaziri katika serikali yake ili kuwaziba midomo.

Katika uamuzi wa awali uliotolewa Novemba 15, 2011, Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen na wasuluhihi Swithin Munyantwali, Jonathan Parker uliamuru TANESCO kuilipa Dowans fidia ya dola za Marekani 65,812,630.03 kutokana na kuvunja mkataba kinyume na sheria.

TANESCO kwa upande wake haikuridhika na hukumu hiyo, badala yake ilitekeleza kusudio lake la kukata rufaa kuipinga.

Msingi wa uamuzi huo, ulitokana na hoja kwamba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam haina mamlaka kisheria kusimamisha utekelezaji wa malipo hayo baada ya hukumu ya ICC na jambo hilo lilionywa mapema na baadhi ya wataalamu wa fani ya sheria kabla TANESCO haijakata rufaa, lakini ushauri huo ukapuuzwa na baadhi ya wanasiasa na wanasheria.

Jopo la wasuluhishi liliamuru zaidi ya sh bilioni 36 (dola za Marekani 24,168,343) na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka inayofikia kiasi cha zaidi ya sh bilioni 26 (dola za Marekani 19,995,626) tangu Juni 15, 2010 hadi fidia hiyo itakapolipwa.

Pia jopo hilo la wasuluhishi wa migogoro ya kibiashara liliamuru sh bilioni 60 (sawa na dola za Kimarekani 39,935,765) na riba ya kiasi cha asilimia 7.5 ambayo ni sawa na sh bilioni 55 (dola za Marekani 36,705,013.94) zilipwe kuanzia Juni 15, 2010 hadi wakati wa malipo.

Jopo hilo lilisisitiza kuwa ada na gharama za wasuluhishi na za utawala sh bilioni moja (dola za Marekani 750,000) kwa wasuluhishi wa ICC zilitakiwa zilipwe na pande zote husika yaani TANESCO na Dowans.

TANESCO wanatakiwa kumlipa mdai (mlalamikaji) sh bilioni 3 (dola 1,708, 521) ikiwa ni gharama za uendeshaji wa kesi na gharama zingine.

Pamoja na uamuzi huo wa mahakama, walijitokeza wanasiasa waliosema wamebobea katika sheria, ambao walishinikiza mkataba uvunjwe na kuwa taifa lisingepata hasara na hivyo kushinikiza Dowans isilipwe.

Kati ya watu waliowahi kushauri kuwa TANESCO isilipe Dowans kiasi hicho cha awali cha fedha, yaani dola za Kimarekani bilioni 65, ni Waziri wa Afrika Mashariki, Sitta na Waziri wa Uchukuzi Dk. Mwakyembe.

Viongozi hao kwa nyakati mbalimbali walinukuliwa wakisema Dowans ni genge la wahuni, wasilipwe huku wakiogopa kuwataja kwa majina.

Na sasa TANESCO itabidi iendeshwe kwa hasara ili kulipa deni kubwa zaidi baada ya kushindwa mahakamani.

Taarifa rasmi ya kifedha ya TANESCO inaonesha kuwa hata kama shirika hilo lingeamua lisilipe mishahara wala lisifanye matengenezo ya mitambo, lisinunue vifaa vya kuunganishia wateja au lisiingie gharama nyingine zozote, bado lingepata hasara ya karibu sh bilioni 90.

Shirika linaloendeshwa kwa hasara ya mabilioni hayo sasa linadaiwa kulipa dola za Kimarekani zaidi ya milioni 122.

Suala la malipo ya Dowans lilileta mgongano katika vikao hata ndani ya Baraza la Mawaziri. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa taarifa kutoka ndani ya kikao kimoja zilimkariri Jaji Mkuu Fredrick Werema akieleza kushangazwa na hatua ya Sitta kumshambulia yeye na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, huku akijua kuwa walichokifanya kilikuwa kinagusa moja kwa moja mamlaka yao.

Jaji Werema alikaririwa akimweleza Waziri Sitta kwamba iwapo kweli alikuwa ana uchungu na suala la Dowans, basi wakati kesi ikiendelea alipaswa kuisaidia serikali katika kuwasilisha utetezi dhidi ya malalamiko 17 yaliyokuwa yamewasilishwa na kampuni hiyo.

Habari zilieleza kwamba hatua ya Sitta, ambaye alikuwa akitambua fika namna kesi hiyo ilivyokuwa ikiendelea kutochangia jambo lolote wakati shauri hilo likiwa ICC na badala yake kusubiri hadi serikali ishindwe ndipo aanze kutoa matamshi katika vyombo vya habari ilikuwa ni ya kuchochea hasira za wananchi dhidi ya viongozi.

Kwa mujibu wa Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, Waziri Ngeleja wakati huo kwa mamlaka aliyokuwa nayo kama waziri mwenye dhamana na masuala ya nishati, alikuwa na mamlaka ya kutoa tamko alilotoa baada ya kufanya mashauriano na wataalamu mbalimbali wa masuala ya sheria serikalini.

Licha ya Sitta kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kusema kuwa Dowans ni genge la wahuni, hajawahi kuwataja kwa majina ingawa muda wote wananchi wamekuwa wakiilalamikia serikali kwa kutaka kulilipa shirika ambalo mmiliki wake hakuwekwa wazi.

Waziri Mwakyembe naye alinukuliwa akisema; "Nikiwa mwanasheria ninasubiri kwa hamu maazimio ya Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) yasajiliwe Mahakama Kuu ili kuona maamuzi ya kuilipa Dowans yalifikiwaje, nataka kujua msingi wa tapeli kulipwa fidia kwa utapeli wake."

Licha ya kauli hiyo, tangu shirika hilo lianze kugaragazwa mahakamani hadi sasa linapopaswa kulipa fidia, hakuna Mwakyembe wala Sitta au wanasheria wowote waliosaidia ili serikali isiingie hasara kwa kulipa shirika hilo.

Baada ya uamuzi huo wa ICC, suala hilo lilifikishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ambaye alitoa ushauri kwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, wa kukubali serikali kuilipa Dowans endapo uamuzi wa ICC ungesajiliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Lakini Dk. Mwakyembe aliungana na Sitta kupinga Dowans kulipwa kiasi hicho cha fedha.

Akifafanua kuhusu msimamo wake wa kitaalamu, ambao alisisitiza ni tofauti na wa kisiasa, Dk. Mwakyembe alisema alikuwa na shauku ya kujua ni kwa namna gani serikali imepoteza kirahisi kesi hiyo, ambayo alisema hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa digrii ya sheria angeweza kuisimamia na kushinda.

Alisema kamati teule ya Bunge ilimaliza kazi kwa kutoa maazimio kadhaa, ambayo hadi sasa hakuna lililofutwa, na moja ya maazimio hayo ni kuiona Richmond ni kampuni hewa, hivyo kupendekeza ifutwe kwenye orodha ya kampuni za Tanzania na Oktoba, 2008 ilifutwa rasmi.

Mwakyembe ambaye pia ni mwanasheria aliyebobea na ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati iliyotoa ripoti yenye kuonyesha kuwa Dowans haikuwa kampuni halali, alisema anasubiri kuona ICC ilimuonaje mmiliki wa Dowans Holdings SA, iliyosajiliwa nchini Costa Rica, ambako serikali ya nchi hiyo ilisema haimtambui kwa kuwa hana anuani wala ofisi.

"Kwenye kamati tulifanya utafiti wa kina na serikali ya Costa Rica ilitueleza mmiliki wa kampuni hiyo hajulikani kwa jina, ofisi, anuani ya posta wala namba za simu," alisema Mwakyembe wakati akisoma ripoti ya kamati teule ya Bunge kuhusu Richmond.

Alisema kuwa walichoambulia Costa Rica ni kutajwa jina la Bernal Zamora Arse, anayemiliki kampuni takriban 100 zenye kuishia na SA, lakini hazielezi zipo jengo gani, nyumba ama kumiliki gari au pikipiki.

Kwamba kutokana na ukweli huo, anashangazwa kuona uamuzi wa ICC ulivyofikiwa na kuhoji fedha hizo zitalipwa kwa nani.

Dk. Mwakyembe alisema anasubiri uamuzi huo usajiliwe ili apate fursa ya kuupitia kwa kina na kuoana hatua za kuchukua kama mwanasheria.

Vile vile, Mwakyembe alinukuliwa tena ilipoibuka hoja ya kununua mitambo ya Dowans, Machi 25, 2009, akisema: "Dowans hatuna mkataba nao. Wametushtaki Mahakama ya Usuluhishi Ufaransa. Mitambo yao ni chakavu na ni kinyume na sheria kununua mitambo chakavu."

Alisema suala la Dowans liliisha zamani ndani ya Bunge, lakini wanaotaka kulifufua wanaweza kulipeleka bungeni. "Dowans italetwa bungeni, tutaikataa…wengine wanafikiri ni Mwakyembe peke yangu…sheria ipo."

Wengine wanaotajwa kuwapo katika harakati hizo kiasi cha kujitolea kupambana kisheria ili Dowans ama isilipwe au malipo yapunguzwe ni Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono.

Mkono aliwahi kuiwakilisha Tanzania katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi dhidi ya kesi iliyofunguliwa na Kampuni ya City Water, iliyoshindwa kutekeleza mkataba wake wa kusambaza hudumu ya maji safi Dar es Salaam na mkataba wake kuvunjwa, baada ya uamuzi wa Baraza la Mawaziri, chini ya Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Mbali na Mkono, mwingine aliyeshiriki kuzungumzia suala la malipo kwa Dowans katika wigo wa kisheria ni aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa zamani, Andrew Chenge, ambaye wakati wa Awamu ya Tatu, nchi iliingia mikataba mingi yenye utata.

Hata hivyo, katika kumsaidia Waziri Ngeleja kwenye msimamo wa kuilipa Dowans, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alieleza kuwa; kitendo cha kupishana kauli kati ya Sitta na Ngeleja kilitokana na ugeni katika kazi za uwaziri.

Mwingine aliyejitosa katika mjadala huo ni aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, John Chiligati, ambaye pia alishindwa kusimamia msimamo wake hadi akaambiwa ametia chumvi hasa mtazamo au hisia binafsi tamko la kikao cha Kamati Kuu kuhusu sakata la Dowans.

Chumvi anayotajwa kuikoleza Chiligati ni kutokana na kudai kwake kuwa Kamati Kuu "imebariki" malipo kwa Dowans.

Lakini muda mfupi baadaye Makamu Mwenyekiti wa CCM mstaafu Bara, Pius Msekwa alinukuliwa akisema: "Kama ilivyopendekezwa zichukuliwe hatua za kisheria na si kuchukua hatua za kulipa, huo ndiyo msimamo wa sasa wa chama."

Hatua hiyo inakuja baada ya uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani kukubaliana na hoja za pingamizi la wakili wa Dowans, Kennedy Fungamtama kuwa maombi ya TANESCO kupinga kulipa fidia za kuvunja mkataba yaliwasilishwa nje ya muda.

Hili ni pigo kubwa kwa baadhi wanasiasa waliokataa Dowans isilipwe na wanasheria waliotumia vibaya taaluma zao kuishauri serikali, na hivyo kuwabebesha mzigo Watanzania.

Kufuatia Mahakama ya Rufani kutupilia mbali maombi ya TANESCO kuzuia utekelezaji wa hukumu ya Mahakama Kuu iliyoiamuru iilipe fidia Dowans, deni hilo limeongezeka mara dufu.

Kwa sasa TANESCO italazimika kuilipa Dowans zaidi ya sh. bilioni 122 za awali kwa kuvunja mkataba kinyume cha sheria.

Lakini kwa kukaidi amri ya mahakama na kusikiliza ushauri wa wanasiasa na wanasheria waliolazimisha mkataba huo uvunjwe na isilipwe, kesi hiyo imechukua muda mrefu mahakamani, na hivyo kusababisha ongezeko la deni kwa dola bilioni 58 nyingine za Kimarekani.

Hizo ni gharama zilizotokana na ongezeko lililosababishwa na TANESCO kugoma kulipa deni mara baada ya uamuzi wa awali wa mahakama. Hazujumuishi gharama za uendeshaji wa kesi.

Sababu kubwa iliyotajwa na Mahakama ya Rufaa kutupitilia mbali maombi ya TANESCO ni kuwa maombi ya rufaa yaliletwa nje ya muda unaotakiwa, huku wanasheria wa TANESCO wakilaumu Mahakama Kuu kuwa ndiyo ilichelewa kuwapatia nakala ya hukumu ili waweze kukata rufaa.
 
Dowans walitakiwa kulipwa sawa na $65 million sasa article inadai kutokana na kuchelewa kulipwa kwa deni, riba imeongeza deni kwa $58 million kwa maana hiyo deni halisi kwa sasa ni $123 million ukiweka exchange rate ya $1 to Tshs 1,500 (sidhani hii kama ni accurate kwa conversion rate ya leo au hata ya jana) pesa zitakazolipwa kwa pesa za madafu ni sawa na Tshs 184,500,000,000.

Daily News | CCM against Dowans' award

mbona ndogo?
 
Umekataa kununua mitambo ukapigwa fine ya mil. 58. Umekataa kulipa kwa sababu za kisiasa sasa hivi imefika mil 122. Bado unaendeleza ubishi. Sijui unataka Mungu akutumie malaika wa kuiamsha saneness yako ili ujue kuwa kadri unavyozidi kupoliticise swala hili la kisheria ndivyo unavyozidi kuingia gharama zaidi!!!
Suala la kisheria kwa Kampuni Hewa Vs TANESCO? Hata haiingii akilini!
 
Wanabodi,
Sisi wengine tulisema tangu mwanzi kuwa hili la Dowans, halikwepeki!, tulinyooshewa vidole hadi kutukanwa kuwa hatuna uzalendo!. Wajameni, dawa ya deni ni kulipa tuu!.

Niwakumbushe kidogo mlolongo mzima na mwisho wa siku, deni litalipwa!.

  1. Game lilianza rasmi 1995 baada JK na EL kutoswa kwenye urais, wakaunganisha nguvu, "stand together, fight together", as one, hivyo kuunda rasmi mtandao!. The Master Mind was "The King Maker!"
  2. Tangu mwanzo the plan was JK rais, EL, PM!, ndani ya mtandao kuna watu "safi" wakadai EL ni "too dirty", hivyo wakampendekeza 6 ndie awe PM!.
  3. Baada ya ushindi wa kishindo wa JK, he had no option bali kusikiliza zile sauti za "who paid the piper, had to call the tune!", na kwa kusingatia walipoamzisha Boys II Men tangu 1995, JK akakumbuka fadhila, akamuimbua EL as PM!. 6 na wengine waliojiita "wasafi" waka mind!.
  4. The King Maker, akamng'oa Msekwa kwenye us Spika na kumzawadia 6 as consolation ya kuukosa u PM, wakijua yamekwisha!. Kumbe wapi!.
  5. Kulipotokea dili la umeme wa dharura, "Jamaa" mwenyewe alitia timu, ndipo Richmond ikazaliwa!, na baada ya koboronga, ndipo "The King Maker" akaokoa jahazi kwa kuileta "Dowans" ili ku save face ya "jamaa!", na kiukweli, Dowans walifua umeme kweli!.
  6. Kwa vile 6 bado alikuwa na usongo wa kuukosa u PM, na kumepatikana kiji opportunity cha kumfix EL, ili atoswe na yeye eteuliwe!. 6 kwa kumtumia Mwaki, wakatimiza lengo, tena kwa kuhakikisha EL hahojiwi wala kuulizwa chochote, bali kusukumiwa zigo zima zima just to save the face ya "Jamaa!", na El angekohoa, nyumba nzima ingeporomoka na wangekosa wote!.
  7. Ilimbidi EL kukubali matokeo na kuwapa walichotaka na yeye kujikalia kimya, pembeni!, na kuvumilia dhihaka, matukano, kubeswa na matusi ya kila aina!, na alivumilia yote, kama yule aliyewambwa msalabani!. Si wengi wanaoelewa ni kwa kuteswa kwake, CCM ilipona!.
  8. Ni kufuatia ripoti ile, mkataba halali wa Dowans ulisitishwa kwa sababu za kijinga kabisa!. ZZK kupitia kamati yake ya POC alishauri, kama tumevunja mkataba, bora basi tuinunue mitambo ile tuendelee kuzalisha umeme!, na kama hija za kuuvunja mkataba, ni kosa la Dowans, then, bora tuitaifishe mitambo ya Dowans, iwe mali ya umma!. Kwa mnao kumbuka, mtakumbuka waliopinga kwa nguvu zao zote!.
  9. Dowans wakafungua kesi ICC, wakashinda!, mkataba ukaletwa humu jf, watu tulipouona tuu tukasema wazi, hakuna pa kutokea!. Dawa ni kulipa the sooner the better!. Hatukulipa tukaendelea kudanganywa sasa deni limeongezeka mara dufu na lazima tulipe!.
  10. Tanzania ni nchi ya ajabu sana!, tunaviongozi wa akili za panzi kweli kweli!, Tumevunja mkataba wa Dowans, tumeingia mkataba ule ule na Simbion, kwa masharti yale yale ya Dowans!. Nunueni mashine basi muendelee kuzalisha umeme! eti "hatununui mashine kuu kuu!" na sasa tumepitisha sheria ya kununua mashine kuu kuu!. Wakati wote mitambo ya Dowans imezimwa, tuliwasha mitambo ya IPTL kwa gharama ya mara kumi ya mitambo ya Dowans!, na uchafuzi mkubwa wa mazingira on top of that!. Sasa hizi ni akili au matope?!.
  11. Sasa maandamu Tanesco wameamriwa rasmi kulipa!, na aliyeiponza Tanesco ni serikali, hivyo kiukweli, na hali halisi ilivyo sasa, Tanesco haina "capacity to pay!", hivyo deni litalipwa na serikali!, hii ikimaanisha fedha za kulipa deni hilo zitatokana na kodi zetu!, jiandaeni kufunga mikanda kwa kuongezwa gharama katika maeneo mbalimbali hadi fedha za kulipa Tozo ya Dowans zipatikane!.
  12. Pia namshauri EL, now its about time atoke to the open, aweke wazi his role kwenye Richmond, ili Watanzania wamjie who is the real beneficiary of "tozo ya Dowans!", kwa kuendelea kukaa kimya, "he has everything to loose and nothing to gain!" lakini kwa kumtaja sasa, "he'll have everthing to gain and nothing to loose!", kwa sababu, 2015, yeye sio mgombea!. He'll save his face, his party and his nation!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Jumapili Njema!.

Pasco.
Tozo ya Dowans imelipwa.
P
 
Na Flora Mwakasala

MAHAKAMA ya Rufaa imetupilia mbali ombi la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) la kusimamisha utekelezaji wa hukumu ya Mahakama Kuu, iliyoamuru wailipe Sh bilioni 94 kampuni ya Dowans.

Katika ombi hilo Tanesco walidai kuwa fedha hizo walizoamriwa kulipa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) kutokana b kukatisha mkataba kinyume cha sheria ni nyingi na hawana uwezo wa kulipa.

Aidha wanadaia kuwa, kama watatekeleza hukumu hiyo, itaathiri uwezo wake wa kuzalisha na kusambaza umeme nchini na hivyo kusababisha tatizo kubwa la ukosefu wa umeme, ambao utaathiri uchumi wa nchi kwa jumla.

Katika hoja zao, walidai kuwa tayari walishawasilisha nia ya kukata rufaa kupinga hukumu hiyo na ya Mahakama Kuu na wanaamini watashinda rufaa hiyo.

Akisoma uamuzi huo jana, Naibu Msajili wa mahakama hiyo Elizabeth Mkwizu, alitupa ombi hilo na kuiamuru kwa kuwa waliwasilisha ombi hilo nje ya muda unaotakiwa kisheria.

Mahakama hiyo ilikubaliana na hoja za Wakili wa Dowans Kennedy Fungamtama aliyedai ombi hilo lilipaswa liwasilishwe katika muda wa siku 60 tangu kutolewa kwa hukumu, lakini badala yake Tanesco iliwasilisha maombi hayo baada ya siku 351.

Septemba 28, mwaka juzi, Mahakama Kuu iliiamuru Tanesco kuilipa Dowans fidia ya Sh biloni 94 na riba ya asilimia 7.5 baada ya kukubali kuisajili tuzo ya Dowanc.

Katika hukumu ya Mahakama ya ICC, iliyotolewa Novemba 15 mwaka juzi, Tanesco iliamriwa kuilipa Dowans Holding SA na Dowans Tanzania Ltd (Dowans) dola za Marekani milioni 65, pamoja na riba na gharama za kuendesha kesi, baada ya kuvunja mkataba na kampuni hiyo kinyume cha sheria.

Hata hivyo, Tanesco ilipinga hukumu hiyo lakini Septemba 28 mwaka jana, Jaji Emilian Mushi wa Mahakama Kuu, alikubali kusajili tuzo ya malipo ya Dowans na kuiamuru Tanesco kulipa fedha hizo pamoja na gharama za uendeshaji kesi.

Baada ya hukumu hiyo Tanesco iliwasilisha ombi la kibali cha kukata rufaa kupinga hukumu hiyo na ombi la kusimamisha utekelezwaji wa hukumu hiyo.

Hata hivyo Februari 20, mwaka jana , Mahakama ilitupilia mbali ombi la kibali cha kukata rufaa na Septemba 6, 2012, pia mahakama hiyo ilitupilia mbali ombi la kusimamisha utekelezwaji wa hukumu hiyo.

Kutokana na uamuzi huo, ndipo Tanesco wakafungua ombi la kusitisha utekelezaji wa hukumu hiyo katika Mahakama ya Rufaa, huku wakitoa hoja walizozitoa katika ombi la Mahakama Kuu.

Kwa mujibu wa Wakili wa Dowans, Kenedy Fungamtama, hadi kufikia Novemba mwaka jana, deni la Dowans lilifikia zaidi ya Sh bilioni 122 kutokana na kuongezeka kwa riba ya asilimia 7.5 ya deni la awali la kila siku.

Mwisho.
Acha kutukumbusha ufisadi wa awamu ya nne.
 
Ni wakati wa wahuni kutesa.

Tunawakumbusha jinai haifi. Watailipa hii gharama, kama si wao basi vizazi vyao.

Mafisadi, wauza madawa ya kulevya na wasiopenda haki wote tutawashughulikia siku moja.

RIP Magufuli, tunaamini ipo siku tutapata kiongozi wa kweli kama ulivyokuwa.
 
Back
Top Bottom